Prof. Eliamini Sedoyeka asomewa tuhuma nne kwenye Baraza la Maadili, azikana zote

Prof. Eliamini Sedoyeka asomewa tuhuma nne kwenye Baraza la Maadili, azikana zote

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Snapinsta.app_463280059_563212429507622_1474099077116797862_n_1080.jpg

Snapinsta.app_463584099_849897927336324_5562262567682456705_n_1080.jpg

Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma imemfikisha mbele ya Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma Mkuu wa chuo cha Taasisi ya Uhasibu Arusha (IAA), Prof. Eliamin Sedoyeka kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo kumpandisha cheo Afisa Rasilimaliwatu II kuwa Mkuu wa sehemu ya Rasilimaliwatu bila kuwa na sifa.

Tuhuma nyingine zinazomkabili ni kuingilia mchakato wa zabuni ya ununuzi na ufungaji wa viti na meza katika kampasi ya Babati kwa kuifuta bila kufuata utaratibu na kufanya uhamisho wa ndani wa mtumishi Afisa Ugavi kutoka kitengo cha Ununuzi na Ugavi kwenda Idara ya Maktaba tofauti na sifa za kitaaluma za mtumishi.

Akiwasilisha mashtaka mbele ya Baraza tarehe 16 oktoba, 2024 Wakili Mkuu wa Serikali Bi Emma Gelani alilieleza Baraza kuwa mlalamikiwa anakabiliwa na mashtaka manne na ameshindwa kutimiza matakwa ya kifungu cha 6(1)(a) 6(1)(c) na 12(1)(c) vya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

“Mlalamikiwa wakati akitekeleza majukumu yake ya uongozi pasipo kufuata sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma alimpandisha cheo Bw. Hakimu Ndatama kutoka Afisa Rasilimali II kuwa Mkuu wa sehemu ya Rasilimaliwatu kabla ya kukamilika kwa uhamisho wa mtumishi.”

Bw. Ndatama ambaye ni mmoja kati ya mashahidi wanne waliotoa ushaidi wao mbele ya Baraza alikiri kuwa tarehe 13.5.2023 alipandishwa cheo kutoka Afisa Rasilimaliwatu II kuwa Mkuu wa sehemu wa Taasisi ya Uhasibu Arusha kabla ya taratibu za uhamisho kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii hazijakamilika.

Kuhusu suala la zabuni, Bi Gelani alieleza kuwa mlalamikiwa aliingilia mchakato wa zabuni ya ununuzi na ufungaji wa viti na meza na kuifuta kinyume kifungu cha 59(2) cha Sheriai ya Ununuzi wa Umma, Sura ya 410.

“Kitendo hicho Mhe. Mwenyekiti ni kinyume na kifungu cha 6(1)(c) cha Sheria ya Maadili kinachomtaka kiongozi wa Umma kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Sheria za nchi,”alisema.

Ilidaiwa mbele ya Baraza kuwa Prof. Sedoyeka alifuta zabuni kwa madai kuwa gharama ilikuwa kubwa kuliko bajeti ya taasisi ya shilingi bilioni 1.274

Shahidi wa kwanza katika lalamiko hilo Bw. Ramadhani Mwanang’waka ambaye ni Afisa wa Sekretarieti ya Maadili alisema kuwa katika uchunguzi wao walibaini kuwa kampuni mbalimbali ziliomba zabuni hiyo.

Alizitaja kampuni hizi kuwa ni Jaffery ING Sain Ltd iliyopata zabuni kwa shilingi 1,144,057,200/ , Timber and Hardware Ltd 1,013,974,000.03, Vadeck Investment Company Ltd iliyoomba zabuni kwa shilingi 762,625,003/= jumla ya

“Baada ya kupitia nyaraka za zabuni tulibaini kuwa sababu za kusitisha zabuni hazikuwa miongoni mwa sababu zilizoainishwa kisheria,” alisema.

