Prof Kabudi: Kati ya pesa na heshima ya nchi yetu, tutasimamia heshima. Tuko tayari kuwasikiliza na kujadiliana kwa heshima

Prof Kabudi: Kati ya pesa na heshima ya nchi yetu, tutasimamia heshima. Tuko tayari kuwasikiliza na kujadiliana kwa heshima

Yeye ni mtanzania, yeye ni mwanaccm, yeye ni muwakilishi wa wananchi kupitia ccm, yeye ni waziri na anasimama kama serikali kutoa msimamo wa nchi

Kama hawawezi kutuheshimu kama tunavyowaheshimu watajibiwa tuu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji106]
Yale yale ya Zimbabwe kujitutumua na kujibizana na mabeberu leo hii wanaoumia ni wananchi wa hali ya chini kwakuwa viongozi wao wanalipana mishahara.

Huyu ni waziri anayedili zaidi na diplomasia kwahiyo tulitegemea kauli za kidiplomasia zaidi kuliko kujibu kwa mihemko madhara yake ni makubwa.
 
Yeye ni mtanzania, yeye ni mwanaccm, yeye ni muwakilishi wa wananchi kupitia ccm, yeye ni waziri na anasimama kama serikali kutoa msimamo wa nchi

Kama hawawezi kutuheshimu kama tunavyowaheshimu watajibiwa tuu😂😂😂👍
Anzeni kwa kuwaheshimu na kujali utu wa wananchi wenu bila kujali itaikadi zao!
Lakini mnaua,mnabambikizia kesi,mnateka na kupiga risasi wapinzani halafu mnasema utu?Shame!
 
Hizo Euro zimetjmika Kama zilivyokusudiwa...wewe unadhani ziko wapi?
Mzee mimi nadhani serikali haina haja yakutoa mipasho yote hii. Kikubwa hizo bilioni 75 za msaada zirudishwe tuepukane na kelele za mabeberu.

Sidhani kama kuna haja yakuendeleza majibizano.
 
Prof Kabudi ambaye ni waziri wa mambo ya nje amesema Tanzania haiwezi kuyumbishwa na vitisho vya kunyimwa misaada.

Kabudi amesisitiza kuwa Tanzania ni nchi huru inayoheshimu utu wa mtu na kamwe haitayumbishwa na nchi yoyote kwa vitisho vya kukatiwa misaada.

Kuhusu uchaguzi Prof Kabudi amesema ulikuwa huru na wa haki na dunia nzima imeshangaa maana hatukutumia posta kama wale wengine lakini uchaguzi wetu umefanyika kwa amani kabisa.

Source ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
=========

Prof. Kabudi: Nayasema haya kwa sababu kizazi cha sasa wanadhani hii nchi ndogo, sisi ndio nchi pekee hatujawahi kushindwa vita, hakuna mahali majeshi yetu yalipokwenda yakashindwa vita. Si Zimbabwe, Msumbiji, Comoro, Seychelles, si Uganda na hivi karibuni sio DRC Congo.

Nawahamasisha pia na vyombo vyetu vya habari tujue nini cha kuiambia dunia na watanzania, uchaguzi huu katika bara la Afrika umekuwa tulivu, wa amani.

There is nobody in the world has ever conducted a perfect election, give me one country! There is no country in the world which has conducted a perfect election. Perfect election is only conducted in heaven.

Mataifa yote yanafanya uchaguzi ambao ni huru, haki na wawazi na sisi wa utulivu na amani. Lazima tuiambie dunia hivyo na Taifa hili, nimesema na narudia, halijawahi kupigishwa magoti.

Na si jambo la kukumbusha kila wakati, sipendi, haina maana tunataka kufanya hivyo. Tulivunja uhusiano wa kibalozi na Uingereza mwaka 65 mpaka 72 na Mwalimu hakuvunja tu balozi na Uingereza, aliwarudishia msaada wao wote wa paundi milioni 5 na wakati ule zilikuwa nyingi, aliwarudishia.

Sisi leo watu wakisema vikwazo tu, tunaanza tetemeka nini? Hivi mngekuwa wakati wa Mwalimu! Hivi Tanzania ya 65 ni Tanzania ya leo? Lakini aliona kati ya heshima ya Tanzania na kudhalilishwa, aliwaambia waingireza, tumeshindwa kuelewana katika haya, basi. Ingawa tulibaki kuwa wanachama wa commonwealth.

Wajerumani mwaka 64 walipoanza kumpa masharti mwalimu baada ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Ujerumani mashariki iko Zanzibar, Ujerumani Maghiribi iko Tanzania bara, tukawaambia hapana, hamuwezi kuanza kunipa masharti. Suala la kufunga ubalozi wa Ujerumani Mashariki Zanzibar, si la kuamua mimi, tupeni muda.

