Na kwa wale wagonjwa wengine ambao waliugua na mwisho kufariki, vipi Tuseme Yesu hakutaka kujitukuza kwao? au Aliwapotezea? Au aliwadharau?
Kupona kwa prof jay Kwanza ni uwepo wa msaada wa kifedha uliopatikana kupitia Serikali yake na michango ya watu binafsi, maana Kwa maradhi yake kama kapuku kutoboa ni ngumu
Na mwisho kabisa ni bahati yake tu kuwa hai hadi muda huu, hayo mambo ya Yesu hivi au Yesu vile mbona wapo wanaofia Makanisani wakila maombi usiku kucha
Kwetu kuishi ni Kristo kufa ni faida.
Wafilipi 1:21-27
Kwangu, kuishi ni Kristo, na kufa ni faida zaidi.
Lakini, kama kwa kuishi nitaweza kufanya kazi yenye faida zaidi, basi, sijui nichague lipi!
Nakabiliwa na haya mawili yaliyo sawa. Natamani kuyaacha maisha haya nikakae pamoja na Kristo, jambo ambalo ni bora zaidi; lakini ni jambo la maana zaidi kwenu kama nikiendelea kuishi.
Nina hakika ya jambo hili, na hivyo najua kwamba nitaendelea kuishi pamoja nanyi nyote, ili nipate kuongeza maendeleo yenu na furaha katika imani.
Basi, nitakapokuwa nanyi tena mtakuwa na sababu ya kuona fahari juu yangu katika kuungana na Kristo Yesu.
Basi, jambo muhimu ni kwamba mwenendo wenu uambatane na matakwa ya Injili ya Kristo, ili kama nikiweza kuja kwenu au nisipoweza, nipate walau kusikia kwamba mnasimama imara mkiwa na lengo moja, na kwamba mnapigana vita kwa pamoja na mnayo nia moja kwa ajili ya imani ya Injili.