Kuhusu uhamisho wa mtumishi bila kufuata taratibu, Bi Gelani alilieleza Baraza kuwa Prof. Sedoyeka alifanya uhamisho wa ndani wa Bw. Robert Mwitango ambaye ni Afisa ugavi kutoka Kitengo cha Ununuzi na Ugavi kwenda idara ya Maktaba tofauti na sifa zake za kitaaluma.

“Mhe. Mwenyekiti uhamisho huu ulifanyika bila kuzingatia matakwa ya Kifungu cha 6(1)(c) cha Sheria ya Utumishi wa Umma kinachowataka wakuu wa Taasisi kusimamia na kuhakikisha watumishi wanakuwa katika taaluma zao,” alisema na kuongeza kuwa, “kitendo hiki ni kinyume na Kifungu cha 6(2) cha Sheria ya Maadili.”

Bw. Robert aliyefika mbele ya Baraza kutoa ushahidi, alikiri kuhamishiwa Idara ya maktaba kwa barua aliyoipata tarehe 6.10.2023 ambayo haikubainisha majukumu ya kazi.

“Niliporipoti Maktaba nilipangiwa kukaa mapokezi kukagua wanafunzi wanaoingia na kutoka ndani ya Maktaba.

Bw. Robert ni Afisa ugavi daraja la I ambaye ni Certified Procurement and Supply Professional (CPSP).

Mlalamikiwa ameyakana mashtaka yote manne na tarehe 17.10.2024 anatarajia kuwasilisha utetezi wake mbele ya Baraza.

Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma linasikiliza lalamiko hilo chini ya

Mwenyekiti Mhe. Jaji (Mst.) Rose Teemba na wajumbe wa Baraza Bw. Peter Ilomo na Bi Suzan Mlawi.

Profesa ajitetea:
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Honoratus Ishengoma amesema “Baraza limesikiliza utetezi wake (Prof. Sedoyeka), Mwenyekiti amesema baada ya kusikiliza pande zote mbili, litafanya hitimisho na ushauri utapelekwa kunakohusika.



============================ ======================​

BARAZA LA MAADILI LAHITIMISHA KUSIKILIZA TUHUMA ZINAZOMKABILI PROF. SEDOYEKA
Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma limehitimisha kikao chake cha siku mbili cha kusikiliza tuhuma za ukiukwaji wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma zilizokuwa zikimkabili Mkuu wa chuo cha Taasisi ya Uhasibu Arusha (IAA), Prof. Eliamini Sedoyeka.

Kikao hicho kilichohitimishwa tarehe 17.10.2024 kiliongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Maadili Mhe. Jaji (Mst.) Rose Teemba akisaidiana na wajumbe wa Baraza Bw. Peter Ilomo na Bi Suzan Mlawi.

“Baraza litafanya hitimisho baada ya kusililiza pande zote mbili, ushauri utapelekwa kunako husika,” alisema Mhe. Teemba baada ya Prof. Sedoyeka kutoa ushahidi wake.

Prof. Sedoyeka alikuwa akikabiliwa na mashtaka manne anayodaiwa kutenda wakati akitimiza majukumu yake ya uongozi.

Mashtaka hayo kumpandisha cheo Bw. Hakimu Ndatama kutoka Afisa Rasilimaliwatu daraja la II kuwa Mkuu wa sehemu ya Rasilimaliwatu bila kuwa na sifa, kuwa na mgongano wa maslahi kwa kufanya uamuzi wa kumnufaisha Bw. Hakimu Ndatama, kuingilia mchakato wa zabuni ya ununuzi na ufungaji wa viti na meza katika kampasi ya Babati kwa kuifuta bila kufuata utaratibu na kufanya uhamisho wa ndani wa Afisa Ugavi kutoka kitengo cha Ununuzi na Ugavi kwenda Idara ya Maktaba tofauti na sifa za kitaaluma za mtumishi.

