Prof. Janabi: Chama cha Figo Tanzania kitawasilisha pendekezo la kuvuna Figo za Marehemu

Prof. Janabi: Chama cha Figo Tanzania kitawasilisha pendekezo la kuvuna Figo za Marehemu

Hili kwa macho ya kiroho,naona sio sahii,mungu alivyo kuumba aliweka hivyo vitu.iweje marehemu mtoe figo zake bila rithaa yake.
 
Mkuu Wala usiende maili buku mbele jiulize tu kwanini damu tunauziwa na Ili Hali Kuna watu wanajitolea Bure kabisaa damu Yao?

Lini umeenda hospital ukakuta damu zipo za kutosha na wanatoa Bure?
Hakika muungwana.....

Hili suala linaweza kuwa na nia njema lakini kwa tunavyojuana waTanzania linaweza kufungua mlango mwingine wa maafa.....

Unashtukia ndugu yako ametolewa figo imeishauzwa......
 
Kila mtu afe kivyake anayekufa kwa kukosa figo afe tu na anayekufa na figo zake afe tusimpangie Mungu yeye ndie anayejua amepanga nini
 
Nahs harufu ya human organ trafficking(not sure of the spelling)... hapa tanzania itashika kasi.
 
Nahs harufu ya human organ trafficking(not sure of the spelling)... hapa tanzania itashika kasi.
Sahihi, hili jambo linaweza kuwa maafa makubwa katika jamii kama hii yetu.
 
Mimi si mjuvi sana,ila mtu anapofikwa na umauti figo inaweza kuendelea kufanya kazi?
Na je ni serikali au wananchi wapewe pendekezo hilo?
 
MY TAKE: Kwa namna yoyote hali hii ikipita inaweza kuleta mtafaruku kwenye kuvuna hizo FIGO kwa marehemu au watu kumaliziwa wakiwa wodini ili wawahishe FIGO kwa wahitaji.
Hivi unajua hadi ili jambo kufanyika ni mpaka consent ya muhusika ? Ni kama kutoa Damu kwani Hospitali wanakushikia Bunduki utoe au unajipeleka ?

Hence kinachohitajika na cha maana wala sio muswada Bungeni bali ni Elimu kwa wananchi ili waone umuhumi na kufanya hili jambo.., Ni upuuzi kufukia viungo wakati vinahitajika kwa wengine waliopo hai
 
Nahs harufu ya human organ trafficking(not sure of the spelling)... hapa tanzania itashika kasi.
Hata kwa nchi zinazoruhusu organs donation haziruhusu organ business..., huwezi kuuza organs zako its illegal all over the world
 
Hivi unajua hadi ili jambo kufanyika ni mpaka consent ya muhusika ? Ni kama kutoa Damu kwani Hospitali wanakushikia Bunduki utoe au unajipeleka ?

Hence kinachohitajika na cha maana wala sio muswada Bungeni bali ni Elimu kwa wananchi ili waone umuhumi na kufanya hili jambo.., Ni upuuzi kufukia viungo wakati vinahitajika kwa wengine waliopo hai
Kama ni utashi wa mtu kufanya hivyo basi usiite upuuzi......

Kuwa ni khiyari ya mtu akufanyi watu tusitoe maoni kwa kuwa sote tunajua namna ambavyo mambo yanaendeshwa hapa nchini.......watu wanaweza kufoji vyeti wakati umezidiwa na huna kauli wakauza viungo vyako bila ridhaa yako
 
Kama ni utashi wa mtu kufanya hivyo basi usiite upuuzi......
Hakuna mtu anayelazimishwa ila ndio hivyo zamani watu walikuwa wanazikwa na wafalme wakiamini kwamba wataenda kuwafanyia kazi huko wanapokwenda..., ilikuwa utashi wao baadhi ila mwisho wa siku tunajua kwamba haikua sahihi...

Sasa kama unaona it makes sense kwa watu kuhangaika kwa kukosa viungo na kupoteza nguvu kazi ni sawa (na wengine wanafanya hivi kwa sababu na kitamaduni na kiimani) utaona kwamba tunahitaji elimu ili watu waelewe kwamba kuna uhitaji wa hivyo tunavyozika ili vioze
Kuwa ni khiyari ya mtu akufanyi watu tusitoe maoni kwa kuwa sote tunajua namna ambavyo mambo yanaendeshwa hapa nchini.......watu wanaweza kufoji vyeti wakati umezidiwa na huna kauli wakauza viungo vyako bila ridhaa yako
Sasa wakifanya hivyo itakuwa ni Jinai kama Jinai zote zilivyo..., sababu watu wanaweza kutumia visu kuua watu hatuwezi kuacha kutengeneza vitu ili vitusaidie kukata vitunguu...
 
Bado pia upandikizaji ni gharama sana aseee ,kuna mtu namfahamu figo zote mbili zimefeli ameshapata wa kumtolea ila bado muhimbili wanataka Mill 30 bado hiyo hela ni kubwa kwa mtu wa kawaida
 
Naanza kumpinga mwenyewe hapa hapa.

Wazo lake ni jema sana sema tumegumbwikwa na ufisadi na uroho mnoo

Imagine ni lini umeenda hospital ukaptiwa damu Bure?

Kila Leo watu wanajitoa damu Bure lakini ukienda unauziwa Tena Hela ndefu!!

Hii Nchi hapana Wacha nizikwe na viungo vyangu vyote tu hawana utu.

Uliuziwa damu au ulilipia huduma?

Huduma hailipwi kwa maombi nyie watanganyika. Duniani kote huduma sio bure kama hulipi wewe jua kuna mtu anakulipia, ila organs na damu ni bure.
 
Back
Top Bottom