Prof Kabudi: Mwandishi mmoja wa kigeni aliandika kuhusu kifo cha Sokoine kwamba Nyerere alihusika au alifaidika na kifo hicho

Excellent
Lakini kwenye hilo la Kambona na Kawawa; kuna 'dynamics' za ziada kuliko hiyo ya usomi na kutokuwa na kisomo.
Kumbuka 'balancing' iliyo hitajika wakati huo katika kujenga taifa lenye umoja. Kawawa alikuwa na mchango wake huko.

Kambona, sidhani kwamba ni tofauti za kisomo ndizo zilizo mtenganisha na Mwalimu. Kama ni swala la mfumo wa kiuchumi, 'ujamaa versus ubepari' la wakati huo; tofauti hiyo Kambona hakuweza kui-'articulate' vyema ili watu wamwelewe alipo kuwa amesimamia, hata baada ya kukimbia nchi, na baadae kurudi.
Kwenye swala kubwa kama hilo haukuwa ni uamzi wa mtu binafsi. Hilo lilikuwa swala la chama na liliamuliwa katika vikao vya chama baada ya majadiliano mengi. Sasa kama Kambona aliona hakukubaliana na maamuzi wa mwelekeo wa chama, bila shaka maoni yake yangekuwepo huko kwenye hivyo vikao kwenye ngazi mbalimbali. Simlaumu kwa kukimbia nchi kwake wakati huo, lakini ningetegemea kusikia/kusoma maoni juu ya msimamo wake hadi kuona bora akimbie nchi.
Sasa, kama kawaida yetu siku hizi; kuna mijadala mingi tu humu inaibuka humu na kwingineko na habari nyingi tu za kutungwa kuhusu kutofautiana huko kati yake na Mwalimu Nyerere.

Ngoja nikupeleke kwenye eneo jingine ambalo unaweza kuona tofauti kubwa sana, kati ya leo, na wakati ule.
Baraza la Mawaziri: la leo na la wakati ule. Angalia hata kwenye utendaji wa mawaziri wenyewe.

Bunge: leo hii, Bunge la watu ambao ungetegemea ni wa kisomo cha hali ya juu zaidi na kuwa na uelewa wa maswala mbalimbali ya kidunia; linganisha na Bunge la nyakati zile; bunge la watu ambao kisomo chao wengi kingekuwa ni cha wasiwasi mkubwa.. Angalia maamuzi ya vyombo hivyo viwili vyenye maamuzi muhimu ya nchi.

Hata Mahakama siwezi kutazama hii ya leo na kulinganisha na yale ya wakati ule.
 
Sure Kambona na Nyerere ilikuwa itikadi - ubepari Vs ujamaa
Kambona alikuwa critic kawawa alimsupport Nyerere.

Kuhusu parliament yetu, comparison; yote hii ni matokeo ya Siasa ya Ujamaa na education system; base ni dhaifu sana
 
Si mgeni lakini sijawahi kuona utapeli wa Kabudi.Infact katika mawaziri ambao nimeshawahi kuwapenda,Kabudi ni mmoja wapo.Ni mwamba aliye na misimo isiyotumba na mizuri.Tanzania tunahitaji viongozi aina ya Kabudi.
Unakumbuka kuwa aliwahi kumuita Jiwe kuwa ni Mungu?
 
Kama kweli ilikuwa hivyo usemavyo,Chukua Chako Mapema walimchukua mapema.
 
Izo mambo ungezifanya kipindi hiki tungekuwa tunakutafuta umepotelea wapi?
 
Hans Pope ni hatari na nusu, kwenye ile kesi ya uhaini nilikuwa naisoma kama movie hivi.
 
nchi alipokuwa ameifikisha Nyerere haikuhitaji mtu mwenye akili kama Sokoine alihitajika mtu Royal kwa mwalimu ndiyo maama akampiga chini Salim baada ya Sokoine kufa na kum pendekeza Mwinyi.
Baada ya kifo cha Sokoine Salim alipewa kuwa PM, kwenye urais ikasemekana bado mdogo ngoja akue kue kwanza.
 
Mbona hayo ni kawaida tu.
Kiongozi wa juu akifariki hasa ghaflaghafla anatafutwa tu mtu wa kumsingizia.
Mfano JPM alipofariki wengine walidai JK na Kinana walihusika wakati hata kunufaika hawajanufaika kwa chochote.
Wengine tumeisingizia corona
 
TUFUNGUE KESI DHIDI YA MSUYA NA WENZAKE SERIKALI ILI TUPATE UKWELI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…