Juzi Kabudi aliiongoza ujumbe uliofuata dawa nchini Madagascar kwa ndege yetu. Inasemekana zimeletwa maboksi 13 zikiwemo dawa za aina mbili. Hapo hapo tukaonyeshwa akijaribisha kwa kunywa na pale tukaona chupa mbili. Jana ameongea na vyombo vya habari na pia tukaonyeshwa walioshiriki akiwemo Mganga Mkuu wa Serikali.
Swali langu: Ni hii sintofahamu juu ya ushiriki wake 190% katika zoezi. Sikuwasikia mawaziri wa wizara hii ya afya. Nikawa najiuliza kuwa dawa ikifuatwa nje ya nchi, Wizara ya Mambo ya Nje ndiyo inahusika na haiko chini ya Wizara ya Afya.
Pengine kwa hili Kabudi anisamehe, sijatambua vizuri nafasi yake kwenye masuala ya afya. Na kubwa kumbe haijawa dawa kama tulivyosikia kuwa ndege imefuata dawa, kumbe ni sampuli ya kufanyia utafiti.
Nimeshindwa kuelewa, nielekezeni huyu Kabudi anakotupeleka. Hii ni mara yake ya pili kuona akituaminisha kitu baada ya sakata la makinikia.
Sent using
Jamii Forums mobile app