Prof. Kabudi: Kwa sasa Wananchi hawatapewa dawa za kukabiliana na Corona kutoka Madagascar, inafanyiwa utafiti kwanza

Prof Kabudi aseme ukweli kuwa wamepigwa mikwara na wazungu, hii dawa ilikuwa kwaajili ya matumizi ya watanzania na walichukua cotton za kutosha.

Watu wanashindwa kucheza beat moja na wazungu... Hii dunia ina wenyewe hii
 
Mbona yeye alikunywa halafu utafiti, nasi atupe tunywe huku wanaendelea na utafiti kwani tukifa naye atakufa

Naamini maneno waliyopokea Jana ndiyo yamebadilisha upepo
 
Juzi Kabudi aliiongoza ujumbe uliofuata dawa nchini Madagascar kwa ndege yetu. Inasemekana zimeletwa maboksi 13 zikiwemo dawa za aina mbili. Hapo hapo tukaonyeshwa akijaribisha kwa kunywa na pale tukaona chupa mbili. Jana ameongea na vyombo vya habari na pia tukaonyeshwa walioshiriki akiwemo Mganga Mkuu wa Serikali.

Swali langu: Ni hii sintofahamu juu ya ushiriki wake 190% katika zoezi. Sikuwasikia mawaziri wa wizara hii ya afya. Nikawa najiuliza kuwa dawa ikifuatwa nje ya nchi, Wizara ya Mambo ya Nje ndiyo inahusika na haiko chini ya Wizara ya Afya.

Pengine kwa hili Kabudi anisamehe, sijatambua vizuri nafasi yake kwenye masuala ya afya. Na kubwa kumbe haijawa dawa kama tulivyosikia kuwa ndege imefuata dawa, kumbe ni sampuli ya kufanyia utafiti.

Nimeshindwa kuelewa, nielekezeni huyu Kabudi anakotupeleka. Hii ni mara yake ya pili kuona akituaminisha kitu baada ya sakata la makinikia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani ulitarajia waende wizara ya afya kwani umesikia mzigo ni wa wizara ya afya ule?

Mzigo unaenda Chato ule jombaa!!

Yaani Jiwe atoe ndege yake hadi Madagascar kufuata kikombe halafu awape nyie kabla hajahakikisha umeshatosheleza Chato?

Kule kwa wajomba zangu wangekuambia ".. kalaghabao...!"
 
Juzi Kabudi aliiongoza ujumbe uliofuata dawa nchini Madagascar kwa ndege yetu. Inasemekana zimeletwa maboksi 13 zikiwemo dawa za aina mbili. Hapo hapo tukaonyeshwa akijaribisha kwa kunywa na pale tukaona chupa mbili. Jana ameongea na vyombo vya habari na pia tukaonyeshwa walioshiriki akiwemo Mganga Mkuu wa Serikali.

Swali langu: Ni hii sintofahamu juu ya ushiriki wake 190% katika zoezi. Sikuwasikia mawaziri wa wizara hii ya afya. Nikawa najiuliza kuwa dawa ikifuatwa nje ya nchi, Wizara ya Mambo ya Nje ndiyo inahusika na haiko chini ya Wizara ya Afya.

Pengine kwa hili Kabudi anisamehe, sijatambua vizuri nafasi yake kwenye masuala ya afya. Na kubwa kumbe haijawa dawa kama tulivyosikia kuwa ndege imefuata dawa, kumbe ni sampuli ya kufanyia utafiti.

Nimeshindwa kuelewa, nielekezeni huyu Kabudi anakotupeleka. Hii ni mara yake ya pili kuona akituaminisha kitu baada ya sakata la makinikia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sampuli tu unatuma ndege, mbona ni matumizi mabaya ya pesa za watanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabudi mwenyewe alikuwa hana uhakika wa kupata ya kunywa akanywa kabisa...

Sisi ni Taifa la masihara ..kila kona
Halafu Kuna vijing'ombe vinataka Bujibuji niwe serious.
Niwe serious kwa manufaa ya Nani wakati Kuhani Mkuu mwenyewe ni katuni kuliko Mimi?
Mapapai yanapimwa korona ili upate Nini?
Tunaficha takwimu ili tufaidike na Nini?
Tunazikwa watu saa Saba usiku ili tuwape mboga wachawi?
 
Back
Top Bottom