Prof. Ali Mazrui mwalimu wangu wa masafa marefu

Sheikh Mohamed na wewe unasikiliza mambo ya kikafir? Sikutegemea statement kama hiyo kutoka kwako Mzee wetu.
Dudus,
Bahati mbaya sana kwako.
Kwani ulikuwa na picha gani yangu?

Hapakuwa na haja ya kuwatukana watu wenye imani nyingine kwa kuwaita ''makafiri.''

Ungeweza kuaandika hayo yote kwa adabu na ungeeleweka.

Nilijaaliwa kipaji cha muziki toka udogo wangu.

Baba yangu alikuwa na collection kubwa sana ya muziki wa nyakati zake hadi Ball Room Dancing.

Athari za ukoloni wa Waingereza.

Nimezaliwa nimeikuta hiyo maktaba.

Najua kupiga guitar, key board na naweza kuimba ingawa ni miaka mingi sana imepita.

Lakini huwa nasikiliza muziki ninapokuwa na wakati.

Nimepata kuwashangaza wengi pale ninaponyanyua guitar au ninapokaa nyuma ya piano ingawa niko ''rusty.''

Hii picha nimepiga nyumbani kwa Dr. Harith Ghassany Mascut mwaka wa 2015 lakini hapa alikuwa anajua kuwa mimi najua kupiga piano.

Mara yake ya kwanza kushagaa ilikuwa 1999 hapa hapa nyumbani kwake nilipompigia, ''Crying in the Chapel,'' yeye na mkewe.

Ilikuwa ndiyo siku ya kwanza tunakutana.

 
Wazee wa takbir bana.
Wa kupuliza,
Unatoa hukumu haraka ukiwa unanihukumu kwa fikra zako utataabika.

Mimi ni huyo hapo chini nikiwa mwanafunzi Uingereza katika ujana wangu:



Hiyo picha hapo chini nilipiga nyumbani kwa Abdilatif Abdalla Humburg waka wa 2011, nilikuta mwanae ana guitar pale nyumbani.

Nilimfunza mwanae chords chache na nikapiga baadhi ya nyimbo ambazo bado nazikumbuka kama ''As Tears Go By,'' ya Rolling Stones.

Abdilatif alishangaa sana.

Ningependa kukufunza kitu.
Mimi si wa lugha hiyo ya ''bana'' na kejeli.

Kuwa na heshima andika kwa adabu tunaweza tukajadili mengi ambayo yatastawisha hii barza na tukafaidika sote, mimi, wewe na wengine.

Wanangu huangalia picha zangu za utotoni na wakaniuliza mengi kwa adabu kwa nia ya kutaka kunijua nami huwaeleza makuzi yangu.

 
The Boss,
Ahmed Rajab ni kaka kwangu, ndugu na rafiki.

Nimemtaja sehemu nyingi inabidi niingie Maktaba nianze kuchakura.

JF anaijua na angetaka angeshajiunga siku nyingi.
Mmmh, hapo sawa. Ahmed Rajab moto wa kuotea mbali. But not Mazrui, he is a nut, tungwita Farisayo.
 
Mmmh, hapo sawa. Ahmed Rajab moto wa kuotea mbali. But not Mazrui, he is a nut, tungwita Farisayo.

Mazrui was a nut? Nakushangaa sana wewe unaesema hivyo!!!!! Labda alikuwa na akili nyingi hata wazungu walimuheshimu.

Kwenye moja ya documentaries zake ‘The Africans: a triple heritage’ alieleza jinsi alivyokuwa promoted from lecturer to full professor bila ya kupitia zile hatua nyingine za chuo. Hata wenzake walishangaa.

Au unadhani akili nyingi wanazo wazungu tu?
 

Jecha, Mazrui ni kabila tu la waarabu kama vile ya huku bara. Mfano ukisema Mnyamwezi unajua anatoka Tabora.

Mazrui wa ‘Okello’ kama ninakumbuka vyema ni mzee wake Nassor Mazrui (iliwahi kuzungumziwa kwenye Zanzinet miaka kadhaa nyuma).

Nimejaribu kumtafuta yule aliyeandika ile makala sikufanikiwa.
 
Huwa nawachukia sana watu kama Nyie. Watu wanajadili masuala wewe unawatoa kwenye mada! Bakia tu na kazi ya kulamba nayo za watawala huku tuache tunataka kujifunza. Tuache bhana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…