Prof. Kabudi: Kwa sasa Wananchi hawatapewa dawa za kukabiliana na Corona kutoka Madagascar, inafanyiwa utafiti kwanza

Prof. Kabudi: Kwa sasa Wananchi hawatapewa dawa za kukabiliana na Corona kutoka Madagascar, inafanyiwa utafiti kwanza

Uchoyo ni jadi yetu, wametumia jina lako kujipatia tiba kwa ajili ya familia zao.
 
IMG_20200509_162025.jpg
 
Nijuavyo mimi msemaji wa maswala ya tiba na dawa kisekta ni waziri wa afya au Naibu wake wakisaidiwa na wataalamu wa wizara...
The Guys are obviously desperate and stressed.He took the whole bottle of it?Imagine if every one is gonna drink like he did,we may need about 50 million bottles.

What's the cost of @,effectiveness of the Herb, side effects and safety of usage to consumers.
What if it's not effective? Who will be blamed, may be Ummy?

I suspect that our country isn't in right direction.
 
Nijuavyo mimi msemaji wa maswala ya tiba na dawa kisekta ni waziri wa afya au Naibu wake wakisaidiwa na wataalamu wa wizara.

Lakini kwa hii dawa mpya ya Covid 19 kutoka Madagascar nimeshangaa kuona msemaji wake mkuu ni Prof Kabudi ambaye ni waziri wa mambo ya nje, hapo ndio ninapoomba maana Ummy Mwalimu yupo na anadunda kama kawa.

Hii imekaaje wadau?

Maendeleo hayana vyama!
Mbona hata kina jafo wanazungumzia nyungu, sasa hii nyungu ina upekee gani au sababu imepanda ndege?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna bwege mmoja sasa ameanza kutembea kifua mbele anashangilia zimeletwa dawa za code 19 sorry i meant covid 19.

Ameacha na kuvaa bakoroa...i mean barakoa.ndo nmemwambia hapa aache ujinga. Nmemuuliza maswali haya.

1. Akiumwa corona wangap watasikitika? Amekosa jibu

2. Akifa taifa litaingia hasara gani? Hamna. Sana sana hata ndugu zake watashukuru wamepungukiwa na mtu wa kuwapiga mizinga.

Anataka eti naye apewe dawa.toka amekua mpaka sasa amewahi kuliingizia nini taifa?zàidi ya kulitia hasara tu hata kazi hana...hakatwi kodi kubwa ya wafanyakazi. Hana kitu kikubwa cha maana anachonunua.mtu anashindia mihogo tu na maji huyu anachangia nini kwenye pato la Taifa?

Halafu kama bwege anashangilia eti dawa ya Corona imeletwa ile dawa nashauri anywe Mh.Rais na ndugu zake kama itabaki awape na watu wake wa karibu ambao wanamsaidia kulijenga Taifa.

Ndo maana Prof Kabudi aliamua anywe yake kabisa huko huko ili asije kusumbua tena huku kutaka nyingine na hivyo kupunguza bajeti.

Mwacheni mh rais anywe hiyo dawa ili awe na kinga zaidi.tena anywe tu kama juice natumaini haina ladha mbaya.mh rais ni mtu namba moja na muhimu hapa tanzania.

Sisi watanzania tuvaeni barakoa,tufungeni vitenge na vipande vya nguo usoni kuzuia midomo na pua zetu kuonekana.

Watanzania tuacheni kuomba omba omba.tumwache rais anywe atulie mazingira salama.HUO MZIGO WA DAWA ULIOLETWA UKWELI NI KWAMBA HAMNA KITU KWENDA KWA WATU WASIO NA FAIDA. sisi tupige kazi jamani.huo ndo ushauri wangu.
 
Kabudi ni mtu wa propaganda na abrakadabraa

na ndio maana wamemvalisha hiyo dawa ya Rajoelina wa Madagascar
 
Hapa kwetu ndio kuna mambo ya ajabu huwezi kuyaona katika ulimwengu wote labda ulimwengu wa Roho.

Dawa anayotuambia kuwa imeletwa karibu tani nzima kama SAMPLE ili ipelekwe maabara kwa uchunguzi ameamua kwa hiari yake bila kulazimishwa na mtu kuinywa chupa nzima.
Huyu sio mwingine bali ni Waziri wa mambo ya Nje, Msomi wa kiwango cha Profesa wa sheria na mshauri wa karibu wa Rais...
Huyu alishakuwa nao, kanusurika ivyo anahisi utamrudia tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nijuavyo mimi msemaji wa maswala ya tiba na dawa kisekta ni waziri wa afya au Naibu wake wakisaidiwa na wataalamu wa wizara...
Bwashee kwa kawaida baadhi ya dawa za mitishamba zinakuwa na masharti magumu unayo pewa na mganga. Anae kwenda kwa mganga ndie anae pewa masharti hayo, kwa hiyo ni vigumu sana kusikia mtu amemfundisha mwingine masharti aliyo pewa na mganga. Ndio naamini kwamba Kabudi ndie waziri wa mambo ya nje ya nchi, lakini linapokuja suala zima la kuhusu tiba ni lazima wataalamu washirikishwe kwa kuwa ndio wenye taaluma na dhamana juu ya afya za binadamu.

Je, wataalamu wetu kupitia wizara husika waliambatana na waziri kwenda kuleta dawa? Na kama walishirikishwa, je waliidhinisha kwa mujibu wa taaluma yao kuwa ni dawa iliyo tayari kutumika? Ama ni dawa inayo hitaji utafiti zaidi kwa matumizi ya binadamu?
 
Back
Top Bottom