That's what you were told; and what did you find out on your own?
This is ridiculous isn't it?- kwenye Majukwaa tunaambiwa na Waunda Azimio, "usawa", "usawa", then many years later wanatuambia, "si usawa kwa maana vidole havilingani".
You ask me what did I find on my own, I just find that we were duped!, a kind of Animal farm where some animals are more equal than others. this kind of flip flop is destined to fail and this is what happened exactly few years later.
ngoja sasa nikuwekee baadhi ya masharti ya Azimio la arusha then utaona kwamba Azimio la Arusha lilihitaji modification katika kipengele cha Maadili ya Viongozi.
kipengele cha 4 kinasema hivi:
ASIWE NA MISHAHARA MIWILI.
Hii ilikuwa inadumaza, inakwaza mtu mwenye uwezo wa kutumikia kazi mbili kwa ufanisi kujiinua, na kutoa mchango mkubwa kwa jamii!, mathalani kuna ubaya gani daktari Bingwa/kiongozi wa idara kuwa daktari na kuwa lecturer na kisha kupokea ujira kwa kazi zake hizo mbili anazofanya?.
Azimio la Zanzibar lilikuja kuondoa discrepancies kama hizi, sasa badala ya watu kuona kwamba ni modification ya msingi kwa sababu Azimio la Arusha siyo Msahafu, wakaona kwamba eti ni kulipinga Azimio Zima, HIYO SI KWELI. bali hayo ni mabadiriko ya msingi ambayo yalibidi yafanywe kutokana na wakati.
kipengele cha Tano cha maadili ya Kiongozi kinasema hivi.
ASIWE NA NYUMBA YA KUPANGISHA
Hii pia ilikuwa ni kikwazo na unnecessary, kama mimi ni mkulima na mfanyakazi nina kipato halali kwa nini nisiweze kuwa na nyumba na nikaipangisha pia?.
Je kama nina nyumba tupu, au nina nyumba ambayo siitumii yote, je siwezi kupangisha vyumba vilivyobaki?.
Mwisho basi, Azimio ni sera ya Chama, na si Watanzania Wote ni wanachama wa vyama vya siasa, hatuwezi kulilia sera ya Chama labda uwe ni mwanachama wa Chama hicho!. Azimio la Arusha ilikuwa ni sera ya TANU/CCM na wanaCCM walikuwa na haki ya kuibadirisha na kusema kweli hicho ndicho walichokifanya Zanzibar mwaka 91, suala ni kujiuliza je hayo mabadiriko waliyoyafanya ni ya msingi au la?. so far mimi ninaona Azimio la Zanzibar lilikuwa halikwepeki na lilikuwa ni la muhimu sana.
Then angalia kipengele cha Sita kinamdefine Kiongozi ni mtu wa Namna gani?
(6) -
Viongozi tunaofikiria hapa ni wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Mawaziri, Wabunge, wakuu wa Vyama vilivyoshirikishwa na TANU,Wakuu wa Mashirika ya Kiserikali, Viongozi kutokana na Kifungu chochote cha Katiba ya TANU, Madiwani, na Watumishi wa Serikali wenye vyeo vya kati na vya juu(Kwa mujibu wa kifungu hiki kiongozi ni mtu au mtu na mkewe au mke na mumewe).
Siyo tu kwamba kifungu hicho kimekosea katika kumdefine Kiongozi ni nani lakini pia ni unfair, Haiwezekani Mke wangu awe kiongozi anayefungwa na Sharti la kutokuwa na hisa kwenye kampuni, asiwe na nyumba ya kupangisha n.k, halafu na mimi nisiye na interest katika mambo ya siasa nifungwe na vifungu hivyo, hicho kipengele ni unjust!
Je Azimio la Zanzibar lilisema watu wawe mafisadi?, la hasha
Je kuna Sheria za kupinga Ufisadi?-ndiyo zipo
Sasa je Azimio la Zanzibar ndilo lililosema mafisadi wasichukuliwe hatua za kisheria?-hapana
Binafsi mimi ninaona jambo la msingi ni la KATIBA NA SHERIA, weka maadili kwenye Katiba na Sheria KISHA HIZO SHERIA UZISIMAMIE KWELI KWELI hapo ndo utakuwa umekata mzizi wa Fitina, otherwise azimio peke yake bila kulipa msingi wa kikatiba ni rahisi kulifuta/kulivunja.