Prof. Anangisye: Chuo Kikuu makini hakiwezi kuvumilia Wanataaluma wasiofanya Utafiti

Prof. Anangisye: Chuo Kikuu makini hakiwezi kuvumilia Wanataaluma wasiofanya Utafiti

Unafanyaje utafiti bila pesa, unakuta mtu kama huyu anakomaa na wanataaluma kwamba hawafanyi tafiti huku yeye na serikali yake hawajawahi kutoa hata senti tano kugharimia tafiti, yaani ni kuongea kujifurahisha tu......nafikiri tafiti za nchi hii zinafanyika pale mjengoni maana ndo pesa zinapomwagwa, chini ya watafiti wakuu msukuma na kibajaji...
 
Waanze na utafiti kwa nn vyoo vyao pale SE's karibu na Nkrumah vinaziba kila Mara.
 
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Prof. William Anangisye amesema Utafiti ni muhimu kwa maendeleo kwa Umma na ulimwengu wa ujumla akiongeza kupitia Tafiti hizo, Chuo vina wajibu wa kutatua changamoto zinazokabili jamii.

Ameeleza hayo Mei 24, 2021 katika Maadhimisho ya Sita ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu ambapo amesema Chuo Kikuu makini hakiwezi kuvumilia kuwa wa Wanataaluma wasiofanya Utafiti.

Amewanukuu Wanazuoni akisema, "Vyuo Vikuu bila shughuli za utafiti vina hatari ya kuwa na hadhi ya Shule za Sekondari"
Niice
 
Back
Top Bottom