Prof. Janabi hakuna mwili unaozuiwa kwa kushindwa kulipia gharama za mochwari ila ni kwa kushindwa kulipa madeni ya gharama za matibabu

Tatizo wahudumu wa hospital unakuta hawana hata muda wa kuwaelewesha vizuri ndugu wa maiti kuhusu utaratibu wa malipo wanajibu shortcut as if kila mtu anazielewa taratibu
 
Pamoja na madhaifu ya serikalini ila Wabongo tunapenda kulalamika.
Ina maana mnataka mtibiwe Bure?

Hapa sioni kosa la Janabi, kila akikwepa kulipa Kwa kisingizio Cha maiti hizi taasisi za afya zitakuwa na Hali mbaya sana.

Sikubaliani na Serikalini Kwa mambo mengi sana ila kwenye hili wabongo ustarabu wetu Bado mdogo tukidekezana kulipa kisa maiti, Hakuna mtu atakaelipa hata mmoja na hizi taasisi zitajifia halafu sisi tena tutarudi kuanza kulalamika
 
Ukiwa msomi halafu ukaingia kwenye mfumo wa CCM,bora hata kuku aliyekatwa kichwa.
 
Pamoja na kuwa tunafaham machungu ya mtu aliyefiwa na sote tumeshafiwa na wapendwa wetu naombeni tuwe tunafikiria vizuri hasa changamoto zinazohitaji utatuzi mgumu
Nafikiri mada kama hizi zinatakiwa kujadiliwa kwa lile jukwaa la GREAT THINKERS sio huku ambapo wengi wapo busy kulaumu badala ya kutoa ushauri....

1. Kwa hospitali inakuwa imeshawekeza fedha ambazo kwa Bahati mbaya ndio hivyo tena mgonjwa akafariki; Itazipataje gharama zake za matibabu? Je familia zinafuata taratibu za kuomba kusamehewa deni?
2. Sasa tunatakiwa tuisaidie Hospitali namna nzuri ya kushuhulika tatizo lenyewe, kusema waachiwe wakazike, hii wainaita short term plan; hilo bado sio Suluhisho, kwani watu watafanya ndio utaratibu wa kutolipa hadi waone kama mgonjwa ameruhusiwa....
3. Mimi nafikiri kwa sasa tungejikita kuelimisha familia masikini juu ya utaratibu wa kufuata ili kupata msamaha....sambamba na KUELIMISHANA umuhimu wa kuwa na Bima nk
4. Binafsi siwezi kumlaumu Prof Janabi kwa hili kwani yeye ni mtekelezaji tu wa sheria.
 
Kama kajibu hivyo kwamba mwili unazuiwa kwaajili ya gharama za mochwari kakosea.

Na wewe kama unamsahihisha kwamba mwili hauzuiwi kwa gharama za mochwari bali kwaajili ya gharama za matibabu na wewe pia umekosea.

Kuna mwongozo unaoelekeza mwili wenye deni uwe handled vipi. Na hiyo handling ni kuhakikisha mwili unatoka siyo kuuzuia.

Kama kuna mwongozo unaoujua unaharamisha nilichokisema waweza uonyesha
 
Inakuwa vipi kama ndugu watashindwa kulipagharama hizo?
 
Hiyo maiti isipo lipiwa deni wataenda kuiuza wapi ili kufidia hizo gharama inayodaiwa.....!
 
Kwanini hospital binafsi hawakutwi na haya mambo?

huwa zinakutwa pia.... Nafuu yao ni kuwa, wanaokwenda huko Hospitali za Binafsi, wengi wana Bima na pia wale wenye nafuu ya maisha hivyo, wakijichanga huweza kulipa bila shida na hata kama kuna WACHACHE watashindwa, inakuwa rahisi kuwafikiria kwani ni wachache...
 
Kupitia comment za wachangiaji kwenye huu uzi......nimegundua wabongo tuna shida mahali hasa kwenye upande wa kufikiria...... mihemko ipo juu kuliko akili....
 
Kwa hiyo mtu akilazwa Muhimbili akifariki basi hospital ifute deni kisa mgonjwa amefariki, lol,
Watu wote tumefiwa na tunalipa deni la wapendwa wetu tunachukua mwili na kuendelea na taratibu zingine, na kama hatuwezi kulipia deni basi kuna taratibu za msamaha zipo, aidha tunafutiwa deni lote au tunalipa nusu na serikali nusu, taratibu zingine zinafatwa,
Tuacheni mihemko katika vitu sensitive, hospital inahitaji fedha ili kujiendesha.
 
Huyu sasa ndio great thinker.
Wabongo bwana wao baadala ya kutumia akili kufikiri wanatumia hisia🤣🤣🤣🤣

Yale yale ya magu na wasomi wa mikopo. Wee hujalipa deni naongeza riba unaanza sema nakuonea. Kama hutaki kuonewa ungelipa ili serikari iendelee kuwakopesha wengine
 
Hili jambo naona kama Janabi anaonewa hapa,kipi bora kiubinadam kukataa mtu asitibiwe mpaka alipe au kumtibu na bdae kumdai?.Best way ni matibabu bure,swali tunaweza? Kama nchi?
 
Kuna haja gan kulipia gharama za matibabu wakat wenyewe wameshindwa kumtibu na kuzuia kifo chake...?
Vifo vingi Africa n "man made death". Doctor wanasababisha vifo vya wapendwa wetu kimakusudi sheria ichukue mkondo wake.
 
Kuna matamko wanatoa wasomi wetu, u aona ni bora watoto wetu wawe tu wagamga wa kienyeji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…