Prof Kabudi: Mwandishi mmoja wa kigeni aliandika kuhusu kifo cha Sokoine kwamba Nyerere alihusika au alifaidika na kifo hicho

Horace Kolimba nae aliamua kumwaga ugali na mboga pale aliposema CCM imepoteza dira na mwelekeo.

Mwaka 1994 Kolimba alifanya mahojiano maalum na gazeri la Rai na akaeleza kwa kirefu namna ambavyo CCM imepoteza Dira.

Ile ilikuwa ni kama vile wajitafutia matatizo na marehemu Kolimba akaitwa Chamwino ajieleze.

Kikao kiliokuwa ni kizito kikiongozwa na hayati Mwalimu na marehemu Kolimba akazidiwa masuali mazito likiwemo suali kwamba mbona una "too much ambitions"?

Kolimba alikuwa kwenye lile kundi la watanzania wasomi 14 wa kwanza walokwenda kusoma sheria UDSM na alisomea hivyo kijana wa Minaki alifahamu kutema cheche vifungu kwa vifungu hivyo alikuwa ni tishio.

Hiyo timu ilikuwa na watu kama mzee Joseph Warioba, mzee Job Lusinde, Mohamed Kissoky, mzee John Malecela, mzee Alfred Tandau na wengine.

Kolimba alikuwa na vision na alipanua mawazo alipofanya kazi na marehemu Sokoine na Salim Ahmed Salim ndo maana aliona CCM imepoteza Dira, kwani viongozi hao walikuwa na maono makali juu ya nchi hii, ila CCM ilikuwa ndo tatizo.
 
Kabudi anajua sana kupuyanga guku akitoa macho kama amebanwa na mlango.

Busara yake i wapi hapa?
 
Mbona hayo ni kawaida tu.
Kiongozi wa juu akifariki hasa ghaflaghafla anatafutwa tu mtu wa kumsingizia.
Mfano JPM alipofariki wengine walidai JK na Kinana walihusika wakati hata kunufaika hawajanufaika kwa chochote.
Hawajanufaika?

Kwenye kuhusika sijui, kwenye kunufaika mbona iko wazi?
 
Nilidhani Profesa amekuja na Nyaraka za uthibitisho wa nguvu ili kupinga madai hayo yaliyoibuliwa na huyo Mzungu?!!!
 
Wenyewe wanasema uzembe ni trafic...wakati wa msafara wake unakuja gari zilisimamishwa gafla
Huyo dube ni kama aliingia mchecheto

Ova
 
Huwa najiuliza uongozi wa Kanisa Katoliki linatumia akili zipi kutaka Nyerere apewe hadhi ya utakatifu. Nikiangalia umbumbumbu wa raia wengi naona kabisa umetokana na sera mbovu za ujamaa?
Usimsingizie Nyerere kwa umbumbumbu wako.
Nyerere ndiye alikuambia ushinde tangu asubuhi unajadili Simba na yanga? Nyerere ndiye aliyekufanya ubaki unajadili maisha ya wasanii wanafanya mapenzi na nani?

Failure zako walaumu wazazi wako.

Nyerere alitoa elimu bure hadi chuo kikuu ili utoe ujinga, Nyerere alimlazimisha babako akupeke shule kwa kumtishia kumfunga jela ikiwa hakupeleki shule.

Nyerere ameondoka madarakani miaka arobaini iliyopita halafu umekallsha makalio unamlaumu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…