Prof. Kabudi aieleza Jumuiya ya Kimataifa kuwa Tanzania haijawahi kushindwa vita ya aina yoyote

Sio lugha ya mwungwana. Prof ametegwa na system akaingia kingi (kama makonda kugombea kigamboni).. Atatumbuliwa soon kuridhisha wafadhili.. Atakuwa mbuzi wa kafara.. Serikali iljshakosea,wanatafuta namna ya kutoka
 
ila watanzania wanajua kujitutumua ila kwa wakati wa nyerere ilikuwa inawezekana ila kwa sasa sijui......

🙄 🙄 🙄
 
Nchi za afrika elewa haziwezi kamwe kujiendesha bila misaada ya au mikopo ya nje
Kila nchi ina kopa wamarekani wanadaiwa na China mkuu. Hivyo kukopa siyo shida hata hao wanaokopesha wanafanya hivyo ili wapate faida bila kukopesha wanakufa kwa njaa pia. Maana yake tunategemea wote!
 
kabudi alitakiwa kuwa mtu wa kutafuta suluhu na sio jeuri hii. Ukimwona hata ongea yake unagundua kuwa huyu mrtu sio mwanadiplomasia kabisa!
 
Kila nchi ina kopa wamarekani wanadaiwa na China mkuu. Hivyo kukopa siyo shida hata hao wanaokopesha wanafanya hivyo ili wapate faida bila kukopesha wanakufa kwa njaa pia. Maana yake tunategemea wote!
Unajihesabu nawe ni mjuaji, kwa kurahisisha mambo kihivyo!

Na si ajabu ukawa unashikilia nafasi mhimu ndani ya serikali hii inayopotosha kila jambo mradi tu ionekane inajitutumua.

Haya, hata nyinyi mna jeshi, kama walivyo nalo wamarekani. Unataka tuwape uwanja mkapimane nguvu?

Inawezekana kabisa usielewe maana ya mfano huo niliokuwekea hapo; na hata kama umeelewa utakaza tu shingo mradi uonekane mjuaji.

Watu wa hovyo sana nyinyi.
 
ndipo tulipofika au bado safari inasonga @ kabudi...
 

That’s right, prof! We have to stand our ground; we aren’t anyone’s colony!
 
Kila nchi ina kopa wamarekani wanadaiwa na China mkuu. Hivyo kukopa siyo shida hata hao wanaokopesha wanafanya hivyo ili wapate faida bila kukopesha wanakufa kwa njaa pia. Maana yake tunategemea wote!
TUNAWEZA KUKATAA MISAADA TUKAKOPA HILI HALINA SHIDA KABISA LAKINI EMBU TATHMINI JINSI DENI LA TAIFA LINAVYOPAA AT ATIME NA MISAADA TUNAPATIWA SASA MISAADA ISITISHWE NA TUWE TUNAKOPA TU NCHI ITAUZWA NDUGU
 
Huyu jamaa alinifanya nihairishe kusomea PHD pamoja na kuchaguliwa kusomea kozi hiyo Mlimani.

Yaani ukimuangalia unaona kabisa anaongea aliyotumwa akaseme Prof mzima unalazimishwa kuongea pumba kwa ajili ya kulinda nafasi yako
Prof Kabudi anajitoa ufahamu! Mwl Nyerere alikuwa na ubavu wa kuwakemea na hata kuwazuia hao anaowaita mabeberu. Mwl hakusita hata mara moja kutembelea na kuhutubia Umoja wa Mataifa, nchi mmoja mmoja na kuwapiga makofi (kauli kantu) bila woga. Aliweza hayo, mmoja kwa kuwa alikuwa na msimamo thabiti, alikuwa na mikono safi, aliaminika lakini pia alikuwa na nguvu ya ushawishi kwa ncha mbili- kwa wale Magharibi na kwa wale wa Mashariki! Ile vita baridi ilikuwa platform nzuri sana kwa Mwalimu.

Kwa sasa hivi, Prof Kabudi hajitambui, na wala hana plan B. Ukweli nisingependa nchi yangu inampigia magoti nchi nyingine, lakini si vyema, nchi yangu ikatumia mabavu kupata watawala, kukamata watu, kuhodhi vyombo vyote vya habari (CCM wamenunua vituo vyote vya Television - naamini bei haikufika kununua Azam TV, wamezuia magazeti yote huru na kuruhusu magazeti na vituo vya propoganda tena visivyo na lugha ya kiustrabu). Kwangu hizi tabia pia kwa taifa letu ndio KUPIGIA MAGOTI- KUJIDHALILISHA! Prof Kabudi anatakiwa aelekeze huko sio vingine!
 
Uhuru wa Tanzania ni kuwabambikia kesi kesi uonevu unyanyasaji uovu mateso manyanyaso kuubaka kuunajisi kuulawiti uchaguzi mkuu kwa njia haramu za kishetani, hii ndiyo Nchi huru
 
Kabudi kichwani kasalia na darasa la nne tu, vile alivyovisomea vyote vimefutika kichwani hana kilichosalia kwenye Ubongo ndiyo maana kawa na mikwara ya kichaa cha dog
 
kweli wameapa kutumikia watu lakini hawajaapa kudharauliwa na wazungu kwa ajili ya misaada, BORA KUFA UMESIMAMA KULIKO KUISHI UMEPIGA MAGOTI.
 
Huyu naye na mahistoria yake ya kale kama kasuku. Sijui amekariri?

Vita ya idi Amini inatuhusu nini sisi? Watu wanahitaji chakula, maisha bora na economic security.

Stori za Idi Amini za kazi gani sasa! Hili zee nalo kwa kukariri halijambo!

Halafu hiyo sovereignty ni kitu gani? Kuua watu na kufanya uharamia bila kuulizwa?

Huyo profesa uchwara hatambui kwamba Tanzania ina wajibu wa kuheshimu sheria za kimataifa?

Ukiua watu wako recklessly kwa kutumia jeshi ni uhalifu wa kivita na unatakiwa kushughulikiwa na taasisi za kimataifa ikiwemo kuwekewa vikwazo, kupelekwa ICC au hata kushughulikiwa kijeshi kama Libya na Gambia!

Hakuna sovereignty ya kuua watu na kuwafanyia uharamia wa kijeshi. You must be answerable!

Huyu nae ni profesa wa sheria? Anafundisha family law NO WONDER!
 
Kuwa na degree 1, 2 au 3 haiondoi ujinga kama una njaa, hawa maprofesa wa Tz wanadhihirisha hilo
Wanaojiita maprofesa Tanzania ni tofauti na maprofesa wengine Duniani, wengi wa maprofesa wa Tanzania ni wasomi feki walioiba mitihani kununua vyeti kusoma kiujanja janja tu mpaka wakamiliki vyeti, ndiyo maana Akili zao ni za hovyo hovyo zisizofanana hata na maprofesa wa Sudan kusini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…