Alafu unajua mimi huwa najiuliza nikiwa tu darasa la pili nilianza kukataa kuimbishwa zidumu FIKIRA za mwenyekiti wa CCM, nikamwuliza mwalimu wangu kwa nini tunaambiwa zidumu fikira za mwenyekiti wa CCM ili hali hatujui anafikiria nini? Ajabu nilishia kulambwa bakora za kutosha na kutumwa nikaite mzazi eti nina tabia mbaya. Mzazi naye bila kunisikiliza akaungana na mwalimu na kunitandika bakora za kutosha kwa hoja dhaifu sana kwamba nina akili darasani lakini ninataka kuanza kuwa na tabia.
Nikiwa darasa la sita nako nikakumbana na kadhia ya kufukuzwa shule kwa sababu nilikataa kujiandikisha kupiga kura, sababu ya kukataa ilikuwa ni dhahiri kwa kipindi hicho sikuwa nimetiza miaka 18, japo uchaguzi wenyewe ulikuwa ni wachama kimoja lakini wabunge walikuwa wanagombea wawili isipokuwa Rais ndo alikuwa anasimama na kivuli.
Nakumbuka mwalimu wangu mkuu alikuwa swaiba sana wa mgombea mmoja wapo aliyekuwa akifahamika kwa jina la Charles Magoti, hivo ili kumwongezea kura alichukuwa vijana wote ambao walionekana warefu na wenye uwezo wa kutambua na kufuata maelekezo wajiandikishe kupiga kura.
Mimi nilihoji tu kama katiba ya CCM inatakamka kwamba mtu ambaye anaruhusiwa kupiga kura ni yule tu aliyetimiza umri wa miaka 18 iweje sisi tulazimishwe kupiga kura? Nikafukuzwa shule kwa muda wa miezi 3. Hizi figusu zilianza miaka mingi sana.
Hoja yangu ni nini? Hoja yangu ni kwamba kitabu cha SOKOINE kilipaswa kuandikwa na watu wasiofungana na upande wowote na si akina KADARI SINGO ( PE)