Wananchi hata tusiiseme muhimbili hapa wakulaumiwa ni serikali tu!, maana yenyewe ndio inaratibu gharama zote na utaratibu wao ndio wanaweza kusema mwananchi achangie asilimia ngapi za matibabu ama asichangie kabisa!.
so mi nachoona janabi yeye ataendelea kusimamia utaratibu wa alichowekewa tu huyo ni muajiliwa tu hata akiambiwa kuanzia leo matibabu ni bure kwake ni sawa tu!, ye kikubwa mshahara wake unaingia sio shida zake!.
hapa ni serikali kuangalia namna gani itaweza kuokoa jahazi kwa aidha kubadilisha utaratibu na kupunguza gharama za matibabu, na ningependekeza ikitokea mtu amefariki ktk hospitali ya serikali basi zile gharama alizotumia kipindi akiwa hai ziweze kupunguzwa kwa asilimia kadhaa!, ili walau kuondosha mzigo kwa wafiwa na kuonyesha ujali kidogo kwa wafiwa, nchi yakwetu sote hii hata kama tunastahili kulipa kodi lkn kuna muda nayo hiyo kodi ipunguze ukali kidogo.
mtu umehangaika na mgonjwa let's say hata miezi mitatu kuna gharama zake, bahati mbaya akafariki ulipe gharama za matibabu na ulipe gharama za mochwari bado msiba wenyewe una gharama zake..😅
oya hivi serikali huwa mnajua experience ya hicho kitu kweli au kwasababu viongozi nyie mifukoni zimejaa, tena wengine hata hizo za mifukoni mwenu hamgusi hapo fungu linatoka serikalini!!, bado mtu atapta na rambirambi, hapohapo serikali itampa mpaka usafiri!.
mnamfikiriaje mwananchi wa kawaida mtu kama mlinzi anaelipwa laki na nusu kwa mwezi..???😅
oya acheni masihara babuu!