Prof. Janabi: Kitu hatari zaidi ni sukari na wanga. Ataka watu kula wakihisi njaa kwani mwili hauendeshwi na ratiba ya chakula

Prof. Janabi: Kitu hatari zaidi ni sukari na wanga. Ataka watu kula wakihisi njaa kwani mwili hauendeshwi na ratiba ya chakula

Hivi vitu havina fomula, jamaa alikuwa anafuata ratiba ya lishe bora lakini amekatika katika umri mdogo tu ila kuna jamaa kula kula hadi sasa anadunda na anaendelea kula na kitambi juu 🤣
Anafanya mazoezi mkuu
 
Wabongo kwa ujuaji🫔🫔 .
Kwahiyo mtu mpaka amekuwa profesa ina maana hajui tofauti ya wanga na sukari.
Kachemka ndio,tena pakubwa.sukari na wanga ni kitu kimona.Yaani sawa na kuongelea chumba na nyumba.
Vipi mkuu,ulikimbia umande au ulitembea na ma_H...kuna ni?
 
Mkurugenzi wa hospitali ya Muhimbili, Profesa Mohammed Janabi amesema mpaka sasa wanawake 100 wamewekewa puto na wanaume wachache. Prof ameongeza kuwa puto ni kitu kimoja lakini nidhamu kwenye chakula ni kitu kingine.

Janabi amesema kitu hatari zaidi kwenye mwili ni sukari na wanga na wala si mafuta kwasababu mwili hautunzi wanga wala sukari bali huvibadilisha kuwa mafuta. Ametaka watu kupunguza matumizi ya vitu vyenye sukari, utamu mkubwa na sukari yenyewe.

Prof Janabi amesema matatizo ya kushindwa kupata watoto, moyo, kiharusi, magonjwa ya kupumua, vifo vya ghafla asilimia mkubwa vinachangiwa na uzito usio sahihi na kula mara kwa mara. Profesa amesisitiza kutopeleka mwili kwa utaratibu wa chakula bali wale chakula wanapohisi njaa.
Sukari ni kitu mbaya sana hasa sukari ya kuongeza kwenye vyakula au vinywaji. Tangu niache kuweka sukari kwenye chai najisikia vizuri sana.
 
Back
Top Bottom