Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Horace Kolimba nae aliamua kumwaga ugali na mboga pale aliposema CCM imepoteza dira na mwelekeo.
Mwaka 1994 Kolimba alifanya mahojiano maalum na gazeri la Rai na akaeleza kwa kirefu namna ambavyo CCM imepoteza Dira.
Ile ilikuwa ni kama vile wajitafutia matatizo na marehemu Kolimba akaitwa Chamwino ajieleze.
Kikao kiliokuwa ni kizito kikiongozwa na hayati Mwalimu na marehemu Kolimba akazidiwa masuali mazito likiwemo suali kwamba mbona una "too much ambitions"?
Kolimba alikuwa kwenye lile kundi la watanzania wasomi 14 wa kwanza walokwenda kusoma sheria UDSM na alisomea hivyo kijana wa Minaki alifahamu kutema cheche vifungu kwa vifungu hivyo alikuwa ni tishio.
Hiyo timu ilikuwa na watu kama mzee Joseph Warioba, mzee Job Lusinde, Mohamed Kissoky, mzee John Malecela, mzee Alfred Tandau na wengine.
Kolimba alikuwa na vision na alipanua mawazo alipofanya kazi na marehemu Sokoine na Salim Ahmed Salim ndo maana aliona CCM imepoteza Dira, kwani viongozi hao walikuwa na maono makali juu ya nchi hii, ila CCM ilikuwa ndo tatizo.