Prof Kabudi: Kati ya pesa na heshima ya nchi yetu, tutasimamia heshima. Tuko tayari kuwasikiliza na kujadiliana kwa heshima

Kauli kama hizi zitatupelekea tususwe then mifumo ya kupata external funds ifungwe then tuanze kukamuana humu humu nchini na ndiyo maana issue kama kila mtumishi kuwa na TIN number tumeanza kuandaa mazingira ya kukamuana hadi utumbo maana ma.vi wameshayamaliza
 
Safi sanaaaaaaaa Prof. Kabudi ni lazima ifikie sehemu watuheshimu na sisi.

TANZANIA IS SOVEREIGN STATE.
Uko sahihi kwenye sovereign state....ila lazima tukubali nchi za dunia ya 3 tuna uhuru wa bendera,kucompose our national anthem..........wakikutana ma Rais wa US,Urusi,Comoro,Mauritius,Ufaransa,Zambia,Malawi,Tz siyo level sawa japo zote ni nchi huru....hata kama kutakuwa na red carpet.....21 guns salutes .Tukubali lazima hii ngoma tuicheze vizuri
 
Nendeni mkaishi huko basi,yaani watupangie kila kitu tuwaangalie tuu
Sasa mnaomba hela zao za nini mjomba, mnapangiwa sababu mnaomba mpunga wao, acheni kuomba muone kama watawapangia. Baniani mbaya lakini kiatu chake dawa
 
Huyo hana utu anamuita Rais Mungu, ndio prof mjinga kuwahi kutokea duniani tangu ulimwengu kuumbwa
 
Nyinyi hamjaelewa Kabudi katumwa na bosi wake kutoa hayo majibu, maana hiyo ni akili ya boss wake mzee wa kukurupuka bila kufikiri. Yeye wewe anatenda halafu kufikiri ndio kunafuata. Yaani mapimbi ya CCM yana akili za ajabu sana yaani yanajifaragua kwa watu wanaoyasaidia bajeti kwa 45% bila aibu halafu hayana hata kiwanda cha toothpicks, hayana hata cha kutengeneza pini ulungu.

Halafu mazao ya biashara including madini mtaenda kuuza wapi nyie mapimbi? China mwenyewe anapigwa vikwazo na Marekani mpaka analia ije kuwa nyie malofa.
 
Ni hatari kuwa na madiplomasia kama hawa. Jambo linalogombaniwa ni jingine, naye anajibu au kuelewa jingine! Ulaya haitaki kuwatawala nyie, wala kuwaamulia. Kila wanachotaka ni kuona haki zile zilizokubalika na nyie wenyewe mkazikubali na kutia saini katika Azimio la Umoja wa Mataifa: uhuru na haki za binadamu, haki za kiraia, utawala wa sheria, uhuru wa maoni na kukusanyika, uhuru wa raia kuchagua serikali waitakayo= demokrasia. Hayo yote mmeyakubali. Sasa hili la kusema Tanzania ni soveign country na bla bla bla…..mlipokubali ilikuwa ni lip service tu siyo? Yaani mwuue, mwibe, mpige watu risasi …...mtu akisema, madam ni mweupe….ni Ukoloni?

Si mlisema mtajitawala wenyewe nyie, ili yale maovu yote ya Wakoloni yasiwepo? Kweli! Hakunauchaguzi wowote duniani ulio 100% safi. Tofauti ni kuwa nchi nyingine watu wana uhuru kusema hivyo, na wana haki ya kupinga matokeo na kujaribu kurekebisha, naam, hata Marekani! Waweza kusema hivyo Tanzania ya sasa?

Halafu kuna misingi na vigezo wazi duniani kwa uchaguzi kuwa 'huru na wa haki, na matokeo yake kuwakilisha matakwa halisi ya wananchi'. Hili si jambo la kukisiwa tu. Uhuru wa wote kuwakilishwa katika vyombo vya habari sawa sawa, uhuru wa kufanya mikutano waitakayo, wakati watakao na mahali watakapo, Tume Huru ya Uchaguzi nk.
Vyote hivi vimetupiliwa mbali, halafu uuambie ulimwengu kuwa uchaguzi ulikuwa huru na wa haki, na kulazimisha wakubali!
 
Sasa mnaomba hela zao za nini mjomba, mnapangiwa sababu mnaomba mpunga wao, acheni kuomba muone kama watawapangia. Baniani mbaya lakini kiatu chake dawa
Kwanza hao wanatakiwa kutulipa fidia ya unyama waliotufanyia kipindi cha colonization pia sisi tuna resources za kutosha kwahiyo wasituzingue
 
Halafu kwanza nani kampa mic Kabudi kuanza kuropoka yale. Wakina Kikwete wanachekea chooni kuona mr mjuaji anavyohangaika na hii nchi.
 
Nikifiria maisha wanayoishi wa Zimbabwe Sina cha kusema...
 
Hicho kibabu Kabudi naona kinazeeka vibaya mno, kinadhani mikwara yake ya hovyo itaisaidia Taifa wakati kanyewe kanakula posho zake
 
Utu?!

Kutesa, Kuteka, Kubambikia kesi, kupora wapinzani ushindi wao, hayo hayahusishi utu?

Au huyo Prof. hajui maana ya utu.

Anyway bado hajajibu swali, Euro 27m iko wapi?
Kabudi ni mzee mpumbavu haijapata kutokea ulimwenguni kote, ngoja waanze nae apigwe vikwazo mpaka achanganyikiwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…