Prof. Janabi hakuna mwili unaozuiwa kwa kushindwa kulipia gharama za mochwari ila ni kwa kushindwa kulipa madeni ya gharama za matibabu

Prof. Janabi hakuna mwili unaozuiwa kwa kushindwa kulipia gharama za mochwari ila ni kwa kushindwa kulipa madeni ya gharama za matibabu

Cannabis

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2014
Posts
11,557
Reaction score
33,535
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Mohamed Janabi amesema miili huzuiwa mochwari kutokana na madeni ya gharama za matibabu ambazo marehemu alikuwa akidaiwa pindi alipokuwa hai na si kushindwa gharama za mochwari.

 
Ni njia gani bora ya kumdai marehemu/ndugu wa marehemu deni la matibabu?
1000017209.jpg
 
Amefafanua vizuri sana:

Kwamba hakuna maiti inayozuiwa, ni watu wanapotosha ili kutafuta public sympathy.

Kama ndugu wameshindwa kulipia gharama alizotumia marehemu pindi akiwa hai, basi utaratibu ni kuleta vielelezo ikiwamo barua ya mjumbe wa mtaa, balozi, au mwenyekiti kuthibitisha.

Tatizo wanaloface ni kwamba watu wengi hizi taratibu watu hawataki kuzifuata.
 
Wananchi hata tusiiseme muhimbili hapa wakulaumiwa ni serikali tu!, maana yenyewe ndio inaratibu gharama zote na utaratibu wao ndio wanaweza kusema mwananchi achangie asilimia ngapi za matibabu ama asichangie kabisa!.
so mi nachoona janabi yeye ataendelea kusimamia utaratibu wa alichowekewa tu huyo ni muajiliwa tu hata akiambiwa kuanzia leo matibabu ni bure kwake ni sawa tu!, ye kikubwa mshahara wake unaingia sio shida zake!.

hapa ni serikali kuangalia namna gani itaweza kuokoa jahazi kwa aidha kubadilisha utaratibu na kupunguza gharama za matibabu, na ningependekeza ikitokea mtu amefariki ktk hospitali ya serikali basi zile gharama alizotumia kipindi akiwa hai ziweze kupunguzwa kwa asilimia kadhaa!, ili walau kuondosha mzigo kwa wafiwa na kuonyesha ujali kidogo kwa wafiwa, nchi yakwetu sote hii hata kama tunastahili kulipa kodi lkn kuna muda nayo hiyo kodi ipunguze ukali kidogo.
mtu umehangaika na mgonjwa let's say hata miezi mitatu kuna gharama zake, bahati mbaya akafariki ulipe gharama za matibabu na ulipe gharama za mochwari bado msiba wenyewe una gharama zake..😅

oya hivi serikali huwa mnajua experience ya hicho kitu kweli au kwasababu viongozi nyie mifukoni zimejaa, tena wengine hata hizo za mifukoni mwenu hamgusi hapo fungu linatoka serikalini!!, bado mtu atapta na rambirambi, hapohapo serikali itampa mpaka usafiri!.
mnamfikiriaje mwananchi wa kawaida mtu kama mlinzi anaelipwa laki na nusu kwa mwezi..???😅

oya acheni masihara babuu!
 
Kuhusu masuala ya kugombea nafasi ya mkurugenzi mkuu wa WHO Kanda ya Afrika, Profesa Mohamed Janabi anaweza kuwa na changamoto kutokana na tuhuma zinazohusiana na usimamizi wa madeni ya matibabu. Kawaida, mtu anayegombea nafasi kama hiyo anatarajiwa kuwa na rekodi nzuri ya maadili na uongozi, na masuala kama haya yanaweza kuathiri hadhi yake.

Kuhusu sheria za WHO, hakuna sheria maalum zinazosema kuwa maiti zinapaswa kuzuiwa mochwari kutokana na madeni. Hata hivyo, ni muhimu kwa nchi na taasisi za afya kufuata maadili na taratibu zinazohusiana na usimamizi wa miili, ili kuhakikisha kwamba heshima ya marehemu inahifadhiwa na familia zinapata haki.

Kwa hiyo, ikiwa Profesa Janabi anataka kugombea, itakuwa muhimu kwake kushughulikia masuala haya kwa njia ya uwazi na kujenga imani katika uwezo wake wa kuongoza.
 
Haina noma tutawaachia maiti ili awalipe
 
Back
Top Bottom