Ni simanzi, ni huzuni, ni sikitiko, ameondoka gwiji, guru na mwanazuoni mbobevu Prof. Haroub Othman. Sina mengi ya kusema ulikuwa mwalimu wangu, upole wako na sauti yako ya chini lakini yenye ushawishi mkubwa itakumbukwa daima dumu.
.......Umetutangulia tu nasi twaja muda si mrefu, si mbali ulikoenda ni karibu mno, ni kweli utakwenda kuonana na hawa watu Mwl. Nyerere, Prof. Chachage, Abdulrahamni Babu, Yasser Arafat na wengineo. Waambie haya yafuatayo
Mwl. Nyerere
...Mwambie Uzanzibar na Utanganyika umepamba moto, kila mtu anataka taifa lake,
...Mwambie sio mpasuko tena kwenye muungano ila ni handaki ambalo bila dua zake uko aliko muungano utazama umo na kupotea milele
...Nchi imevemiwa na si wahujumu uchumi tena ila ni mafisadi wanaojibatiza majina wenyewe ya upapa na unyangumi
...Nchi imeoza inanuka, vijana aliowaacha hawafai wameshaiuza kitambo mara tu alipofariki
...Nchi inatawaliwa na mabepari aliowakataa enzi zake, wajanja wa kujitajirisha wenyewe na familia zao
...Ardhi aliyoilinda kwa faida ya wote sasa iko mikononi mwa mabepari wachache uchwara wa ndani na nje ya nchi,
...Usisahau kumwambia pia kuwa punde si punde Butiama itakuwa wilaya
Prof. Chachage
... Mwambie wale makuhadi wa soko huria wamekuwa moto, hakuna tena wa kuwaponda na kuwasema wazi,
...Mwambie wale wanafunzi wa vyuo vikuu aliowatetea hasa UDSM siku hizi hawana mtetezi tenz wanafukuzwa kwa memo kama manamba kwenye mashamba ya mkonge, hamna tena wa kuwatetea, UDASA ya sasa siyo ile ulioyoiacha, ina maprofesa waoga kama kunguru wa Zanzibar
Yasser Arafat
...Mwambie bado wapalestina hajakombolewa, ni danadana kila siku
...Mwambie bado muisraeli mmoja anafidiwa na wapalestina 1000
...Mwambie mauaji ndi yanapamba moto ukanda wa Gaza, mwambie wanawake na watoto wa KIpalestina wanauawa kila kuchapo hawana tena msemaje kama yeye
Adlrahamani Babu
...Mwambie Muungano unasuasua kutokana na maslahi binafsi
...Mwambie upinzani ndio kabisa unafifia hakuna jipya tena
...Mwambie Wazanzibar wanmkumbuka sana na kamwe hawawezi kumsahau
Usisahu kuwasalimia Kwame Nkrumah, na kumwambia muungano wa Afrika imekuwa ndoto za abunuwasi. Wasalimie pia akina Mwanawasa, Jomo Kenyatta, na wanamapinduzi wengineo wote waliokwisha tangulia mbele za haki. Amen
RIP Prof. Haroub Othmani