kiranjamkuukss
Member
- Jun 8, 2015
- 81
- 20
Naomba kueleweshwa matumizi ya "My take" kwenye threads
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hako kazee kalishatumika mpaka basi, sikapendi kama nini!
Akiiona anaweza kuwa mwehu hii thread itafikia page 70Ha ha aione Nicholas
CCM imeingiwa hofu, Magufuli kuwa shughuli
Mojawapo ya mambo ambayo yametokea baada ya Magufuli kutangazwa ni kauli za kuwa yeye "anakubalika na anachagulika". CCM imetaka kuliaminisha taifa kuwa Magufuli siyo tu anajulikana kwa utendaji kazi wake kwa kweli wananchi wengi wanampenda na wanaweza kumchagua. Kiasi kwamba wametaka watu waamini kuwa Magufuli ni Rais anayesubiria (President in waiting). Kwamba, upinzani hauna nafasi hata kidogo ya kumnyang'anya uwezekano huo.
Ukweli ni kuwa matendo ya CCM hayaoneshi kujiamini huku. Kama kweli CCM inaamini Magufuli anajulikana na kazi zake zinakubalika nchi nzima kwa nini juhudi kubwa sana inajaribu kufanywa ya "kumtambulisha". Unamtambulisha vipi mtu ambaye tayari unaamini anajulikana, kufahamika na kukubalika?
Tayari wizara ambayo amekalia imeshagubikwa na kashfa lukuki na hili peke yake lingetosha hata kumchafua. Akija mgombea mzuri kutoka upinzani na akajizibu hizi takwimu za Magufuli, basi Magufuli na CCM iko matatani. Yote haya yanatosha kufanya watu wajiulize mara mbili kama kweli Magufuli hatokuwa shughuli kweli kweli.
CCM imepasuka, rekodi yake mbovu, na upinzani ukimsimamisha mgombea makini, Magufuli ataweza vipi kushinda? Njia pekee ya kushinda katika mazingira ya namna hiyo ni matumizi makubwa ya nguvu, vyombo vya dola na hata kuliingiza jeshi katika siasa kama walivyofanya chini ya Jenerali Shimbo mwaka 2010. Vyovyote vile ilivyo hata hivyo kuna hofu imetanda kwa CCM; hofu kama vile wingu zito la mvua lenye dalili ya radi na ngurumo. CCM hawajui sasa wafanye nini zaidi ya kuombea Magufuli aweze kuwaokoa. Akishindwa je Hili ndilo swali la kuogopesha zaidi kwa kila mwana CCM
Chanzo: Raia Mwema
Wataiba kura!! Wala hawatahangaika! CCM Janga!!
Safari hii hatulali hadi kieleweke. Hatutasubiri sijui nini. Atakayeanzisha upumbavu wowote unaoashiria udanganyifu, bila kujali ni nani na yuko wapi tutamalizana naye pale pale kwa maslahi ya taifa.
Tuko tele, tunanguvu na tumetawanyika Tanzania nzima. Sasa tunachoanza kukifanya ni kufundishana namna tutapiga na kulinda kura zetu kwa kufuata kanuni za nchi.
Hawa wanaoanza kusema eti hakuna kukaa mita 100 wanahofu gani? Hao ndio wezi wa kura number 1. Tunaanzana nao kabla hata ya uchaguzi hadi wajue Tanzania ni ya Watanzania na si ya ccm na majambazi wenzao.
Askari wa polisi wanaoandaliwa kutumia mabavu na vitisho ili kutoa mwanya kwa ccm kuchakachua matokeo ya uchaguzi, wafahamu hizo silaha ni kodi zetu na hawatatuua sote. Tutakufa lakini tutaishi kwa watoto wetu katika Tanzania sahihi. Na kwa hiyo, wasije kudhani katika vita askari bila ushirikiano na raia bado ni askari. Bahati nzuri wanajulikana wote kwa sura, majina na koo zao. Bora wakafanya kazi kwa uadilifu bila kujaribu kuvuruga mchakato wa Tz kupata viongozi wetu. Haijalishi nani wanashinda lakini wasithubutu kuingilia kipum.ba.vu.
Hiki kitu kinaitwa tume ya ccm, wamepewa mamlaka makubwa na katiba ya 1977 ambayo ilitungwa kwa kufuata sura ya mwalimu bila kujua kuwa kunaweza kuja matawala nyang'au. Hata hivo, tunawapa angalizo la kufanya kazi kwa uaminifu. Hila zozote za kulinda green guards na tred brigade ili kutoa penalty kwa ccm wa sabbu binafsi, wasithubutu.
NA SASA TUNATAKA KURA ZA RAISI ZIHESABIWE VITUONI TUME IFANYE MAJUMUISHO.
HATUTAKUBALI HUJUMA YOYOTE KWA UPANDE WOWOTE. TUNAHITAJI TANZANIA YA WATANZANIA YENYE AMANI. WATUACHE TUFANYE MAAMUZI. HABARI YA KUTULETEA UCCM WA KUPATA KURA NYINGI AMINA ALLY NA KUTANGAZWA MAGUFULI, HATUTAKUBALI ZIHAMIE KWA TAIFA. HIZO NI ZA CCM TU!
Yaani mkuu ninakuunga mkono asilimia mia. Hilo suala la ulinzi wa kura ni mhimu sana, watu wakae umbali wa mita 100 ili kufuatilia nyendo za watu wanaopita na kwenda kule. Lkn kitu kingine mhimu sana, mwaka huu wapinzani wasikubali kurubuniwa kama mwaka 2010 kuwa kura za Rais zisihesabiwe vituoni bali zitaenda kujumuishwa na tume. Hapo ndipo uchakachuzi wa matokeo ulianza kufanyika. Mwanzoni Tume ilikuwa imeacha kura zinahesabiwa vituoni, lakini baada ya kuona jamaa aliyekuwa madarakani ameshikwa koo wakazuia (nadhani baada ya tume kushauriwa na TISS).
Hili jambo ni mhimu sana wapinzani wakalifanyia kazi na wasije wakakubali jambo hilo kufanyika kwa sbb kwanza ilikuwa ni kinyume na sheria za uchaguzi. Sheria ya uchaguzi inaruhusu kura zihesabiwe vituoni na matokeo ya Rais, Mbunge na Diwani kutangazwa hapo hapo badala ya kusubiri tume. Maana kama 2+2=4, kila mtu atapata jibu hilo hata awe wapi. Kwa namna hiyo, vyama vya siasa, vyombo vya na wadau wengine watakapopata matokeo nchi nzima toka kwa mawakala wao wataweza kujua kabisa nani ameshinda nafasi ya Urais hata kabla tume haijatoa matokeo rasmi. Nigeria hili jambo liliwasaidia sana, na ilikuwa vigumu matokeo kuchakachuliwa.