Prof. Eliamini Sedoyeka asomewa tuhuma nne kwenye Baraza la Maadili, azikana zote

Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma ikiamua kwa dhati kabisa kufuatilia tuhuma za namna hii kwenye taasisi mbalimbali Basi ni Wakuu wa taasisi wachache Sana watanusurika, wengi wao zaidi ya 80% wataenda na maji. Makosa Kama haya yamekuwa yakifanyika kwa wingi Sana kwenye hizo taasisi za Serikali.
 
Sishangai Baada ya mama yangu kufarki wiki mbili. Tu baadae ikaja samansi aachie eneo lenye thamani ya milion 300 tulizidiwa uwezo na wenye fedha basi ikapita
Juzijuzi kafiwa na yule mke wake alokuwa mbunge wa Africa Mashariki sasa kaingia kwenye huu msala, kweli shida zikianza kukuandama hazipoi. Ndo maisha
 
Takukuru ni useless wale wanakula pesa za Bure tu hakuna kazi pale.
tako kuuruuuuuuuuu hamna kitu wale mbwa , yani mapolisi wenyewe wanavuna za barabarani mpaka wanajaza mihela kwenye makapu lakini hao umwa wapo tu inauma sana.
 
Ingawaje kwa kiasi fulani amejitahidi kujibu baadhi ya hoja kwa usahihi, lakini bado kuna baadhi ya hoja ambazo anapaswa azitolee ufafanuzi wa kina zaidi, hususani kuhusu suala hili la Uhamisho wa Ndani wa huyo Mtumishi mwenye taaluma ya manunuzi kwenda Idara ya Maktaba.
1. Kama lengo lilikuwa ni kuongeza ufanisi kwenye Idara hiyo ya Maktaba, Je, ni kwa nini Mtumishi huyo aliyehamishwa hakupewa na Maainisho ya Majukumu yake Mapya (Job Descriptions mpya) wakati alipohamishiwa huko Maktaba??
2. Kwa kuwa Mtumishi huyo hakupewa New Job Descriptions, maana yake ni kwamba Majukumu yake yale yale ya awali aliyopangiwa na Mwajiri wake ndiyo anapaswa kuendelea nayo akiwa huko kwenye Idara mpya ya Maktaba alikohamishiwa. Sasa; Je, kwa nini Mtumishi huyo apangiwe majukumu mengine Mapya kabisa kinyume na taaluma yake aliyosomea na kinyume kabisa na majukumu yake ya awali ambayo alipangiwa na ambayo pia ndio sababu za Msingi zilizopelekea Mtumishi huyo kuajiriwa na hiyo taasisi? So Where is the purpose of Professionalism and Job Specialization for the Job-seekers or Employees?? Je, kulikuwa na sababu gani ya kumuajiri Mtumishi mwenye sifa hizo za taaluma ya Manunuzi wakati kazi zake au majukumu yake atakayopangiwa hayaendani na uhitaji wa taaluma hiyo?? Jambo hili ni kitendo cha hatari Sana endapo kama utalifanyia tathmini ya kina Sana.

Mathalani, Yaani Kama vile Utawala wa Hospitali ya Muhimbili Leo hii kwa kutumia njia za holela waamue kuwabadilishia majukumu ya kazi baadhi ya Madereva na kuwapangia Majukumu Mapya ya kazi za Udaktari wa Tiba ya Binadamu na kisha kuwaruhusu Madereva hao waanze kuingia kwenye Vyumba vya Upasuaji Wagonjwa ili waweze kuwafanyia Upasuaji (Surgery) wagonjwa wenye uhitaji wa huduma hiyo!
Ridiculous!
 
Hali uliyoeleza inaonyesha changamoto kubwa katika usimamizi wa rasilimali watu na ufanisi wa kazi katika taasisi. Hapa kuna baadhi ya maswali na mawazo ya kuzingatia:

1. Kukosekana kwa Maelezo ya Majukumu Mapya:
Ni muhimu kwa kila mtumishi kupewa maelezo ya majukumu yake mapya ili kuelewa wazi nini kinatarajiwa kutoka kwake. Kukosa maelezo haya kunaweza kusababisha kutokuelewana na mkanganyiko kuhusu majukumu yake.

Kwa maelezo hayo hapo juu,Prof. Eliamini Sedoyeka,anastahili kufukuzwa KAZI na kushitakiwa.

2. Mabadiliko ya Majukumu:
Ikiwa mtumishi anahamishiwa idara mpya, inapaswa kuwa na mantiki kuhusu majukumu ambayo atapewa. Kuteua majukumu yasiyohusiana na taaluma yake inaweza kuathiri ufanisi na morali, na hata kusababisha mtumishi kuhisi kutokuwa na thamani.

3. Umuhimu wa Utaalamu:
Kila mtaalamu anatarajiwa kutumia ujuzi na maarifa aliyoyapata katika masomo yake. Kutoa kazi zisizoendana na taaluma yake kunaweza kuondoa motisha na kuathiri ubora wa kazi.

4. Athari za Kitaaluma:
Kitendo cha kuteua mtumishi mwenye sifa fulani kisha kumpa majukumu yasiyohusiana na sifa hizo kinaweza kuathiri si tu mtumishi huyo, bali pia taasisi kwa ujumla. Hali hii inaweza kupelekea kupoteza wataalamu wenye uwezo na hatimaye kuathiri ufanisi wa kazi.

5. Mwanzo wa Mabadiliko:
Ni muhimu kwa waajiri kuzingatia uhusiano kati ya mahitaji ya kazi na sifa za mtumishi. Hii inahitaji tathmini ya kina kabla ya kufanya uhamisho au mabadiliko ya majukumu.

Kwa ujumla, kuna umuhimu wa kuweka wazi mawasiliano na kuelewa majukumu ya kila mtumishi ili kuhakikisha kuwa wanaweza kufanya kazi kwa ufanisi na kwa kutumia uwezo wao wa kitaaluma. Hali ya kutokuwepo kwa maelewano inaweza kuathiri si tu mtumishi mmoja bali pia ufanisi wa jumla wa taasisi.

Kwa maelezo hayo hapo juu, Professor anatakiwa awajibishwe kwa kupelekwa UDSM. akafundishe. Uongozi ni ni ziro.
 
Aisee kumbe uwa Kuna hili baraza la maadili lkn wakeup wa idara wanaishi kama miungu watu aisee
 
Vipi sasa aliwajibishwa au alishinda??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…