Mkurugenzi mtendaji wa hospitali kuu ya taifa ya Muhimbili, Profesa Janabi ameelezea mbinu za kuepuka kuzeeka mapema ambapo ameelezea kama ifuatavyo;
1. Tembea hatua 10,000 kwa siku
2. Kula kwa wastani
3. Punguza wanga
4. Epuka vitu vyenye sukari
5. Epuka sigara, pombe
7. Pata muda kidogo wa kupumzika
Akaongezea, vitu hivyo haviitaji hata senti 5 ya gharama. Akasema tena watu hawafi kwa sababu ni wazee, watu wanakufa kwa sababu ni wagonjwa, ukisoma vitabu vya dini watu walikuwa wanaishi miaka zaidi ya 100.
Leo hii unaweza kukutana na mtu anamiaka 40 na mwingine 30 ukafikiri yule mwenye miaka 30 ndio ana miaka 45.
Kwa hizo mbinu ningetegemea Janabi awe na babe face lakini yeye ndio amekongoroka na ngozi kupauka kama ya marehemu ama kama vile ana miaka 90.
Janabi aache watu waishi. Kuchukua tahadhari za kawaida kwenye maisha ni jambo jema ila Janabi anataka tuwe extreme, ngozi zetu zikose nuru kama marehemu haiwezekani.
Kwa hizo mbinu ningetegemea Janabi awe na babe face lakini yeye ndio amekongoroka na ngozi kupauka kama ya marehemu ama kama vile ana miaka 90.
Janabi aache watu waishi. Kuchukua tahadhari za kawaida kwenye maisha ni jambo jema ila Janabi anataka tuwe extreme, ngozi zetu zikose nuru kama marehemu haiwezekani.
Janabi mwwnyewe sura imepauka utadhani sio profesa wa afya. Hii ni kutokana na mwili kukosa lishe hivyo ngozi inafubaa na kukosa nuru.
Kufuata kanuni za afya ni jambo jema ila sio kuwa mtumwa kwa dunia kwa sababu ya lishe.
Kila jambo hapa duniani lafaa ila hakikisha unadhibiti kiasi kwa ajili ya afya yako
Kuna watu wengi tu hawaishi kama Janabi ila wana afya imara na bora kuliko huyo Janabi mwenyewe.
Hapa duniani zakuambiwa nawe changanya na za kwako.
Kwa namna anavyo amini Janabi leo, yumkini kuna maisha na vyakula kwa dunia ya leo hawezi kuwapatia watoto wake akiamini kuwa vitawadhuru afya lakini vyakula hivyohivyo pengine ndivyo vimemkuza akiwa kinda mikononi mwa mama yake.
Sipingani sana na Janabi kwenye suala la lishe ila napingana na nadharia zake za kutia chumvi masuala ya lishe ambayo hata yeye mwenyewe kiuhalisia huwa hayaishi.