Akiwasilisha mashtaka mbele ya Baraza tarehe 16 Oktoba, 2024 Wakili Mkuu wa Serikali Bi Emma Gelani alilieleza Baraza kuwa mlalamikiwa anakabiliwa na mashtaka manne na ameshindwa kutimiza matakwa ya kifungu cha 6(1)(a) 6(1)(c) na 12(1)(c) vya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

“Mlalamikiwa wakati akitekeleza majukumu yake ya uongozi pasipo kufuata sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma alimpandisha cheo Bw. Hakimu Ndatama kutoka Afisa Rasilimali II kuwa Mkuu wa sehemu ya Rasilimaliwatu kabla ya kukamilika kwa uhamisho wa mtumishi.”

Bw. Ndatama ambaye ni mmoja kati ya mashahidi sita waliotoa ushaidi mbele ya Baraza alikiri kuwa tarehe 13.5.2023 alipandishwa cheo kutoka Afisa Rasilimaliwatu II kuwa Mkuu wa sehemu wa Taasisi ya Uhasibu Arusha kabla ya taratibu za uhamisho kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii hazijakamilika.

Akitoa utetezi wake mbele ya Baraza kuhusu tuhuma hiyo, Prof. Sedoyeka alisema, “Sikuwa na mamlaka ya kumpandisha cheo Bw. Hakimu, isipokuwa nilimteua na kumpangia majukumu. Nilimtea kwa nia njema ya kuongeza ufanisi, kwa maelezo hayo, naomba Baraza lako lifute shtaka hili kwasababu nilitekeleza kwa nia njema.”

Kuhusu lalamiko la kufanya uamuzi wa kumnufaisha Bw. Hakimu, Prof alilieleza Baraza kuwa hakuhusika na mchakato wa kumuombea uhamisho Afisa huyo kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii kwenda IAA.

“Mimi sikuhusika kwa namna yoyote ile, kuomba Bw. Hakimu kuja IAA kwa barua ya tarehe 9.3.2023 wakati mimi nililipoti IAA tarehe 13.3.2023, hivyo, sikusaini barua yake ya kuomba ahamie wala kukumbushia,” alieleza.

Kuhusu kuingilia zabuni ya ununuzi na ufungaji wa viti na meza na kuifuta kinyume kifungu cha 59(2) cha Sheriai ya Ununuzi wa Umma, Sura ya 410, Mkuu huyo wa chuo cha IAA alilieleza Baraza kuwa Taasisi yake ilipohitaji viti katika kampasii ya Babati, alielekeza iundwe kamati kutembelea maeneo tofauti nchini kuangalia mzabuni mwenye uwezo.

“Nilielekeza Kitengo cha Manunuzi kumhusisha mzabuni Timber and Hardware Ltd na kamatii ilikuwa na mapendekezo yake,” alisema na kuongeza kuwa, “Baada ya mchakato kufanyika, nilipitia nyaraka za mchakato .wa ununuzi na kugundua kuwa kuna wazabuni wawili walikuwa na bei ndogo hawakushinda kwa madai ikuwa bidhaa zao hazikufikia viwango, watu hawa walishinda zabuni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, lakini kwetu hawakufikia viwango.”

Kwa mujibu wa kiongozi huyo, taarifa ya ukaguzi ya vifaa husika haikuwa na maelezo ya kitaalam kukataa wazabuni waliokuwa na bei nafuu.

“Kwangu mimi hii ni dosari, nilikuwa kwenye mtanziko, nikaamua kufanya kikao na mwenyekiti wa Bodi ya zabuni tukakubaliana kuwa hata tukitangaza zabuni upya kwa kuwa nyaraka ni zilezile, hakuna jinsi atashinda Jaffery ING Sign Ltd aliyekuwa na bei kubwa.

Katika mchakato huo wa ununuzi wa viti na meza, jumla ya kampuni nne zilijotokeza ikiwemo Jaffery ING Sain Ltd iliyopata zabuni kwa shilingi 1,144,057,200/, Timber and Hardware Ltd 1,013,974,000.03, Vadeck Investment Company Ltd iliyoomba zabuni kwa shilingi 762,625,003/= na kampuni ya Mult Cable Ltd kwa gharama ya shilingi 1,163,527,200.03.

