Privadinho amjibu Jemedari Said kuhusu kumpigia makofi Engineer Hersi ikulu wakati akiwa anaingia

Privadinho amjibu Jemedari Said kuhusu kumpigia makofi Engineer Hersi ikulu wakati akiwa anaingia

political monger senior

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2020
Posts
1,827
Reaction score
5,994
NI KWELI NILIMWAMBIA JEMEDARI APIGE WAKATI RAIS WA YANGA ANAPITA?

Nilimwambia kwa sababu niliona amekaa kimya wakati ukumbi mzima unampongeza @caamil_88

Kimsingi alikosa heshima kwa Rais wa Yanga.

Tujiulize alikwenda Ikulu kwa sababu zipi? Lets assume hamkubali Hersi kwa sababu zake binafsi, je hajui Hersi ndiye aliyempeleka Ikulu?

Kilichosababisha yeye aalikwe Ikulu ni klabu ya Yanga ambayo ipo chini ya Uongozi wa Hersi Said. Ukipenda boga basi penda na boga lake.

Je mafanikio haya ya Yanga unaweza kumtenganisha na Hersi?.

Nilitegemea awe proud na namna ambavyo vijana kwa hivi sasa wameshika hatamu kwenye soka la AFRIKA

Wakati Dr Motsepe anachaguliwa kuwa Rais wa CAF akaweka kijana wake mwenye miaka 32 tu

@football_senzo 2010 akiwa na miaka 31 pekee aliteuliwa kuwa makamu M/Kiti wa maandalizi ya kombe la dunia. Baadae 2011 akateuliwa kuwa Meneja Orlando Pirates na Platnumz stars. Na amefanya makubwa

2012 Raja Casablanca ilimchagua Mohamed Boudrika akiwa na umri wa miaka 28 na kuweka rekodi ya kuwa Rais mdogo zaidi katika historia ya klabu hiyo iliyoongozwa na maraisi takriban 25 tokea mwaka 1948

Boss wa Orlando ni Irvin Khoza ambaye aliichukua klabu hiyo akiwa na miaka 43 pekee mwaka 1991 na mwaka 1995 klabu hiyo ikashinda ligi ya mabingwa Afrika kwa mara ya kwanza

Leo Eng Hersi akiwa hajafikisha miaka 40 amefika fainali ya Kombe la Shirikisho, ametwaa ubingwa wa ligi, amefanikisha mchakato wa mabadiliko. Je hastahili pongezi?

Au Jemedari anamchukia Injinia?

Uthubutu wa kumkosoa Injinia anao, lakini mshipa wa aibu wa kutambua mchango wa Injinia hana.

Hiyo sio sportsmanship.

Huwezi kuipongeza Yanga halafu unasema simpongezi Hersi.!

Rais wa Nchi Mama Samia anampongeza Hersi wewe huoni thamani hiyo ?

Shida yenu mnaamini kumpongeza Injinia ni uchawa ila kumkosoa ni ushujaa.

Very bad mentality.

All in all hakuna kitu kitapungua, kwa Hersi, ndio kwanza shughuli imeanza. Itakusumbua sana moyoni kaka. Itakutesa..Ameandika Privadinho.

1686222306712.jpg
 
Huyu Dogo siku hizi anajiona matawi sana,amesahau alianza kwa kuwa mfanyakazi kwenye instagram ya Shaffih Dauda.Amshukuru Dauda kumpa kazi then kumpa kazi ya bila mkataba pale clouds fm ndo akapata uwanja hadi akajulikana.
 
Ni kweli kwamba Injinia Hersi ni kiongozi mzuri, kijana safi mwenye maono na akili.
Pamoja na hayo, hiyari ya kumpigia makofi inabaki kuwa ni ya mtu mwenyewe. Hili halihitaji kulazimishana.
 
Kwahivyo Jemedar hatakiwi kwenda kuangalia Yanga dimbani ikicheza kisa hamkubali Hersi? Yanga ni Taasisi yenye kujishughulisha na mpira ambapo hata hapo Ikulu alifuata Taasisi ya Klabu ya Yanga kwa mwaliko wa Ikulu na hamkufuata Hersi

Acheni ujinga.
 
Huyu Dogo siku hizi anajiona matawi sana,amesahau alianza kwa kuwa mfanyakazi kwenye instagram ya Shaffih Dauda.Amshukuru Dauda kumpa kazi then kumpa kazi ya bila mkataba pale clouds fm ndo akapata uwanja hadi akajulikana.
Baada ya kutoa tunu ya Manhood ndo amekua hapo na hivyo alivyo sasa. Wala sio wa kumshangaa kabisa.

Ndo hulka inayomjia automatically, ila anashindwa kujizuia hata kwa kiasi lol.
 
Huyu Dogo siku hizi anajiona matawi sana,amesahau alianza kwa kuwa mfanyakazi kwenye instagram ya Shaffih Dauda.Amshukuru Dauda kumpa kazi then kumpa kazi ya bila mkataba pale clouds fm ndo akapata uwanja hadi akajulikana.
Ukishaona kijana tena wa kichagga kageuka kuwa chawa, muogope sana.Wanaume wa kichaga ni wapambanaji kwenye maisha,huyu Mrombo yeye kageuka kuwa chawa,kutwa kupiga mayowe kama Mwijaku.Warombo okoeni huyu dogo anawatieni aibu.
 
Kabisa ,mchaga anaetafuta hela kwa kuwa chawa.Halafu ans degree ya Law eti ,sijui ni kweli ?Kama ni kweli sijui kwa nini hakwendi Law school na pesa anayo ,walau amiliki Law firm akiwa wakili.
 
Back
Top Bottom