Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
- #21
Dudus,Sheikh Mohamed na wewe unasikiliza mambo ya kikafir? Sikutegemea statement kama hiyo kutoka kwako Mzee wetu.
Bahati mbaya sana kwako.
Kwani ulikuwa na picha gani yangu?
Hapakuwa na haja ya kuwatukana watu wenye imani nyingine kwa kuwaita ''makafiri.''
Ungeweza kuaandika hayo yote kwa adabu na ungeeleweka.
Nilijaaliwa kipaji cha muziki toka udogo wangu.
Baba yangu alikuwa na collection kubwa sana ya muziki wa nyakati zake hadi Ball Room Dancing.
Athari za ukoloni wa Waingereza.
Nimezaliwa nimeikuta hiyo maktaba.
Najua kupiga guitar, key board na naweza kuimba ingawa ni miaka mingi sana imepita.
Lakini huwa nasikiliza muziki ninapokuwa na wakati.
Nimepata kuwashangaza wengi pale ninaponyanyua guitar au ninapokaa nyuma ya piano ingawa niko ''rusty.''
Hii picha nimepiga nyumbani kwa Dr. Harith Ghassany Mascut mwaka wa 2015 lakini hapa alikuwa anajua kuwa mimi najua kupiga piano.
Mara yake ya kwanza kushagaa ilikuwa 1999 hapa hapa nyumbani kwake nilipompigia, ''Crying in the Chapel,'' yeye na mkewe.
Ilikuwa ndiyo siku ya kwanza tunakutana.