Prof. Sedoyeka alifuta zabuni kwa madai kuwa gharama ilikuwa kubwa kuliko bajeti ya taasisi ya shilingi bilioni 1.274 Mchakato huo uliositishwa Juni, 2023, hadi sasa hivi bado haujakamilika.

Shahidi wa kwanza katika lalamiko hilo Bw. Ramadhani Mwanang’waka ambaye ni Afisa wa Sekretarieti ya Maadili alisema kuwa “baada ya kupitia nyaraka za zabuni tulibaini kuwa sababu za kusitisha zabuni hazikuwa miongoni mwa sababu zilizohainishwa kisheria.”

Kuhusu uhamisho wa ndani wa Bw. Robert Mwitango Afisa Ugavi kutoka kitengo cha Ununuzi na Ugavi kwenda Idara ya Maktaba tofauti na sifa za kitaaluma za mtumishi, aliliambia Baraza kuwa, “Mimi ninayo mamlaka kumpangia shughuli nyingine mtumishi na uhamisho huu ulikuwa na nia njema kwa maslahi ya Taasisi.”

“Kitengo cha Unununzi kilikuwa na watumishi 10, Idara yamaktabab ilikuwa na upungufu wa watumishi na walitaka kufanyay ununuzi mkubwa wa vitabu, kutokana na uhaba mkubwa wa rasilimali watuu katika Maktaba mimi kuhamisha mtumishi niliona ni suala la kawaida katika taasisi,” alilieleza baraza.

Bw. Robert aliyefika mbele ya Baraza kutoa ushahidi, alikiri kuhamishiwa Idara ya Maktaba kwa barua aliyoipata tarehe 6.10.2023 ambayo haikubainisha majukumu ya kazi.

“Nililipoti Maktaba nakupangiwa kukaa mapokezi kukagua wanafunzi wanaoingia na kutoka ndani ya Maktaba.

Bw. Robert ni Afisa ugavi daraja la I ambaye ni Certified Procurement and Supply Professional (CPSP).

Wakili Mkuu wa Serikali Bi. Emma Gelani alilieleza baraza kuwa .“uhamisho huu ulifanyika bila kuzingatia matakwa ya Kifungu cha 6(1)(c) cha Sheria ya Utumishi wa Umma kinachowataka wakuu wa Taasisi kusimamia na kuhakikisha watumishi wanakuwa katika taaluma zao,” alisema na kuongeza kuwa, “kitendo hiki ni kinyume na Kifungu cha 6(2) cha Sheria ya Maadili.”.

Wakati akimsomea mashtaka mlalamikiwa, Wakili Gelani aliliambia Baraza kuwa, “Malalamiko hayo dhidi ya Prof. Sedoyeka ni kinyume na kifungu cha 6(1)(c) cha Sheria ya Maadili kinachomtaka kiongozi wa Umma kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Sheria za nchi,” alisema.

Snapinsta.app_463468483_1291375852232629_8787437121067840154_n_1080.jpg
Pia soma ~ Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma yawasilisha malalamiko kuhusu Prof. Eliamini M. Sedoyeka

Majibu ya Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Prof. Eliamini Sedoyeka mbele ya Baraza la Maadili
 
Tunaomba hilo baraza la maadili lisiishie hapo wamchunguze na huyu.

 
Favor ni nzurii sanaa Kama mtu anakua na VIGEZO (qualifications) zoteee
Favoritism is real Ila Sasa uwe na VIGEZO qualifications zoteee..

"""Is like you don't have qualifications and you need an excuse for a favor""
Nikajua aliyepewa favour ana msambwanda. Prof toka akiwa Wizarani alikua mtu wa totoz sana
 

 
Juzijuzi kafiwa na yule mke wake alokuwa mbunge wa Africa Mashariki sasa kaingia kwenye huu msala, kweli shida zikianza kukuandama hazipoi. Ndo maisha
Haya mashtaka hua hayaibuki tu, huenda yapo chini kwa chini hata miaka miwili. So huenda hili lilianza fukuto hata kbl ya mkewe kufariki.
Jamaa yupo poa sana nakumbuka alinifundisha IFM akisimamia mtuhani hana mbwembwe kama wengine, yeye na simu yake furesh hakuna kukurukakala wala we hamia hapa we toka hapo wala nn!!
 
