Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kila nchi ina kopa wamarekani wanadaiwa na China mkuu. Hivyo kukopa siyo shida hata hao wanaokopesha wanafanya hivyo ili wapate faida bila kukopesha wanakufa kwa njaa pia. Maana yake tunategemea wote!Nchi za afrika elewa haziwezi kamwe kujiendesha bila misaada ya au mikopo ya nje
No."Chemical" Ally
Unajihesabu nawe ni mjuaji, kwa kurahisisha mambo kihivyo!Kila nchi ina kopa wamarekani wanadaiwa na China mkuu. Hivyo kukopa siyo shida hata hao wanaokopesha wanafanya hivyo ili wapate faida bila kukopesha wanakufa kwa njaa pia. Maana yake tunategemea wote!
WAZIRI WA MAMBO YA NJE TANZANIA PROFESA PALAMAGAMBA KABUDI AWAJIBU MABEBERU, HATUJAWAHI KUPIGISHWA MAGOTI, UCHAGUZI ULIKUWA HURU NA HAKI
Waziri wa Mambo ya Nje Prof. Palamagamba Kabudi aijibu EU - Umoja wa Ulaya kufuatia kikao cha bunge hilo la ulaya huko makao makuu ya EU kutishia uwezekano wa vikwazo kupitia Kamati yake Mambo ya Nje ya Bunge la Umoja wa Ulaya kujadili uwezekano wa kuibana Tanzania kwa vikwazo vya aina mbalimbali ikiwemo kusitisha msaada wa kuifadhili bajeti ya Maendeleo ya Tanzania.
Prof. Palamagamba Kabudi ameomba msaada wa vyombo vya habari nchini kuisaidia serikali ya Tanzania kwa kujitokeza na kuieleza Jumuiya ya Kimataifa ukweli wa mambo. Na kueleza Nyerere aliwahi kuwadindia Germany na United Kingdom na kukataa misaada na fedha zao. Prof. Palamagamba Kabudi anashangaa waTanzania kuanza kutetemeka ktk mitandao ya kijamaii kuhusu nchi yetu kuwekewa vikwazo.
Prof. Palamagamba Kabudi amesema Tanzania haifuati sera za kidiplomasia za kujitenga kufanya kazi na Jumuiya za Kimataifa. Hivyo waziri Prof. Kabudi amesema Tanzania ipo tayari kukaa ktk meza moja na wadau wa kimataifa kuzungumzia mapungufu yaliyopo lakini si kwa kuburuzwa na mabeberu bila kuwa na facts mezani.
Prof. Palamagamba Kabudi amesema kuwa watu wahuni wachache wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Ulaya EU hawawezi kuitisha na kuidhalilisha Tanzania na watambue Tanzania ni nchi huru.
Prof. Palamagamba Kabudi amesema maneno hayo mazito akiongea na Wafanyakazi wa Wizara hiyo muhimu ya Mambo ya Nje akatumia fursa hiyo kujibu uvumi kuwa Tanzania itanyimwa misaada na kuwakumbusha wafanyakazi hao kutembea vifua mbele kwani Tanzania siyo nchi ndogo kidiplomasia, kimsimamo, kiji-Geopolitiki na kiushawishi kimataifa.
.....................................................
EU Parliament Committee on Foreign Affairs discussion on Tanzania
Tujikumbushe walioitwa "wahuni wachache" na Prof. Kabudi, tarehe 19 November 2020 jijini Brussels kwa dakika 45 mfululizo walisema nini kuhusu Tanzania ktk kikao cha Kamati ya Mambo ya Nje cha Bunge la Jumuiya ya EU
Tazama / sikiliza dakika 45 za mjadala ktk kamati hiyo:
TUNAWEZA KUKATAA MISAADA TUKAKOPA HILI HALINA SHIDA KABISA LAKINI EMBU TATHMINI JINSI DENI LA TAIFA LINAVYOPAA AT ATIME NA MISAADA TUNAPATIWA SASA MISAADA ISITISHWE NA TUWE TUNAKOPA TU NCHI ITAUZWA NDUGUKila nchi ina kopa wamarekani wanadaiwa na China mkuu. Hivyo kukopa siyo shida hata hao wanaokopesha wanafanya hivyo ili wapate faida bila kukopesha wanakufa kwa njaa pia. Maana yake tunategemea wote!
