Prof. Assad: Nikipigiwa simu kutoka juu ya maagizo, asubuhi yake nilikuwa naandika barua

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Mstaafu, Mussa Juma Assad, amesema katika kipindi chake cha utumishi alikuwa akipokea simu za maelekezo kutoka kwa baadhi ya watu wakimtaka asifanye maamuzi fulani, lakini mara nyingi alisimamia alichokiamini kuwa sahihi. “Unaweza ukapigiwa simu ‘ah usilifanye bwana’, na wewe ukasema ‘hapana, mimi hiki nitakifanya’, na mimi nilikuwa nikifanya hivyo,” alisema.

Aliongeza kuwa ilikuwa desturi yake kila alipopokea maelekezo ya namna hiyo, asubuhi yake aliandika barua rasmi kuweka kumbukumbu ya mazungumzo hayo na msimamo wake kuhusu suala husika.
Ndio maana yule shujaa wao alimfukuza kazi Kwa kuzuia ufisadi 😂😂
 
Serikali mpeni haki yake .

Ina maana hii Nchi haithamini maslai ya citizens Wake ?
 
Profesa anaongea sana, ni kama vile wenzake waliopita hawakufanya chochote na huyu tuliye naye hatimizi wajibu wake ipasavyo ila yeye tu ndiye aliyefanya kazi kubwa ya kusifiwa na ndiye anayefaa kwa kazi hiyo.
Hili si jambo jema kwa profesa kama yeye.
Ukishakuwa kiazi Bora usicomment. Hao wenzake hawakufanya kazi kwenye mazingira sawa na Assad.
Halafu hawakuondolewa kinyume na utaratibu kama Assad ndo maana anakwambia muda Wa kustaafu rasmi ulikuwa bado, na Kwa Sheria zetu ukishastaafu uCAG huruhusiwi kuwa mtumishi wa umma tena.
Sasa ulitaka baada ya pale Assad aende wapi?
 
Mkuu yeye anazungumza kipindi chake
 
Kwahiyo ataongea mpaka lini?
Huoni kama wewe ndiye kiazi kilichooza!!
Profesa unalalamika mpaka lini ili iweje sasa?
Nani asiyejua kuwa Magufuli amekiuka Katiba kumtengua CAG ?
Sasa yupo huyo Magufuli ili tumuwajibishe?
Tumia akili yako vizuri.
 
Mkuu yeye anazungumza kipindi chake
Sawa, lakini hili alishaongea mara nyingi.
Na jamii inajua kuwa Katiba imekiukwa.
Tugange yajayo.

Kama bado hajaridhika sheria iko wazi aingie kwenye siasa aje aliponye taifa.
 
Unaambiwa mwamba meza yake kwenye ofisi yake ya CAG alielekeza Makkah.

Yeye ni kati ya watanzania wachache maarufu wana uhakika wakifa wanabadilika na kuwa waarabu. Wenginiene ni Profesa Janabi, Profesa Abdullah Safari, mzee muhamed Said, Sheikh Mwaipopo, Sheikh Rusanyaga, maulid kitenge, Masoud Kipanya, Mwijaku, Malaria 2 na adriz
Hapa ndipo Watanzania wanafeli

Suala siyo meza wala kanzu yake. Je, hoja anazozitoa zina mashiko ?

Kwa mfano, kunywa chai ofisini mara baada ya kuingia ina mantiki? Kuna sababu gani za viongozi wanaopewa kila kitu bado wapewe chai ofisini

Profesa kasema hakuna kuoanisha kati ya performance na payment. Nchi zote zilizoendelea ndicho wanachofanya. Unalipwa kutokana na utendaji si kwasababu umeajiriwa. Kama tutaweka mfumo huo hakutakuwa na rushwa na ufujaji wa pesa.

Hizo ndizo hoja za Profesa, sasa meza yake inaelekea wapi ni mjadala wa kipuuzi sana. Inasikitisha
 
The guy still ana depression.
Anaona kama alionewa sana.
Changamoto yetu huwa tunailaumu serikali kwa sababu huwa hawajitetei.
Kuongea ukweli ndio depression? Huyo siyo mwenzako mpaka kufikia kuwa CAG hana dhiki ndogondogo
 
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Mstaafu, Mussa Juma Assad, amesema katika kipindi chake cha utumishi alikuwa akipokea simu za maelekezo kutoka kwa baadhi ya watu wakimtaka asifanye maamuzi fulani, lakini mara nyingi alisimamia alichokiamini kuwa sahihi. “Unaweza ukapigiwa simu ‘ah usilifanye bwana’, na wewe ukasema ‘hapana, mimi hiki nitakifanya’, na mimi nilikuwa nikifanya hivyo,” alisema.

Aliongeza kuwa ilikuwa desturi yake kila alipopokea maelekezo ya namna hiyo, asubuhi yake aliandika barua rasmi kuweka kumbukumbu ya mazungumzo hayo na msimamo wake kuhusu suala husika.
Anasemaje kuhusu ripoti zake kwenye Miradi ya nssf na Nhc
 
Sawa
 
Bado yuko bitter sana baada ya miaka yote hiyo; hata mtu aliyekataa kuongeza mkataba wale alishatangulia mbele ya hakei, lakini yeye bado analialia. CAG siyo cheo cha miaka kumi, ni miaka mitano halafu anaweza kuongezewa miaka mitano mingine na rais aliyeko madarakani. Yeye alimaliza miaka mitano ya kwanza halafu rais aliyekuwapo madarakani hakumwongezea miaka mingine mitano, asilalamike. Hakufukuzwa kazi bali alimaliza mkataba wake wa miaka mitano ila hakuongezewa miaka mingine mitano. Hatama Marekani, Gavan wa benki kuu ana mktaba wa miaka mitano, baada ya hapo rais aliyeko madarakani anaweza kumwongezea miaka mingine mitano. Janet Yelen alitumikia miaka mitano tu chini ya Obama, halafu Trump hakutaka kuendelea naye, wakati Bernanke alitumikia miaka mitano chini ya Bush na baadaye Obama akamuongezea piaka mitano mingine kabla ya Yelen.

Hata uchaguzi wa rais kwetu ni miaka mitano, ila akigombea tena akashinda ndipo anakamilisha miaka kumi. Tungekuwa na uchaguzi huru, ingewezekana kabisa kwa rais aliyeko madarakani kushindwa kipindi cha pili.

Huyu mtu ni professor lakini haongei mambo ya ki-professor. Kila anapoongea huwa ni mambo ya u-CAG tu, haongeieli profession ya accounting
 
Kwahiyo ataongea mpaka lini?
Huoni kama wewe ndiye kiazi kilichooza!!
Profesa unalalamika mpaka lini ili iweje sasa?
Nani asiyejua kuwa Magufuli amekiuka Katiba kumtengua CAG ?
Sasa yupo huyo Magufuli ili tumuwajibishe?
Tumia akili yako vizuri.
Ataongea mpaka masikio yenu yakariri....maana kenge hasikii mpaka masikio yatoke damu.

Simply anaweka more records Kwa vizazi vyenu vya baadae ili waje wajuwe how stupid the govt was......
 
Back
Top Bottom