Prof. Kabudi aieleza Jumuiya ya Kimataifa kuwa Tanzania haijawahi kushindwa vita ya aina yoyote

Prof. Kabudi aieleza Jumuiya ya Kimataifa kuwa Tanzania haijawahi kushindwa vita ya aina yoyote

Tunanunua ugomvi ambao tunajua hatuwezi kushinda. Yesu alisema mfalme anayetaka kwenda vitani hufanya hesabu kwanza ya uwezo wa jeshi la adui. Akiona lina uwezo kumzidi hufanya majadiliano kabla ya kuingia vitani. Hii ndiyo hekima!
 
Tanzania ya 1965 tofauti kabisa na hii ya sasa prof. Alitosha kuwa muhadhiri tu diplomasia haiwez wafadhiri wetu wataona hiyo ni official response ya nchi mpaka itapelekea kuchukua hatua zaidi ya apo bado Tanzania nchi ndogo saana zaidi ya asilimia 50 ya budget yetu tunawategemea wao.
Alipaswa kutolea ufafanuzi jinsi gani pesa ya kupambana na Corona 27m [emoji387] zilivyo tumika wakati tuliitangazia dunia kwamba Tanzania has Corona free,
Alipaswa atoe majibu ya tuhuma za ukiukwaji wa msingi ya utawala bora na kukosekana kwa utawala wa kidemokrasia katika nchi ambalo ndio lengo la misaada yetu tunayopokea
 
Tanzania tulivunja uhusiano na serikali ya Harold Wilson ya Uingereza tarehe 15 Desemba 1965 kwa sababu ya Ian Smith kujitangazia uhuru wa Southern Rhodesia na Wilson kukaa kimya tu. Tulirudisha mahusiano mwezi wa 7 1967 ( sio 1972 kama nimemsikia Mheshimiwa vizuri). Tulikosa mkopo wa £7.5 milioni. Hatukuchukua mkopo. Sio kwamba tulirudisha pesa ambazo tuliishapewa.

Mwaka 1981 mercenaries 44 wakiongozwa na Michael Hordes walijaribu kupindua Seychelles. Wanajeshi wetu wakazima hilo jaribio. Vita hasa ambayo tulishinda ni ile dhidi ya Iddi Amin. Lakini iliathiri sana uchumi wetu kiasi ambacho nchi za magharibi na taasisi zake zilipotubana ili tubadilishe mfumo wetu wa kibiashara Mwalimu hakuwa na jinsi bali kung'atuka na kumuachia Ali Hassan Mwinyi ambae hakuchelea kukubali matakwa ya IMF. Hiyo ni vita ya kiuchumi ambayo bila shaka tulishindwa.

Hawa tunaowaita wahuni hawana haja ya kutuwekea vikwazo. Wao wakiondolea upendeleo wa tariff kwenye bidhaa chache tunazowauzia uchumi wetu utaathirika sana. Hamna haja ya kujibishana nao hadharani. Waziri ana mamlaka ya kumuita balozi wa EU na kumpa ujumbe wa kuwapelekea mabosi wake. Alichofanya sio diplomacy.

Amandla...
 
Acha uoga wa maisha kijana!! Pambana na hali yako acha kufikiri misaada sana! Mtegemea misaada huwa hatoboi kwenye maisha! Be informed!
 
I thin ata wanae kuna wakati wanajuitia kuwa na baba kma uyu
Wazee wengne ovyo sanaaa
 
Kumbe Kabudi naye yuko hivyo, yani naye ni bangi tu. Wewe kweli unaweza ukausukuma mkono unaokulisha na bado ukawa na akili.

Zimbabwe kabla ya kuwekewa vikwazo akina Mugabe walikuwa na kauli za kipumbavu kama hizi lkn leo Zimbabwe ni "The Banana Republic".
 
Mbona mnawatetea mabeberu nyinyi au tayari mmeshaolewa na mabeberu?
 
Acha uoga wa maisha kijana!! Pambana na hali yako acha kufikiri misaada sana! Mtegemea misaada huwa hatoboi kwenye maisha! Be informed!
Nani kazungumzia misaada? Unadhani kubanwa ni kunyimwa misaada tu? Halafu una jeuri yakuniambiwa niwe informed!

Amandla...
 
EGOISM mabaya yatakapolifika taifa miongoni mwa watu ambao hawataathirika kiuchumi ni pamoja na viongozi prof kabudi awe na mwono mpana zaidi hasa juu ya community ya watanzania wote IMPACT ITAKAPOKUJA WAO POSHO ZAO BENEFICIARY ZAO ZITAKUWA PALEPALE SO THEY WOULDNT FEEL ANY THINGS
 
Acha kuwa na wasiwasi mkuu! Chapakazi tu usitegemee sana misaada!
 
Back
Top Bottom