Prof. Kabudi ndio awe Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba. Apewe nafasi ya kukamilisha alichoanzisha

Prof. Kabudi ndio awe Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba. Apewe nafasi ya kukamilisha alichoanzisha

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Posts
2,789
Reaction score
4,951
Kwa kuwa mchakato wa katiba mpya utaendelezwa panapo Majaliwa yake Mwenyezi Mungu mwaka ujao wa fedha 2023/2024 na tume maalumu itaundwa kufanikisha mchakato huo naona Prof. Kabudi atafaa sana kuwa Mwenyekiti wa bunge maalumu la Katiba.

Ni mwanasheria mzuri na mwenye uwezo mkubwa wa masuala ya katiba, anaifahamu vyema historia ya ukombozi wa nchi kabla na baada ya Uhuru, ni mzalendo wa kweli mwenye kuipenda Tanzania kwa dhati.

Ameshiriki kwa kiwango kikubwa kuandaa Rasimu ya Katiba ya Mzee Warioba hivyo kama mchakato wa katiba mpya utaendelezwa pale kwenye Rasmi ya Mzee Warioba basi Prof.Kabudi ndiye mtu sahihi wa kuendeleza mchakato huo na hata kama mchakato utaanza upya kabisa Prof.Kabudi ni mtu sahihi kwa uwezo na ujuzi wake katika masuala ya sheria na Katiba kutupatia katiba iliyo bora.

Ninaamini Prof. Kabudi ni mtu sahihi kabisa wa kutupatia katiba bora.
 
Bila kumsahau Prof,Lipumba,Oroso na Mruma
20221004_104944.jpg
 
Kumtumia huyo si bora hata akachukuliwa Juma Lokole!!? Kumbe wasomi wengi tuliowaamini huko nyuma zilikuwa njaa tu! Walipopewa chakula tu. Yupo wapi Ayubu Rioba wa kipindi kile? Yupo mlimani. Prof Jicho Kodo wa Tume ya Warioba na huyo akiwa waziri awamu ya tano?

Yupo wapi Bushman wa Tume ya Warioba na wa kipindi cha JPM? Yuko wapi Bashiru? Kidogo ukiniambia Prof. Shivji naweza kukuelewa, kwani hata wiki iliyopita alikuwa TBC, aliwanyoosha sana kina Wasira na Rioba juu ya suala la katiba.

Ila huyo Prof. Majalala hapana, heshima yake aliishusha mno, yaani unakuwa mpambe hadi BOSS ana nuna!
 
Huyu huyu profesa majalala aliyesema katiba hii inajitosheleza, acha utani kiongozi. Mtu pekee wa kuongoza zoezi ni walioba aanzie alipoishia, kwisha.
 
Aaa wapi, huyu alituaminisha nchi italipwa fedha nyingi na Barrick kiasi kwamba kila Mtanzania anaweza kupewa gari la Noah halafu baadaye anakuja kusema kiasi hicho cha fedha hakikuwa kweli. Atatugeuka tena huyu. Akafundishe chuo.
 
Huyo mjinga aliyekunywa kikombe cha babu wa Madagascar hadharani eti ni tiba ya Covid? Hilo zee kazi yake na kutumika tu kama ule mpira wa kufanyia mapenzi.
 
Hakuna bunge la katiba tena. Ni upotevu wa fedha za watanzania tu. Mnakwenfa kule halafu hamuelewani, wengine wanatoka bungeni. Ni ujinga.

Hakuna Katiba utakayofurahisha kila mtu. Wacha this time I've kwa style tofauti.
 
Kabudi hata wafunga majangili wote wanao iba pesa zetu za Tanzania walahi !
Hanaga nsalie Mtumeee
 
Labda kama hiyo katiba ni ya sukuma gang na walio okotwa majalalani hapo sawa.

Kama katiba ya nchi ya watu wenye Akili propesa macho hawezi hata kuwa mjumbe. Arudi majalalani aliko tolewa.
 
Huyu ni muongo, anajikomba sana wala hawezi kuongoza hata kundi la kuku. Kwa aliowafundisha UDSM wanajua alivo wa hovyo.
Uwezo wa Prof.Kabudi kwenye taaluma ya Sheria hautakiwi kubezwa. Ana uwezo wa kutupatia katiba bora kwa uzalendo alionao
 
Back
Top Bottom