Prof JOYCE NDALICHAKO haya yakufikie hata kama yatakuuma, lakini ndio ukweli wenyewe

Prof JOYCE NDALICHAKO haya yakufikie hata kama yatakuuma, lakini ndio ukweli wenyewe

Ninafurahi sana pale nikimuona prof ndalichako akiongea kizungu kwa sababu ananifanya nione kuwa mimi ninaweza sana kiingereza na nina pronounce vizuri sana maneno yake ilhali hata hiyo master sina
Huwezi mcheka mtanzania kwakutojua kingereza ila asipojua kiswahili ndio aibu
 
Inglish ya kuchomelea na kuunga kwa super glue.
Inglish kavu kama ule wali wa mgagaa na upwa.
Inglish mbaya kama barabara ya kibondo to kasulu.
 
Also aah, we, we political aah will by ensuring that we we we make aah the result known for example we have exhibitions for students to participate in science and technology so those who are doing aah innovative things we make them aah, we make public exhibition, so that people can come and see and appreciate aah, whot why is it important to to to invest in education and our country is the among the 19 countries which we aah we commited to kenyata decleration ahh"[emoji848][emoji15][emoji2827][emoji1544][emoji1544]
alikariri au sio mkuu!
 
Daaah umenukuu kabisa,Yani anaongea Kama anapresha
 
Sio lugha yake mama acheni uraia kingereza ndo nn mazwazwa wajinga hakujielewi kosa lake nn n kujifanya wasomi nyote weusi kingereza hakiwahusu
Unawezaje kumjudge mtu kwa kingereza

Basi kamchukueni mtoto wa miaka 7 England anajua kingereza muje kumpa uprofessor au kumuabudu kabisa ..

Nyuzi izi hazifai katika maadili ni kumdhalilisha mtu na ni kinyume cha mila na desturi zetu kwani hyo ni lugha ya kigeni hata ujue kingereza sio kwamba utatushikia akili labda mazwazwa wenzio
 
By the way Mh Ndalichako ni mtaalam wa elimu,she is not a Linguist..Mbona wachina wana kiingereza kibovu huko UN kuliko sisi?

Hoja ya msingi hapa ni kwamba ni lini Tanzania itaamua haswa (angalau hatua kwa hatua) kufanya mabadiliko ktk elimu yake duni? Mkuu hii elimu yetu ni mbovu mno na haikidhi hata kidogo mahitaji ya dunia ya leo. Serikali haioneshi juhudi,wala mpango,wala mkakati wa kututoa hapa. Ukitaka kuthibitisha hili,fanya assessment ya uelewa wa hawa wasomi wetu kutoka vyuo vikuu!

Binafsi naamini profesa anajua namna ya kufanya kuiboresha elimu yetu tena katika tanuru hilihili la uchumi wetu duni. Kikwazo ni kwamba masuala ya kitaaluma ktk nchi hii yanafanywa kisiasa! Taaluma ni useless hapa kwetu mbele ya siasa...na wanasiasa wetu wengi hawana elimu au ni zao la elimu yetu mbovu! Mama anafanya kazi kwa kuzingatia mipaka ya kisiasa...tusitegemee taaluma yake itumike ipaswavyo! Ukimtazama ktk maamuzi yake wakati wa awamu ya tano na hii ya sita ni ukinzani...hii itakupa picha nzuri

Sina ushahidi ila naamini kuna mabeberu somewhere wameshika rimoti na wanaivuruga elimu yetu! Inaonekana hata marehemu hakua mdau wa elimu,yeye aliamini ktk miundombinu peke yake la sivyo angefanya jambo hapa! Mimi kama mwalimu naumia sana kuona hakuna kitu serious kinafanyika kutoa elimu bora ktk taifa langu nilipendalo! Nachukia sana!
 
Huwezi kulinganisha China na Tanzania kwa english ukabaki na credibility ya uelewa na uchambuzi. wachina wanasoma kichina na wanatumia kichina katika kila kitu. Kuongea Kiingereza kwao ni juhudi za kutafsiri wanachokielewa ili kiweze kuwasilishwa na kueleweka kimataifa.

Tanzania Tangu shule ya msingi tunasoma kingereza hadi chuo kikuu. Ofisini tunatumai kiingereza kama moja ya llugha rasmi. Halafu mtu ashindwe kuongea kingereza bado umpigie chapuo kwa kulilnganisha na wachina? Ujinga huu.
By the way Mh Ndalichako ni mtaalam wa elimu,she is not a Linguist..Mbona wachina wana kiingereza kibovu huko UN kuliko sisi?

