Prof Kabudi: Mwandishi mmoja wa kigeni aliandika kuhusu kifo cha Sokoine kwamba Nyerere alihusika au alifaidika na kifo hicho

Prof Kabudi: Mwandishi mmoja wa kigeni aliandika kuhusu kifo cha Sokoine kwamba Nyerere alihusika au alifaidika na kifo hicho

Excellent
Lakini kwenye hilo la Kambona na Kawawa; kuna 'dynamics' za ziada kuliko hiyo ya usomi na kutokuwa na kisomo.
Kumbuka 'balancing' iliyo hitajika wakati huo katika kujenga taifa lenye umoja. Kawawa alikuwa na mchango wake huko.

Kambona, sidhani kwamba ni tofauti za kisomo ndizo zilizo mtenganisha na Mwalimu. Kama ni swala la mfumo wa kiuchumi, 'ujamaa versus ubepari' la wakati huo; tofauti hiyo Kambona hakuweza kui-'articulate' vyema ili watu wamwelewe alipo kuwa amesimamia, hata baada ya kukimbia nchi, na baadae kurudi.
Kwenye swala kubwa kama hilo haukuwa ni uamzi wa mtu binafsi. Hilo lilikuwa swala la chama na liliamuliwa katika vikao vya chama baada ya majadiliano mengi. Sasa kama Kambona aliona hakukubaliana na maamuzi wa mwelekeo wa chama, bila shaka maoni yake yangekuwepo huko kwenye hivyo vikao kwenye ngazi mbalimbali. Simlaumu kwa kukimbia nchi kwake wakati huo, lakini ningetegemea kusikia/kusoma maoni juu ya msimamo wake hadi kuona bora akimbie nchi.
Sasa, kama kawaida yetu siku hizi; kuna mijadala mingi tu humu inaibuka humu na kwingineko na habari nyingi tu za kutungwa kuhusu kutofautiana huko kati yake na Mwalimu Nyerere.

Ngoja nikupeleke kwenye eneo jingine ambalo unaweza kuona tofauti kubwa sana, kati ya leo, na wakati ule.
Baraza la Mawaziri: la leo na la wakati ule. Angalia hata kwenye utendaji wa mawaziri wenyewe.

Bunge: leo hii, Bunge la watu ambao ungetegemea ni wa kisomo cha hali ya juu zaidi na kuwa na uelewa wa maswala mbalimbali ya kidunia; linganisha na Bunge la nyakati zile; bunge la watu ambao kisomo chao wengi kingekuwa ni cha wasiwasi mkubwa.. Angalia maamuzi ya vyombo hivyo viwili vyenye maamuzi muhimu ya nchi.

Hata Mahakama siwezi kutazama hii ya leo na kulinganisha na yale ya wakati ule.
 
Sure Kambona na Nyerere ilikuwa itikadi - ubepari Vs ujamaa
Kambona alikuwa critic kawawa alimsupport Nyerere.

Kuhusu parliament yetu, comparison; yote hii ni matokeo ya Siasa ya Ujamaa na education system; base ni dhaifu sana
 
Kesi ilipoanza baada ya kuhairishwa mara tu akakubali makosa yote. Hiki kipindi ambacho kesi iliahirishwa kitu gani kilitokea?

Pili Waziri Mkuu anagongwa na gari anauawa kesi ilisikilizwa jumla ya masaa mawili. Yaani siku ya kwanza si zaidi ya saa moja siku ya pili anakubali na si zaidi ya saa moja. Jumla masaa mawili.

Hukumu inatotelewa
Kama kweli ilikuwa hivyo usemavyo,Chukua Chako Mapema walimchukua mapema.
 
Alafu unajua mimi huwa najiuliza nikiwa tu darasa la pili nilianza kukataa kuimbishwa zidumu FIKIRA za mwenyekiti wa CCM, nikamwuliza mwalimu wangu kwa nini tunaambiwa zidumu fikira za mwenyekiti wa CCM ili hali hatujui anafikiria nini? Ajabu nilishia kulambwa bakora za kutosha na kutumwa nikaite mzazi eti nina tabia mbaya. Mzazi naye bila kunisikiliza akaungana na mwalimu na kunitandika bakora za kutosha kwa hoja dhaifu sana kwamba nina akili darasani lakini ninataka kuanza kuwa na tabia.
Nikiwa darasa la sita nako nikakumbana na kadhia ya kufukuzwa shule kwa sababu nilikataa kujiandikisha kupiga kura, sababu ya kukataa ilikuwa ni dhahiri kwa kipindi hicho sikuwa nimetiza miaka 18, japo uchaguzi wenyewe ulikuwa ni wachama kimoja lakini wabunge walikuwa wanagombea wawili isipokuwa Rais ndo alikuwa anasimama na kivuli.