Fact umenena mkuu.Utu upi anao uongelea Kabudi? Endelea kutoa historical speeches za darasani ukijisahau kwamba upo field.
Prof Kabudi anajitoa ufahamu! Mwl Nyerere alikuwa na ubavu wa kuwakemea na hata kuwazuia hao anaowaita mabeberu. Mwl hakusita hata mara moja kutembelea na kuhutubia Umoja wa Mataifa, nchi mmoja mmoja na kuwapiga makofi (kauli kantu) bila woga. Aliweza hayo, mmoja kwa kuwa alikuwa na msimamo thabiti, alikuwa na mikono safi, aliaminika lakini pia alikuwa na nguvu ya ushawishi kwa ncha mbili- kwa wale Magharibi na kwa wale wa Mashariki! Ile vita baridi ilikuwa platform nzuri sana kwa Mwalimu.Huyu jamaa alinifanya nihairishe kusomea PHD pamoja na kuchaguliwa kusomea kozi hiyo Mlimani.
Yaani ukimuangalia unaona kabisa anaongea aliyotumwa akaseme Prof mzima unalazimishwa kuongea pumba kwa ajili ya kulinda nafasi yako
vyovyote ulivyoelewa lakini ujumbe umeshawafikia bwana zenuAna address Diplomatic issue Akiwa kavaa Viatu vya Ministry of Defence
Vita ya Congo na Sanction za EU wapi na wapi ?
Uhuru wa Tanzania ni kuwabambikia kesi kesi uonevu unyanyasaji uovu mateso manyanyaso kuubaka kuunajisi kuulawiti uchaguzi mkuu kwa njia haramu za kishetani, hii ndiyo Nchi huruJalala bwana
Propaganda full na mimacho kilo mia elfu nane
Sovereignity kwa jambazi na uaji?
Wanapoiba na kuua watu ndio soverignity inasemwa wanataka....
Nyerere alikua na sababu serious na za kweli,jalala sababu zake ni uuaji na ujambazi wa kura...
Anadai ana takwimu na data ku-prove their case....data feki walizozipika wapeleke ziaminiwe,tunataka data kutoka kwa independent investigator na sio vitakwimu vilivyopikwa na jalala mwenyewe
Nchi huru yenye ruksa ya kuiba na kuua watu wake...kama uhuru ndio huo,basi na ufe!
Jalala
Kabudi kichwani kasalia na darasa la nne tu, vile alivyovisomea vyote vimefutika kichwani hana kilichosalia kwenye Ubongo ndiyo maana kawa na mikwara ya kichaa cha dogProf Kabudi anajitoa ufahamu! Mwl Nyerere alikuwa na ubavu wa kuwakemea na hata kuwazuia hao anaowaita mabeberu. Mwl hakusita hata mara moja kutembelea na kuhutubia Umoja wa Mataifa, nchi mmoja mmoja na kuwapiga makofi (kauli kantu) bila woga. Aliweza hayo, mmoja kwa kuwa alikuwa na msimamo thabiti, alikuwa na mikono safi, aliaminika lakini pia alikuwa na nguvu ya ushawishi kwa ncha mbili- kwa wale Magharibi na kwa wale wa Mashariki! Ile vita baridi ilikuwa platform nzuri sana kwa Mwalimu.
