Prof. Haroub Othman Afariki Dunia

Prof. Haroub Othman Afariki Dunia

Mwenyezi MUNGU nakuomba umpumzishe kwa amani Prof. Haroub Othman na mwanga wa milele umwangazie.

RIP Prof.
 
Mungu alitoa Mungu ametwaa jina la bwana libarikiwe.

Tutakukumbuka kwa msimamo wako kama msomi, na mwalimu wetu.

Nenda Prof.
 
It is a great loss indeed!
I first saw proffessor Horoub Othman way back in 1992 while attending an International Conference on the History & Culture of Zanzibar. I was much interested with his presentation and the contribution through out the conference. I came to meet him again in theatre room (ATB) at the University of Dar es Salaam in 1993 when I joined the university giving a DS lecture , I have eversince valued him for the valuable and patriotic and staight forward contributions to the well being of the country and the people.

When I got this sad news through SMS from my friend I said no! but I went on finding the reality and here comes it, My Professor, Mentor, Nationalist is gone!

inna lillahi wa inna ilayhi rajioon

We lost a revolutionary!
 
Usisahu kuwasalimia Kwame Nkrumah, na kumwambia muungano wa Afrika imekuwa ndoto za abunuwasi. Wasalimie pia akina Mwanawasa, Jomo Kenyatta, na wanamapinduzi wengineo wote waliokwisha tangulia mbele za haki. Amen

RIP Prof. Haroub Othmani

KWENYE salamu hizo, mimi SIPO.
Sipo kabisa.
Siamini kuongea na marehemu.
 

Kifo chake kimeleta masikitiko makubwa kwa watanzania na Dunia kwa ujumla.

Marehemu Profesa Horoub Othman
Alikuwa
- msomi mwadilifu, alichukia ufisadi sana.
- mtaalamu mwenye upeo wa mbali katika kuchambua masuala magumu ya kitaifa na kimataifa..
- mtetezi wa haki za binadamu kote ulimwenguni.
- hakupenda makuu wala kujisifu.
- Hakuwa na upendeleo wala udini na ukabila vitu ambavyo ni sumu ya maendeleo.

Nilimfahamu sana.

Nimesikitika sana.
 
Don't tell me!
Ina lilah waina Ilayhi Raj' un, Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi.
siku ya halamisi tarehe 25 mwezi huu,aliudhuria mkutano wa bodi ya wadhamini taasisi ya mwl, nyerere. Alionekana mwenye afya NJEMA mimi nilimfungulia soda nyeupe ndio huwa anakunywa.Don't tell me.
Mungu ailaze roho ya marehemu SHEIKH gorogosi mahala pema. Actually Misiba ya KITAIFA.
 
Will deeply missed by us(me and my wife).....thanks for taking good care of us...much grtings to Chachage S. Chachage.
 
ZANZINET ndio wana data nyingi za Haroub lakini membership wanabania, hivyo ni vigumu kujua Unguja kuko katika hali gani leo
 
Raha ya milele uumpe ee bwana na mwanga wa milele umuangazie apumke kwa amani. Amina. Kwa jina la baba nala mwana nala roho mtakatifu amina.
 
Kwa niaba ya The Civic United Front (CUF – Chama cha Wananchi), ninatoa mkono wa pole kwa kifo cha ghafla ya msomi wetu, Profesa Haroub Othman wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kilichotokea asubuhi hii mjini Zanzibar.

Binafsi nimeshtushwa sana na kifo hiki ikizingatiwa kwamba ni jana tu Prof. Haroub alishiriki katika uzinduzi wa kitabu kinachokhusu maisha yangu katika harakati za siasa za Zanzibar na akafanya uhakiki wa kitabu hicho. Huu ni ushahidi kwamba hata katika saa zake za mwisho, Profesa Haroub alikuwa anafanya kazi zake za kisomi, kwani huyu alikuwa ni msomi hasa aliyeuvaa usomi wake kwa kila hali na mali.

Kwa kuondokewa na Profesa Haroub, chuo chake, Zanzibar, Tanzania, Afrika na ulimwengu kwa ujumla, tumeondokewa na hazina kuu ya elimu na maarifa ya siasa na sheria. Tumeondokewa na mchambuzi wa historia. Mchango wake utakumbukwa daima katika masuala kadhaa ambayo aliyasimamia, kuyachambua na kuyawekea misimamo, likiwemo suala la haki za binaadamu na sheria, Zanzibar, kufikia hadi kuanzisha kituo cha kwanza cha Haki za Binaadamu na Sheria visiwani humu na pia kuendeleza ile azma ya Afrika Moja kama ilivyoanzishwa na waasisi wake, Dkt. Kwame Nkrumah, Mwalimu Julius Nyerere na viongozi wengine wa ukombozi wa Bara la Afrika. Kwa hakika, Profesa Haroub ameishi maisha yake kwa ukamilifu!

Sisi, katika CUF, tunamuomba Mwenyezi Mungu ampokee akiwa amemsamehe makosa yake na aufanye mwema ujira wake. Tunaungana na familia ya marehemu, jumuiya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Wazanzibari, Watanzania na Waaafrika wote katika wakati huu mgumu wa maombolezo.

Mwenyezi Mungu aipe familia ya marehemu nguvu na subira za kuweza kukabiliana na msiba huu. Amin!

Innalillahi wainna ilayhir raaji’un. Sisi sote ni wa Mwenyezi Mungu na Kwake tutarejea!


Seif Sharif Hamad​
Katibu Mkuu​
The Civic United Front (CUF – Chama cha Wananchi)​
 
Nakumbuka ulipokuwa mwalimu wangu pale UDSM, ulikuwa kipenzi cha watu,wanafunzi wote walikupenda.

Mungu Akulaze mahala pema peponi.
Ameen!!!
 
Hivi tuseme angekufa mwesigwa baregu mngeileta obituary yake huku kwenye forum ya celebrities?

Invisible itabidi tuongee
 
hebu mpeni Professa Heshima yake jamani

hivi ni utoto wa moderation team au dharau tuu?
 
Back
Top Bottom