Prof. Kabudi awataka Mabalozi kujipanga na kutafuta fursa za masoko ya bidhaa za Tanzania

Prof. Kabudi awataka Mabalozi kujipanga na kutafuta fursa za masoko ya bidhaa za Tanzania

Mabalozi wanaoiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nje ya Nchi wameelekezwa kujipanga, kushiriki na kutafuta fursa zitakazowezesha bidhaa mbalimbali za Tanzania kupata masoko ya uhakika katika nchi walizopo.

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi wakati akizungumza na mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi na kuongeza kuwa , Ilani ya Chama cha Mapinduzi inatamka bayana juu ya diplomasia ya uchumi sambamba na kuimarisha sauti ya Tanzania na taswira yake katika medani ya uhusiano wa kikanda na kimataifa.

Prof. Kabudi ameongeza kuwa ili kufanikisha hilo Balozi zinapaswa kuimarisha ushiriki wa Tanzania katika jumuiya nyingine za kimataifa zikiwemo, Indian Ocean Rim Association, Indian Ocean Tuna Commission, South South Commission, South West Indian Ocean Fisheries Commission.

Aidha amewataka Mabalozi hao kuzingatia maelekezo ya Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi aliyoyatoa wakati akizundua Baraza la Wawakilishi ya kutaka Uchumi wa Bluu kupitia uvuvi wa Bahari Kuu unakuwa na manufaa kwa Wananchi hususani katika kuongeza mapato, ajira na kukuza uchumi kwa kuzingatia kuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ni ya Muungano.

Pia Prof. Kabudi amesema Serikali inatambua na kuthamini mchango unaotolewa na Watanzania waishio nje ya nchi (Diaspora) katika maendeleo ya Taifa na kuzielekeza Balozi zianze na ziboreshe kanzi data ya Diapora ikiwa ni pamoja na kuwahimiza kuanzisha Jumuiya zao.

“Natambua kazi hiyo inaendelea na kwa sasa tuna data za diaspora takriban 98,658 na kuna jumuiya 77 za diaspora. Nichukue fursa kusisitiza umuhimu wa Balozi zetu kuboresha na kuharakisha zoezi hili kwa kubuni njia mbalimbali za kuwaandikisha”.Amesema Prof. Kabudi

Mkutano huo wa Prof. Palamagamba John Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi umehudhuriwa pia na Naibu Waziri, Mhe William Tate Ole Nasha,Katibu Mkuu Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, Wakurugenzi na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Balozi wa tanzania nchini Kuwait, hajui anachotakiwa kukifanya . Yeye na yule mwendazake walipeana ubalozi tu.
 
Watoto walishindwa kutamka "kalamaganda kabugi!!" Hivi kwanini baadhi ya wasomi wetu tunaowaamini na kuwapa nafasi wanatuangusha?
 
Wengi mnao kashifu mawaziri na viongozi wengine wa awamu ya tano, tukifatilia elimu zenu wengi wenu ni form2/form4 basi, Watanzania walio soma mpaka vyuo vikuu hawawezi kupoteza muda wao wanakashifu, beza beza binadamu wenzao wanatumia lugha ya mipasho ya taarabu kama ya Khadija Kopa.
Yule aliyejisifu ana digrii saba yuko wapi siku hizi? Au nae hakuwa Khadija Kopa kwa taarabu zile?
Wasomi wanaodharaulisha elimu hudharaulika...
 
Wengi mnao kashifu mawaziri na viongozi wengine wa awamu ya tano, tukifatilia elimu zenu wengi wenu ni form2/form4 basi, Watanzania walio soma mpaka vyuo vikuu hawawezi kupoteza muda wao wanakashifu, beza beza binadamu wenzao wanatumia lugha ya mipasho ya taarabu kama ya Khadija Kopa.
We ni pumbavu kweli.sio kila mtu unaemuona hapa jukwaani ufikiri ameishia form 2 kma ww,hata kama basi elimu hiyo ya kina Kabudu hatuna Ila sina ujinga wa kujitoa ufahamu na kua mchumia tumbo kama huyo propesa wa jalalani.
 
Hivi ile elimu ya kabudi inatusaidia nn sisi kama taifa!? Hakuna anachotusaidia zaidi ya hasara ya kuharibu mahusiano yetu alivyopewa kile cheo Cha waziri wa mambo ya nje.
 
Hili zee fata upepo kweli....Leo kutafuta soko LA bidhaa toka TZ,twambie kwann waligoma kuja kuweka uwekezaji Tanzania..
 
We ni pumbavu kweli.sio kila mtu unaemuona hapa jukwaani ufikiri ameishia form 2 kma ww,hata kama basi elimu hiyo ya kina Kabudu hatuna Ila sina ujinga wa kujitoa ufahamu na kua mchumia tumbo kama huyo propesa wa jalalani.
Baadhi ya hasara za ukosefu wa elimu ya kutosha ni kama unavyo jidhilisha hapa - mtu anae jiamini na amelimika vya kutosha hawezi kuanza kutukana tukana watu ovyo anapo shindwa kujenga hoja zenye mshiko, kwa bahati mbaya na wewe ni victim anae sumbuliwa na inferiority complex ndio maana weakness yako inaishia kuwatukana watu ovyo.

Hivi ile elimu ya kabudi inatusaidia nn sisi kama taifa!? Hakuna anachotusaidia zaidi ya hasara ya kuharibu mahusiano yetu alivyopewa kile cheo Cha waziri wa mambo ya nje.
Kweli? Unaonaje ukimshauri Rais S. S.S.Hassan akupatie nafasi ya Dk. Kabudi tuone utatuletea mabadiriko gani yenye tija ndani ya Wizara ya mambo ya nje, kumbuka talking is cheap.
 
Back
Top Bottom