Prof. Issa Shivji bado tunahitaji Tanganyika huru

hata mm niliona kama kachemka kutokana na maelezo yake ya mwanzo.
 
Kweli kwa wasomi hawa bado kazi tunayo!! Yani leo ameongea mambo ambayo hapo mwanzoni wakati wa mchakato wa kukusanya maoni ya katiba alikuwa kwenye kipindi itv ni tofauti kabisa.mi hadi nilihisi tv yangu ina matatizo labda inaleta picha yake ila sauti c yake!!! Kweli inatia aibu kwa msomi wa kiwango chake anakubali kutumika!!!
 
Ikiwa mambo yasiyo ya muungano upande wa zanzibar yanashughulikiwa na serikali ya mapinduzi zanzibar.je upande wa Tanzania bara yanashughulikiwa chombo gani maana si ya muungano?
Swali la nyongeza ikitokea rais wa muungano akatokea Zanzibar na kukawa na mgogoro kati ya serikali ya muungano na serikali ya zanzibar na suala likawa zito ikabidi marais wa pande mbili walitatue.atatoka rais wa zanzibar ambae ni mzanzibari na rais wa muungano ambae pia ni mzanzibar je hakuna conflict of interest kwa rais wa muungano? Naomba ufafanuzi kamarade.
 
SINA nia mbaya na msomi huyu nguli wa mambo ya sheria hapa nchini ila elo nimeonesha wasiwasi wangu juu ya uelewa wake wa mambo ya kisheria hasa kwa tafsiri yake ya dhana ya dola na nchi, wasiwasi wangu uliibuka ple aliposema kuwa maana ya nchi yaani country katika katiba ya zanznibar linamanisha dola hasa kwa kutumia tafiiri ya kingereza akihusisha state ambayo kwa kiswahili ni taifa likiwa na maana nchi ikiwa na utawala sovereignty state huyu mzee leo ajatutendea haki hasa anapo chukua dhana ya utawala na kuifanya nchi, rasmu ya warioba inazungumzia wazi dhana ya nchi kuwa tanzania huku ikionesha utawala wa nchi ikiuweka katika sehemu kuu tatu yaani serikali kuu kama symbol ya muungano ikiwa na mambo machache sana, na serikali mama wa muungano mbili kwa maana ya serikali ya tanganyika na zanzibara na katoa sababu zote rejea randama ya rasimu, hotuba ya mwenyekiti wa tume!

Kitu kingne ni hoja mpya na za upotoshaji juu kukataa dhana ya jina na nchi ya tanganyika unafiki wa unaofanywa na watu mchana kweupe kuwa tangnyika ilikufa huku tukiendelea kuyaishi maisha ya kitangayika kwa sura ya bandia tanzania...! Swali la kufikirisha je uhuru wa ila 9 december tunao sherekea ni wa tanganyika au tanzania na kama ilikwosha kufa tunasherekea nini?

Mwisho spendi kuwachosha, ni nani atafuta historia ambayo haichagui matukio mazuri au mabaya ila hutegemea kutokea kwa matukio ambayo ndiyo chimbuko na mwanzo wake, anayedai tanganyika ni ukoloni kwasababu tu kuwa jina lilitokana na wakoloni atwambie kuhusu majina ya nchi yeyote duniani ambayo haikutokana na ukoloni. na kisha atuchambulie etimology ya neno tanzania kama halina element ya tanganyika mnayokataa kuwa ni jina la wakoloni, akiependa aende mbali zaidi atwambie maana ya SIWA rungu la bunge na atweleze lina maana gani! na kwa tanzania lina wakailisha nini!


Asanteni tujadili bil jaziba!
 
hawa maprofesa wetu wa kichina ni majanga tu,hakuna kitu,shivji amedhoofika sana.
 