Hoja ya msingi hapa ni kwamba ni lini Tanzania itaamua haswa (angalau hatua kwa hatua) kufanya mabadiliko ktk elimu yake duni? Mkuu hii elimu yetu ni mbovu mno na haikidhi hata kidogo mahitaji ya dunia ya leo. Serikali haioneshi juhudi,wala mpango,wala mkakati wa kututoa hapa. Ukitaka kuthibitisha hili,fanya assessment ya uelewa wa hawa wasomi wetu kutoka vyuo vikuu!

Binafsi naamini profesa anajua namna ya kufanya kuiboresha elimu yetu tena katika tanuru hilihili la uchumi wetu duni. Kikwazo ni kwamba masuala ya kitaaluma ktk nchi hii yanafanywa kisiasa! Taaluma ni useless hapa kwetu mbele ya siasa...na wanasiasa wetu wengi hawana elimu au ni zao la elimu yetu mbovu! Mama anafanya kazi kwa kuzingatia mipaka ya kisiasa...tusitegemee taaluma yake itumike ipaswavyo! Ukimtazama ktk maamuzi yake wakati wa awamu ya tano na hii ya sita ni ukinzani...hii itakupa picha nzuri

Sina ushahidi ila naamini kuna mabeberu somewhere wameshika rimoti na wanaivuruga elimu yetu! Inaonekana hata marehemu hakua mdau wa elimu,yeye aliamini ktk miundombinu peke yake la sivyo angefanya jambo hapa! Mimi kama mwalimu naumia sana kuona hakuna kitu serious kinafanyika kutoa elimu bora ktk taifa langu nilipendalo! Nachukia sana!
 
[emoji23][emoji23][emoji23] aibu hii kwa Prof mzima aisee, bongo hii usitishwe na title ya u Dr au Prof, wengi ni vilaza wenye GPA kubwa ila kujieleza hawawezi
Mtetee mwanamke mwenzio kha! [emoji16][emoji16][emoji2099]
 
Hatuwezi kumcheka mtanzania kwa kutokujua kiingereza lakini tunaweza kumcheka msomi mwenye PHD kwa kutokujua kiingereza.

Haiwezekani mtu ashindwe kuongea lugha ambayo kaitumia karibia miaka 22 ya usomi wake
Lugha inaenda kwa kufifia kama huitumii yeye hajazaliwa uingereza kusema lugha yake ya kwanza ni kingereza . Narudi kuncheka mtanzania kwasababu hajui kingereza ni ushamba wa hali ya juu. Wewe je unaweza ongea kama yeye au zaidi yake
 
nakusalimu kwa jina la jamuhuri.
katika hali ambayo ni ya kawaida, umezuka mjadala juu ya uwezo wako wa kujieleza kwa kutumia lugha ambayo kwa asilimia 90 ndio iliyokutunuku kiwango cha elimu ulicho nacho (prof) na watanzania wengi wameenda mbali na kusema kuwa elimu yako ni ya ubabaishaji. mimi napingana nao, naamini unaweza kufanya bora zaidi ya hapo na wala sibezi jitihada ulizofanya mpaka sasa katika kuboresha mfumo wa elimu yetu hapa nchini.
kielelezo:
katika mkutano ulioshiriki hivi karibuni umesema haya
"Also aah, we, we political aah will by ensuring that we we we make aah the result known for example we have exhibitions for students to participate in science and technology so those who are doing aah innovative things we make them aah, we make public exhibition, so that people can come and see and appreciate aah, whot why is it important to to to invest in education and our country is the among the 19 countries which we aah we commited to kenyata decleration ahh"
View attachment 2048403
katika kufasiri hiki ulichokisema hapa kwa niaba ya watanzania wengi ambao hawajaelewa kabisa ulikusudia kusema nini ni kwamba
"sisi wanasiasa tunahakikisha kuwa matokeo yanakuwa bayana kwa mfano, tuna maonyesho kwa ajili ya wanafunzi kushiriki katika sayansi na teknolojia hivyo kwa wale wanaofanya uvumbuzi tunafanya maonyesho ya hadhara ili watu waje waone na kupongeza/kukubali ni kwanini ni muhimu kuwekeza katika elimu na nchi yetu ni moja kati ya nchi 19 ambazo ni washirika wa azimio la kenyata"

kutoka katika maelezo hayo ni wazi kwamba sio tu unawadanganya hao uliokaa nao katika kikao bali unakiri kabisa kuwa mfumo wa elimu uliopo Tanzania si muafaka katika dunia hii iliyo jipambanua kuwa inategemea sayansi na teknolojia katika maendeleo ya watu na vitu kwa kuzungumza mambo ambayo eti yanafanyika (maonyesho ya uvumbuzi wa sayansi na teknolojia) wakati hayafanyiki kwa kiwango cha kitaifa na kwa lugha yako mbuvu iliyojaa makosa kibao.

naomba nikuulize swali hili, ni shule gani hapa nchini inafundisha sayansi na teknolojia katika kiwango cha kuamsha ari ya uvumbuzi kwa wanafunzi wake?

