Prof. Janabi: Chama cha Figo Tanzania kitawasilisha pendekezo la kuvuna Figo za Marehemu

Jambo hili halina ubaya kwani dhumuni na malengo ni kuokoa uhai na kuboresha maisha maana maradhi ya figo yanasumbua Sana....

Mashaka na hofu ya wadau ni kuwa tunafahamiana namna ambavyo taasisi zetu zinavyofanya kazi katika mlango wa rushwa.......hili jambo la khiyari litageuzwa kuwa biashara matokeo yake watu wanaweza kufoji nyaraka ili tu ahalalishe kuuza FIGO la ndugu yake kama donor....
 
Mimi naona kama wakifikia kukubaliana hili basi FIGO la iwekwe kama sehemu ya mirathi kwa mwenye nayo ili hata akifa wanafamilia wanufaike walau.....
 
Mkuu umewaza mbali sana na uko sahihi ila sasaa tukatae Jambo zuri kama hilo la kuokoa UHAI?
 
Hata nywele yangu isibaki hospital 🤣🤣.nitoke kama nilivyoingia.
Hivi ndugu wa marehemu wamegharamika kumtibu ndugu yao.pesa zimewatoka mmewakamua aswaa.baada unakuja kuwaletea habari za ku donate figo kwa maneno matupu watakuelewa?
Wosia wako uheshimiwe mkuu tuanzishe chama chetu kiitwe NFZ (Nabaki na figo zangu) na ukae ukijua tushakupa u weka hazina
 
Mkuu umewaza mbali sana na uko sahihi ila sasaa tukatae Jambo zuri kama hilo la kuokoa UHAI?
Nadhani kinachotakiwa ni kuliwekea mipango au utaratibu mzuri ili kufunga hiyo mianya ya wajanja wajanja....
 
TISs wajiandae kuandaa kitengo Cha kushinda makaburini japo wapo ila wawe kivingine
 
PROF JANABI UNAKOSEA SANA, HAYA MASWALA ACHANA NAYO HARAKA, WAGONJWA WATAUWAWA KWA MAKUSUDI ILI FIGO ZICHUKULIWE. PROF UKIENDELEA NA HAYA MANENO BASI UTALAANIKA. MASWALA YA UGONJWA NI SENSITIVE SANA NA KAMA HUNA MANENO YA BARAKA YA KUZUNGUMZA KWA WANANCHI BASI VYEMA UKAWA KIMYA
 
Figo inakuwa haijafa yenyewe? Ufafanuzi tafadhari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…