Baraza la Maadili limemaliza kumhoji Mkuu wa Chuo cha uhasibu (IAA )Arusha,Professa Eliamani Sedoyeka kuhusu tuhuma nne zinazomkabili ambapo katika majibu yake amedai hazina ukweli wowote na kwamba alifuata taratibu zote za kiutumishi katika kufanya maamuzi.

Akijibu Tuhuma ya kuwa na ukaribu na mtumishi Hakimu Ndatama na uhamisho wake kurudi IAA pindi yeye aliporejea kuwa Mkuu wa Chuo Prof amesema kwamba Uhamisho wa Ndatama kwenda Wizara ya Maliasili na Utalii ulifuata taratibu zote za kisheria na kufuatia mahitaji ya kikazi, Chuoni hapo na hakuna ukiukwaji wowote.

Alieleza kwamba Chuo kiliandika Barua kwenda Wizara ya Maliasili na Utalii ya kuomba,Ndatama arejeshwe.Zoezi hilo lilifanyika kabla ya yeye kurejeshwe Chuoni IAA hapo kutokana na mahitaji ya kikazi .

Na kuhusu Tuhuma za Uteuzi wa Hakimu Ndatama kuwa Mkuu wa Kitengo, Sedoyeka alieleza kwamba Kuhusu tuhuma ya kutekeleza uteuzi wa Hakimu Ndatama na mgongano wa maslahi, napenda kueleza kuwa uteuzi huu ulikuwa na msingi mzuri unaozingatia uwezo na ufanisi wake katika utekelezaji wa majukumu yake ya kazi chuoni hapo.

Alisema kwamba alizingatia sifa za Ndatama na uwezo wake wa kuchangia maendeleo ya IAA akiwa na dhamira ya kulinda maslahi ya taasisi na kuhakikisha kwamba wanapata watu wenye uwezo na wivu wa kuchangia maendeleo katika kufikia malengo ya taasisi.

Alifafanua kwamba Ndatama si ndugu yake wala si kabila lake wala hakuna chochote kinacho muunganisha nacho na kuwa na maslahi juu yake.

Kuhusu malalamiko juu ya Zabuni ya Viti na Meza vya Wanafunzi kwa Kampasi ya Babati Professa alisema kwamba Kwa mujibu wa Sheria ya Manunuzi ya Umma, Na. 7 ya mwaka 2013), inampa mamlaka Afisa Masuuli kukataa kuendelea na zabuni ama kurejesha zabuni kwenye Bodi ya Zabuni.

"Ninaweka wazi msimamo wangu kwamba nilifuata taratibu zote na sikuvunja sheria bali nilikuwa nikitekeleza majukumu yangu kwa mujibu wa Sheria"alisema na Kuongeza

"Kama kiongozi mwaminifu kwa nchi yangu, nimekuwa makini kuhakikisha taasisi inapata bidhaa bora kwa njia za uwazi na kwa gharama nafuu kwa mujibu wa Sheria ya Ununuzi wa Umma".

Na kuhusu Tuhuma za Uhamisho wa Ndani wa Mtumishi Robert Mwitango alieleleza kwamba Kwa ujumla uhamisho wa ndani wa watumishi hufanywa kwa lengo la kuboresha ufanisi wa kiutendaji wa taasisi.

Katika Mwaka wa 2023/2024 Idara ya Maktaba ilipanga kutekeleza shughuli mbalimbali zikiwemo zile ambazo kwa uhalisia wake zilihitaji
msaada wa karibu wa kitengo cha Manunuzi ya Umma, kama Stock taking, Asset Verification” na Ununuzi mkubwa wa vitabu kwa mkupuo.

prof-eliamani-sedoyeka-data.jpg
 
Back
Top Bottom