Binafsi ninafahamu kuwa elimu tuliyonayo imejaa nadharia kwa asilimia zaidi ya 80 na aslimia za vitendo zilizobaki ni vitendo vilivyofanywa na wazee waliosoma miaka ya 70 huko mpaka leo. Mfano tangu miaka ya nyuma mafunzo kwa vitendo kidato cha nne kushuka chini ilihusisha panzi, tandu, samaki mihogo nk. mpaka leo ni hayo hayo, ni lini unategemea mwanafunzi anayefanya vitendo hivi kuwa mshindani na faida kwa taifa katika upande wa sayansi na teknolojia ambao sasa upande huu umejikita katika kurahisisha maisha ya watu kwa uvumbuzi ambao ni muafaka kabisa kulingana na mahitaji ya mwanadamu?

leo hii wewe waziri wa elimu unaonekana mjinga kwa sababu kiwango chako cha elimu na uwasilishaji wa yale yaliyomo kichwani kwako havina uhusiano kabisa na hii ni kwasababu ya mfumo huu mbuvu ambao umeshiriki katika kukujenga na kukufanya uwe na uwanja finyu wa utendi kuanzia katika ubongo wako mpaka matokeo ya masuala unayoyafanya. na hili si kwako tu, ni kwa watanzania wengi ambao nao wanashiriki kukucheka.

Ikumbukwe ujinga ni kivumishi kinachotumika kwa mtu au kikundi cha kijamii ambacho hakina ujuzi wa vitu. Neno ujinga linaweza kutaja mtu kukosa mafundisho au elimu.

nini kifanyike?
katika kipindi hiki ambacho wewe waziri mwenye dhamana ambaye niliwahi kusikia mahali kuwa katika usomaji wako umewahi kuwa Tanzania one, umeshikilia wizara hii nyeti, unahitaji kufumua mfumo mzima wa elimu kwa kuhakikisha kuwa mfumo mpya unaingizwa ambao sasa utajikita katika kuwajenga wanafunzi wa ngazi zote nchini wawe na ujuzi wa juu wa sayansi na teknolojia na pia wawe washindani katika taaluma zao watakazochagua kiutendaji kuliko nadharia hii iliyojengeka kuwa msomi anatakiwa awe na uwezo mzuri wa kujieleza kwa lugha ya kiingereza. (nadharia sasa ichukue asilimia 30 huku vitendo vikiwa asilimia 70.

hii itasaidia kuzalisha wasomi ambao watakuwa na uwezo wa kuigeuza elimu yao kuwa pesa kama mnavyohubiri kila siku kuwa wasomi wanapaswa kujiajiri ili kupambana na wimbi la ukosefu wa ajira unaokumba waja wengi hapa nchini,

yangu ni mengi lakini kwa haya machache niliyoyaandika natumaini utayafanyia kazi na kutusaidia kuzalisha wasomi ambao hawatakuwa aibu kitaifa na kimataifa.
Don't turn a blind eye on my article, otherwise historia itahukumu. ukweli unauma ila usiposemwa unaleta ugonjwa wa kiharusi kwa anayeuficha na mimi sitaki kiharusi.

kacnia.
Tunapendekeza atumie Swahili
 
Sio lugha yake mama acheni uraia kingereza ndo nn mazwazwa wajinga hakujielewi kosa lake nn n kujifanya wasomi nyote weusi kingereza hakiwahusu
Unawezaje kumjudge mtu kwa kingereza

Basi kamchukueni mtoto wa miaka 7 England anajua kingereza muje kumpa uprofessor au kumuabudu kabisa ..

Nyuzi izi hazifai katika maadili ni kumdhalilisha mtu na ni kinyume cha mila na desturi zetu kwani hyo ni lugha ya kigeni hata ujue kingereza sio kwamba utatushikia akili labda mazwazwa wenzio
soma mada sio unakurupuka
 
Back
Top Bottom