Walipomletea kejeli alilihutubia Taifa, aliwafukuza wataalam wote wa kijerumani na aliwarudishia hela yao dochmark milioni 35, sisi leo watu wachache tu wakikaa kuzungumza, ooh tutafanya hivi! tayari watu kwenye mitandao.

Kati ya pesa na heshima ya nchi yetu, tutasimamia heshima ya nchi yetu. Kati ya misaada na utu wetu, tutasimamia utu wetu. Hatutakubali kutoheshimiwa na utu wetu kudharauliwa kwa sababu ya misaada na pesa lakini tutashirikiana na mataifa yote duniani ambayo, moja yatatuheshimu sisi ni Taifa huru na yanatuheshimu sisi ni binadamu tulio sawa na wanadamu wengine wote na tuko tayari kuwasikiliza na kujadiliana kwa heshima yale ambayo wanadhani yamepungua kwetu na yale ambayo tunadhani yamepungua kwao, tuko tayari. We are ready for constructive engagement with those that respect we are sovereign state but who also respect that we are equal and as humans we have our dignity on those matters of principal, we will not compromise.

However we are ready to work with all nations in the world who share our values, sovereignity, equality of nation, human dignity and respect of all human kind and we will never, never allow anyone to use aid or assistance to undermine our sovereignity, NEVER.

That did not happen during the time of Mwalimu, it will never happen now and this is why I distributed this booklet to all staff from mwalimu Nyerere.
Ili uheshimiwe unatakiwa utangulie kuheshimu wengine
Mbona ninyi hamuwaheshimu wengine?
Hivi kuwaita wazungu mabeberu hii ni heshima?
Kuwaambia watanzani maeneo ambayo hamkupeleka maenendeo kuwa hamkupata maendeleo kwakuwa mliuchagua upinzani,hii ni heshima?

NINYI NDIYO MMEKOSA ADABU NA HESHIMA.
Watu wanawapa pesa zao bure ziwasaidie halafu mnawaita mabeberu hii ni sawa?
Ninyi mkiitwa manyani au masokwe mtafurahi?

Mmekosa adabu ndani ya nchi yenu na nje pia.
Oooh! Tutatetea heshima yetu kwanza lakini tutazungumza nao kwa heshima wakitaka.
Uzungumze nao nini wakati unaona wamekuvunjia heshima!!
Mnaweweseka tu

Sasa nasmini maneno ya Lissu kuwa wanaoteuliwa wanaokotwa majalalani.
HUYU WAZIRI ANATOSHA KWELI KWENYE HII WIZARA?

WAZUNGU NJOONI MTUNYOOSHE JAPO TUTATESEKA WOTE,POTELEA MBALI.
 
Hata kwenye korona walisema hawafungi mipaka matokeo yake cc ndio tukafungiwa yaani mipaka yetu ipo wazi unaruhusiwa kutoka lkn huwezi toka kwa sababu kule uwendako mipaka imefungwa yaani upo upo tu,

Sent from my itel S11 using JamiiForums mobile app
 
Mzee mimi nadhani serikali haina haja yakutoa mipasho yote hii. Kikubwa hizo bilioni 75 za msaada zirudishwe tuepukane na kelele za mabeberu.

Sidhani kama kuna haja yakuendeleza majibizano.
Zirudishwe wapi?
 
Mzee mimi nadhani serikali haina haja yakutoa mipasho yote hii. Kikubwa hizo bilioni 75 za msaada zirudishwe tuepukane na kelele za mabeberu.

Sidhani kama kuna haja yakuendeleza majibizano.
Mbona nawe umehusika katika kuzitumia Sasa zitarudishwaje wakati zimetumika
 
Yale yale ya Zimbabwe kujitutumua na kujibizana na mabeberu leo hii wanaoumia ni wananchi wa hali ya chini kwakuwa viongozi wao wanalipana mishahara.

Huyu ni waziri anayedili zaidi na diplomasia kwahiyo tulitegemea kauli za kidiplomasia zaidi kuliko kujibu kwa mihemko madhara yake ni makubwa.

Zimbabwe sio Tanzania wala Mugabe sio Magufuli

Huyu ni waziri anayedili zaidi na diplomasia na ametoa maelezo sahihi na ya kidiplomasia
Wewe ulitaka atoe maelezo gani? Hebu tuwekee hapa ulichotaka Kabudi aongee😁😁😁

Ni wakati sasa wa hao vibaraka na mabwana zao kuacha mihemko kwa taifa lililo huru

Mungu ibariki Tanzania
 
Faza Kabudi akili zake Anaijua mwenyewe na kumbuka alishawai mwambia Magufuli anamshukuru kwa kumtoa jalalani
Pia aliwahi kumuadress " mheshimiwa mungu".
Takataka ambayo haifai hata kutengenezea mkaa,mbolea wala chakula ya funza.
 
Hawajatisha wameuliza tu kale ka fedha ka korona mmekapeleka wapi.

Wajibu tu sio unaanza kuwafokea.
Soma hapa
IMG_20201120_153330.jpg
 
Back
Top Bottom