political monger senior
JF-Expert Member
- Nov 26, 2020
- 1,827
- 5,994
NI KWELI NILIMWAMBIA JEMEDARI APIGE WAKATI RAIS WA YANGA ANAPITA?
Nilimwambia kwa sababu niliona amekaa kimya wakati ukumbi mzima unampongeza @caamil_88
Kimsingi alikosa heshima kwa Rais wa Yanga.
Tujiulize alikwenda Ikulu kwa sababu zipi? Lets assume hamkubali Hersi kwa sababu zake binafsi, je hajui Hersi ndiye aliyempeleka Ikulu?
Kilichosababisha yeye aalikwe Ikulu ni klabu ya Yanga ambayo ipo chini ya Uongozi wa Hersi Said. Ukipenda boga basi penda na boga lake.
Je mafanikio haya ya Yanga unaweza kumtenganisha na Hersi?.
Nilitegemea awe proud na namna ambavyo vijana kwa hivi sasa wameshika hatamu kwenye soka la AFRIKA
Wakati Dr Motsepe anachaguliwa kuwa Rais wa CAF akaweka kijana wake mwenye miaka 32 tu
@football_senzo 2010 akiwa na miaka 31 pekee aliteuliwa kuwa makamu M/Kiti wa maandalizi ya kombe la dunia. Baadae 2011 akateuliwa kuwa Meneja Orlando Pirates na Platnumz stars. Na amefanya makubwa
2012 Raja Casablanca ilimchagua Mohamed Boudrika akiwa na umri wa miaka 28 na kuweka rekodi ya kuwa Rais mdogo zaidi katika historia ya klabu hiyo iliyoongozwa na maraisi takriban 25 tokea mwaka 1948
Boss wa Orlando ni Irvin Khoza ambaye aliichukua klabu hiyo akiwa na miaka 43 pekee mwaka 1991 na mwaka 1995 klabu hiyo ikashinda ligi ya mabingwa Afrika kwa mara ya kwanza
Leo Eng Hersi akiwa hajafikisha miaka 40 amefika fainali ya Kombe la Shirikisho, ametwaa ubingwa wa ligi, amefanikisha mchakato wa mabadiliko. Je hastahili pongezi?
Au Jemedari anamchukia Injinia?
Uthubutu wa kumkosoa Injinia anao, lakini mshipa wa aibu wa kutambua mchango wa Injinia hana.
Hiyo sio sportsmanship.
Huwezi kuipongeza Yanga halafu unasema simpongezi Hersi.!
Rais wa Nchi Mama Samia anampongeza Hersi wewe huoni thamani hiyo ?
Shida yenu mnaamini kumpongeza Injinia ni uchawa ila kumkosoa ni ushujaa.
Very bad mentality.
All in all hakuna kitu kitapungua, kwa Hersi, ndio kwanza shughuli imeanza. Itakusumbua sana moyoni kaka. Itakutesa..Ameandika Privadinho.