Prof. Baregu alifukuzwa UDSM kwa sababu za kisiasa, huku Bashiru akiachwa kwakuwa ni CCM

Tairi bovu

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2017
Posts
3,063
Reaction score
2,985
Miaka kadhaa iliyopita Professor Mwesigwa Baregu akihudumia masomo ya siasa na utawala alinyanyaswa, kudhalilishwa na kudunishwa utu wake pale Mlimani. Bashiru aliachwa aendelee kula mema ya nchi kwa kuwa ni CCM na leo ameteuliwa kuwa Katibu mkuu wa chama. Twaambiwa alikuwa mwanachama wa siri, sijui wanachama wa siri ni kina nani?

Ile sheria inayokataza watumishi wa umma wasiwe wanasiasa kumbe ipo na inafanya kazi kwa wale watumishi ambao wanaunga mkono vyama vya upinzani tu?

Ubaguzi huu hadi lini?
 
Kipindi hicho umri wa baregu ulikuwa miaka mingapi? What I know he was past the statutory retirement age.
 
Acheni kupotosha.

Baregu aliondolewa Mlimani baada ya kubainika kuwa ni mjumbe wa Kamati kuu Chadema. Sio kwa muwa mwanachama wa siri wala wa wazi.

Kitila mkumbo alinusurika kuondolewa baada ya kubainika ni kiongozi ACT lakini aliyakana amajukumu yake ndani ya ACT na badala yake alibaki kuwa mwanachama wabkawaida na mwalimu wa chuo kikuu cha umma.

Bashiru alikuwa mwanaCCM lakini hakuwa kiongozi.

Kinacholeta shida ni pale unakuwa kiongozi sio mwanachama wa kawaida
 
Mkuu watzanaia wote ni CCM by default. Hata wewe ni ccm pia siku ukipewa cheo sehemu utaabaki kimya huku ukila kuku kwa mrija.

Nirudi Kwa Baregu na Bashiru.

Baregu kama mwajiriwa alikuwa ameingia kwenye mlengo kizani na mwajiri.. Ulitegemea aachwe?
Basiru alikuwa bega kwa bega na mwajili unategemea atimuliwe?
 
pesa haiwezi kununua furaha mkuu. chenge pale alipo hana furaha japo ana pesa.
 
utajaza vitabu na vitabu kuutafuta na kuuchora huo mstari hutaweza. ishu ni kwamba unatakiwa uwe mwana ccm tu. huku halmashaur kuna watu ni viongozi kabisa wa ccm hawafanywi lolote japo inajulikana wakati ukikutwa hata na lesso yenye bendera ya chama kingine ni mtihani mkubwa. kitila ni mtu wao. Kwani alipokuwa mjumbe wa kamati kuu CDM Alifukuzwa chuo?
Acheni kupotosha.

Baregu aliondolewa Mlimani baada ya kubainika kuwa ni mjumbe wa Kamati kuu Chadema. Sio kwa muwa mwanachama wa siri wala wa wazi.

Kitila mkumbo alinusurika kuondolewa baada ya kubainika ni kiongozi ACT lakini aliyakana amajukumu yake ndani ya ACT na badala yake alibaki kuwa mwanachama wabkawaida na mwalimu wa chuo kikuu cha umma.

Bashiru alikuwa mwanaCCM lakini hakuwa kiongozi.

Kinacholeta shida ni pale unakuwa kiongozi sio mwanachama wa kawaida
 
Ndo nchi za kiafrika shithole zilivyo mkuu.
 
Kwani Prof. Baregu alikuwa mwanachama wa siri wa chama gani cha siasa?
 
Tuwekee barua ya kufukuzwa kwake tuione inavyosema.
 
Acheni kupotosha.

Baregu aliondolewa Mlimani baada ya kubainika kuwa ni mjumbe wa Kamati kuu Chadema. Sio kwa muwa mwanachama wa siri wala wa wazi.

Kitila mkumbo alinusurika kuondolewa baada ya kubainika ni kiongozi ACT lakini aliyakana amajukumu yake ndani ya ACT na badala yake alibaki kuwa mwanachama wabkawaida na mwalimu wa chuo kikuu cha umma.

Bashiru alikuwa mwanaCCM lakini hakuwa kiongozi.

Kinacholeta shida ni pale unakuwa kiongozi sio mwanachama wa kawaida
Prof. Baregu alikuwa anafanya kazi kwa mkataba, ulipoisha hakuongzewa na si kwa sababu za kisiasa
 
utajaza vitabu na vitabu kuutafuta na kuuchora huo mstari hutaweza. ishu ni kwamba unatakiwa uwe mwana ccm tu. huku halmashaur kuna watu ni viongozi kabisa wa ccm hawafanywi lolote japo inajulikana wakati ukikutwa hata na lesso yenye bendera ya chama kingine ni mtihani mkubwa. kitila ni mtu wao. Kwani alipokuwa mjumbe wa kamati kuu CDM Alifukuzwa chuo?
Prof Baregu alishastaafu na akapewa mkataba wa miaka miwili ilipoisha alipotaka kuhuisha wakamwambia Imetosha!
 
Labd
Miaka kadhaa iliyopita Professor Mwesigwa Baregu akihudumia masomo ya siasa na utawala alinyanyaswa, kudhalilishwa na kudunishwa utu wake pale Mlimani. Bashiru aliachwa aendelee kula mema ya nchi kwa kuwa ni CCM na leo ameteuliwa kuwa Katibu mkuu wa chama. Twaambiwa alikuwa mwanachama wa siri, sijui wanachama wa siri ni kina nani?

Ile sheria inayokataza watumishi wa umma wasiwe wanasiasa kumbe ipo na inafanya kazi kwa wale watumishi ambao wanaunga mkono vyama vya upinzani tu?

Ubaguzi huu hadi lini?
Labda kuna wanachama wa wazi na siri kwenye katiba ya CCM
 
Back
Top Bottom