Fumbokhan
Member
- Jan 16, 2021
- 6
- 23
Priyanka Chopra(38) amesema yeye na mumewe Nick Jonas(28) bado hawana mtoto sababu yupo busy sana na kazi kutokana na mikataba aliyosaini hivyo inakuwa ngumu kwake kubeba mimba kwasasa lakini muda sahihi ukifika atabeba mimba kwakuwa yeye na Nick wana lengo la kuanzisha familia.
Priyanka amesema ndoa yao iliyofungwa 2018 ni muhimu sana kwao lakini bado kila mmoja anamhimiza mwenzie kufanya kazi kwa bidii. Ameongeza kuwa sababu wote mara nyingi wapo busy na kazi lakini ni lazima kila baada ya wiki mbili au tatu mmoja wapo amfuate mwenzie alipo wakaonane hata kama ni nje ya nchi kikazi lazima wakaonane kisha kila mmoja anaendelea na majukumu yake.
Priyanka aliwahi kusema kuwa sababu iliyomfanya amuone Nick kuwa ndiye mwanaume sahihi katika maisha yake ni kujivunia mafanikio aliyonayo huku akizidi kumpa moyo asonge mbele kwa bidii ya kazi afanikiwe zaidi.
Priyanka amesema wanaume aliowahi kuwa nao kabla walikuwa hawajiamini na hawakufurahia mafanikio yake sababu ya kuwa mwanamke na yeye hakutaka kubweteka hata wazazi wake walimlea na kumsomesha kwa bidii awe huru hata kipesa badala ya kutegemea mwanaume.
Nick na Priyanka wote kila mmoja ni milionea.