Kwa sasa hivi, Prof Kabudi hajitambui, na wala hana plan B. Ukweli nisingependa nchi yangu inampigia magoti nchi nyingine, lakini si vyema, nchi yangu ikatumia mabavu kupata watawala, kukamata watu, kuhodhi vyombo vyote vya habari (CCM wamenunua vituo vyote vya Television - naamini bei haikufika kununua Azam TV, wamezuia magazeti yote huru na kuruhusu magazeti na vituo vya propoganda tena visivyo na lugha ya kiustrabu). Kwangu hizi tabia pia kwa taifa letu ndio KUPIGIA MAGOTI- KUJIDHALILISHA! Prof Kabudi anatakiwa aelekeze huko sio vingine!
kweli wameapa kutumikia watu lakini hawajaapa kudharauliwa na wazungu kwa ajili ya misaada, BORA KUFA UMESIMAMA KULIKO KUISHI UMEPIGA MAGOTI.Aliyoainisha Mhe Palamagamba Kabudi ni sahihi kabisa kwa upande mmoja wa sarafu lkn kwa mwenye akili aweza kuchambua hotuba ktk maeneo kadhaa kama ifuatavyo:-
(i). Kuhusu Mwl Nyerere kurudisha fedha kwa Uingereza na Ujerumani miaka ya 60 ilikuwa sawa - sasa kwa miaka hii ya 2020 ni sahihi kurudisha fedha sababu ya kulalamikiwa juu ya uchaguzi kughubikwa na mauaji, kutesa, na kukamata wapinzani?
Sawa ameeleza kuwa duniani kote huwa hakuna uchaguzi huru wala haki kwa standards ya 100 lkn amejiuliza kwa nini katiba ilitungwa, amejiuliza kwa nini Sheria zilitungwa? - Ni kwamba viwe vipimo vyetu ktk utendaji wa kila siku;
(ii). Madai ya kero za uchaguzi (kabla, wakati na baada ya uchaguzi). Hivi tumefika hatua ya kubariki mauaji, unyanyaswaji na ukandamizaji wa kidemokrasia kiasi cha kutambia dunia! Mie nilidhani kwamba angeeleza umma kuwa mambo yaliyojitokeza kwenye uchaguzi yanaendelea kushughulikiwa na mamlaka za ndani na kuahidi kupata suluhu kwa njia za mazungumzo na makundi yanayovutana - sasa chukulia mfano fedha za misaada zizuiliwe - hivi tutakuwa ni ukoo wa binadamu gani?
(iii). Viongozi, ndio wenye maslahi makubwa ya kitaifa sasa wasitengene njia za kuikosesha nchi misaada sababu bado tunaihitaji dunia, bado tuna changamoto kwenye afya, elimu, maji, kilimo, usafiri na usafirishaji, huduma za kiuchumi nk nk - kama tunatofautiana nao tutofautiane kwa sababu zenye uzito kama kukataa ushoga, udini, ukabila au ukanda lkn sababyinayotufanya leo tukosane ni ya kitoto na tunatakiwa kuizuia.
Mhe Palamagamba Kabudi, liangalie taifa hili limejaa watu wenye uhitaji sasa maslahi ya kisiasa kwa kundi dogo si sawa - wanaoathiriwa na kuzuiliwa fedha ni CCM, CDM, ACT, CUF, NCCR na vyama vingine pamoja na wasiokuwa na chama - ninyi mmeapa kutumikia hawa hawa ambao mnataka kuwasitishia misaada - NOT Good at all!
Msakila M Kabende
Kigoma
point gani kama siyo kupayuka?Ameongea point sana huyu mzee
Wanaojiita maprofesa Tanzania ni tofauti na maprofesa wengine Duniani, wengi wa maprofesa wa Tanzania ni wasomi feki walioiba mitihani kununua vyeti kusoma kiujanja janja tu mpaka wakamiliki vyeti, ndiyo maana Akili zao ni za hovyo hovyo zisizofanana hata na maprofesa wa Sudan kusiniKuwa na degree 1, 2 au 3 haiondoi ujinga kama una njaa, hawa maprofesa wa Tz wanadhihirisha hilo
Yawezekana Babu kabudi anakula NdumuKwa mwana diplomasia hii ni Lugha chafu kuwaita wawakilishi wa kamati ya bunge wahuni wachache.