Shivji ulianza vizuri, unamaliza vibaya kwa aibu! Mind you, hao jamaa wa ovyo sana, wanamtumia mtu kama toilet paper, wakiisha kutumia kama wanavyokutumia sasa, watakutupa tu kuleeeeee!!!!!!! Yuko wapi leo Lamwai????? Unayoeleza hayaingii akilini hata kwa mtoto wa darasa la nne, ni akili kubwa kuchezewa na akili ndogo. Looooh, Fedha Fedheha!!!!!!!!!
 
takujibu ki-Shivji Shivji...

Kwanza taelezea maana ya muungano, alafu tafatia maana ya Zanzibar tamalizia maana ya Rais alafu nadhani utakuwa umeshasahau naongelea nini.., mwisho kabisa taleta hoja ambazo hazizungumziwi hapa.
 
Kwanza kabisa swali la kwanza jibu unalo, kwani hata leo serikali ya JMT ndio inasimamia mambo yasiyokuwa ya Muungano Tanzania Bara.
Pili sheria ilishaweka utaratibu wa kushughulikia migongano ya Muungano. Na pia ikumbukwe kama mgogoro utahusu tafsiri ya kisheria basi Mahakama ya Kikatiba itatumika kutatua mkanganyiko huu. Bado sijaona ni mgongano upi ambao maraisi wanaweza kupata mikwaruzano kuutatua.
 

kuna migongano mingi sana na ndiyo maana kuna waziri katika ofisi ya makamu wa rais anae shughulikia muungano kuna masula kama hisa za zanzanzibar katika benki kuu kuna suala la o.i.c serikali ya muungano iliiomba zanzibar ijitoe ili yenyewe ijiunge kuna suala la zanzibar kuwa freeport kuna kutozwa ushuru mara mbili kwa magari yenye znz yakija bara kutaja kwa uchache mkuu.
 
shivji ametekwa na mahaba ya muungano,ameshindwa kubalance uchambuzi wake,ameyasimamia vizuri mambo ya muungano katka uchambuzi wake pale anapoona yana manufaa kwa zanzibar,hakuna lolote alilosema kuhusu tanganyka,'kwenye ardhi mbona hakuongea kwamba wazanzibar wanamiliki ardhi tanganyika kinyume cha sheria? ardhi si suala la muungano,,kuhusu mawaziri wa zanzibar kuongoza wizara zisizo za muungano,ni kinyume cha makubaliano ya mambo ya muungano,hata kama SHVJI KAPEWA CONSULTANCYA NA IKULU KUMSHAURI KIKWETE KUHUSU KATIBA MPYA ASIWEKE USOMI WAKE PEMBENI,NAJUA AMELEWESHWA NA MAMIA YA MAMILIONI ALIYOPEWA, sisi wananchi hatuna hayo mamia ya mamilioni lakini ukweli tunaujua,*anaishia kutoa nasaha kwa watanganyika,kwa wazanzibari ananukuu sheria na mambo ya muungano
 
Hivi huyu Prof. ni Mzanzibar au Mtanganyika? Mbona alikuwa akiitetea sana Zanzibar huku akiwa kama anajipendekeza kwa JK? Ni mawazo yangu tu

Sijapata Kuona Msomi Mnafiki na Hopeless Kama Huyu Na Ni Rasmi Sasa Kuwa Nimetokea Kumdharau. Anazeeka Vibaya Na Nahisi Kuna Sehemu Atakuwa Amebanwa Hivyo Kujinusuru Kwake Ni Lazima Awaunge Mkono La Sivyo Watalisanua na Nahisi Pengine Labda Njaa Imezidi Baada Ya Kustaafu Kufundisha UDSM na Ndevu Zake Utafikiri ZIVUMA ( Kinyume ) Ya Fisi.
 
kumbe Shivji wa Kilosa?! Kwa hiyo anatumika kisiasa? Nilivosikia tbc ndo wanarusha nilistuka sana, ila sasa ni kama nimeelewa ni kwa nini.

Hivi MJOMBA Hamkanyagi Kweli 0713????????????????????????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…