Nakumbuka mwalimu wangu mkuu alikuwa swaiba sana wa mgombea mmoja wapo aliyekuwa akifahamika kwa jina la Charles Magoti, hivo ili kumwongezea kura alichukuwa vijana wote ambao walionekana warefu na wenye uwezo wa kutambua na kufuata maelekezo wajiandikishe kupiga kura.

Mimi nilihoji tu kama katiba ya CCM inatakamka kwamba mtu ambaye anaruhusiwa kupiga kura ni yule tu aliyetimiza umri wa miaka 18 iweje sisi tulazimishwe kupiga kura? Nikafukuzwa shule kwa muda wa miezi 3. Hizi figusu zilianza miaka mingi sana.

Hoja yangu ni nini? Hoja yangu ni kwamba kitabu cha SOKOINE kilipaswa kuandikwa na watu wasiofungana na upande wowote na si akina KADARI SINGO ( PE)
Izo mambo ungezifanya kipindi hiki tungekuwa tunakutafuta umepotelea wapi?
 
Kwani hiki kizazi cha sasa (cha hovyo kabisa) kina jipya la kutishia nyau?

1.Hujui kwamba pale UDSM zamani kulikuwa na Vijana wanaojua kuhoji kuliko leo? Vipanga wa leo pale UDSM na Vyuo Vikuu wote si ni watu wa kukariri madesa tu ili wafaulu kwa GPA kubwa ila uwezo wa kujenga hoja ni 0. Prof.Issa Shivji anajua kuhusu hili.

2.Vijana walioko kwenye Jeshi lenu leo wanaweza kufanya yale majaribio waliyofanya wenzao miaka ya 1964 na 1982? Yaani hao akina Clinton Damas 'Nyundo' wanao huo uthubutu? Kama siyo kwamba wanachojua ni kubaka,kulawiti na kupoteza tu.

Yule Zachariah Hans Pope na wenzake walikuwa watu na nusu wale. Hata alipoamua kujikita kwenye soka pale Simba SC shughuli yale ilionekana, na hadi sasa Simba wanahangaika kuziba pengo.
Hans Pope ni hatari na nusu, kwenye ile kesi ya uhaini nilikuwa naisoma kama movie hivi.
 
nchi alipokuwa ameifikisha Nyerere haikuhitaji mtu mwenye akili kama Sokoine alihitajika mtu Royal kwa mwalimu ndiyo maama akampiga chini Salim baada ya Sokoine kufa na kum pendekeza Mwinyi.
Baada ya kifo cha Sokoine Salim alipewa kuwa PM, kwenye urais ikasemekana bado mdogo ngoja akue kue kwanza.
 
Mbona hayo ni kawaida tu.
Kiongozi wa juu akifariki hasa ghaflaghafla anatafutwa tu mtu wa kumsingizia.
Mfano JPM alipofariki wengine walidai JK na Kinana walihusika wakati hata kunufaika hawajanufaika kwa chochote.
Wengine tumeisingizia corona
 
100% CCM walimuua Sokoine.
Dumisani Dube alikuwa anaenda wapi na yeye alikuwa anaisha Dar kama mkimbizi?

Tangu lini Waziri Mkuu agongwe na Gari na body guards na ulinzi ulivyo?

Kawawa kwa nini aliiwahi ndege ya Sokoine akaenda nayo Liwale? Nia yake ilikuwa akamilishe njama zake yeye na M—ya.

Kesi ilipoanza:
Siku ya kwanza Dumisani Dube alikataa kuwa yeye hakumuua yaani not guilty
Kesi ikaailishwa

Baada ya Kesi kuanza mara ya pili Dumisani Dube alikubali makosa yote na kuhukumiwa jela miaka mitano.

Badala ya kutumikia kifungo unamwona London anaishi maisha mazuri!!!!!

Jifikirishe, hiyo ndiyo CCM.

Muulizeni Cleopa Msuya kabla ya ..,fa, huyu ndiyo kabakia katika master planners
TUFUNGUE KESI DHIDI YA MSUYA NA WENZAKE SERIKALI ILI TUPATE UKWELI
 
Back
Top Bottom