Prof. Janabi hakuna mwili unaozuiwa kwa kushindwa kulipia gharama za mochwari ila ni kwa kushindwa kulipa madeni ya gharama za matibabu

Marehemu ni mlipa mlipa kodi wenu, mpk wanashindwa au wanavutana kulipia ghalama za matibu inamaana hao ni hoehae, na ghalama za muhimbili si za kitoto, kwan mkisamehe mtapata hasara gani,
 
Sawa. Sasa ni njia gani nzuri ya kudai deni la matibabu lililoachwa na maiti? Au mtu asipewe huduma mpaka awe amelipa?
Mgonjwa anaekufa na ndugu hawana uwezo, maiti isamehewe tu, au wanaokufa hapo muhimbili ni wengi sana kiasi wakisema wawe wanasamehe maiti taasisi itafirisika!!
 
Kuna gharama za matibabu na gharama za huduma za mochwari kama kihifadhi mwili wa marehemu na kuukosha
Kuzuia mwili kwa sababu ya gharama yoyote ni ushenzi.

Ni dalili ya jamii iliyokosa utu mpaka kwenye msiba.

Jamii iliyoshindwa kujiwekea utaratibu wa kusema "hawa watu wana msiba, wamefiwa, tuwaache wazike tutamalizana nao deni baada ya kuzika".

Ila sitegemei watu wote waelewe hii dhana, kwa sababu walio katika jamii fulani mara nyingine hushindwa kujua matatizo ya jamii hiyo kwa sababu wameyazoea sana mpaka wanayaona ni kawaida, si matatizo.
 
Wakileta huo uthibitisho ndo nini kitabadirika? huoni hapa ndo ujinga Pumpuni kabisa wa kuhangaisha watu bure. wamefiwa na wao ndo walikuwa wanamuuguza wamesema hawana hela ya kulipia gharama hizo sasa hiyo mijorojongo yoote ya nini?
 
kwa kauli hii who atatupotezea muda tu,
 
Kwahio tushukuru Serikali kwa kutumia Kodi zetu kutupatia huduma za Mortuary (being reactive) badala ya kutupatia huduma za Matibabu ? Kama vipi waongeze gharama kwenye mortuary wapunguze za matibabu huenda hata vifo vikapungua.
 
Wasije wakakumbana na familia yangu, aisee wataachiwa huo mzoga hapo hospitali itajua yenyewe mahali pa kuipeleka.
 
Umeshindwa kumtibu kafa sasa unamdai nini na huo mbona kama wizi
 
Sasa si ni kitu kile kile tyuuh. Huyu Professor Diet yaje ya chakula abadilishe.
 
Wakileta huo uthibitisho ndo nini kitabadirika? huoni hapa ndo ujinga Pumpuni kabisa wa kuhangaisha watu bure. wamefiwa na wao ndo walikuwa wanamuuguza wamesema hawana hela ya kulipia gharama hizo sasa hiyo mijorojongo yoote ya nini?
Ikiwa ivo si kila mtu atasema hana pesa?

Misamaha ipo ila taratibu ni lazima zifuatwe!

Kumbuka mwisho wa siku CAG lazima apite, na ukisamehe bila taratibu na miongozo iliyopo utapata hati chafu!
 
For sure huo ni unyama mkubwa
 
Mgombea wa nafasi ya ukurugenzi WHO Africa.

Sheria ya kuidai maiti ipo Tanzania pekee.

Yaani mtu amekosa huduma bora za matibabu (wengi) anakufa kisha mnamdai pesa ya matibabu.

CCM ni shetani mkubwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…