KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,789
- 4,951
Kwa kuwa mchakato wa katiba mpya utaendelezwa panapo Majaliwa yake Mwenyezi Mungu mwaka ujao wa fedha 2023/2024 na tume maalumu itaundwa kufanikisha mchakato huo naona Prof. Kabudi atafaa sana kuwa Mwenyekiti wa bunge maalumu la Katiba.
Ni mwanasheria mzuri na mwenye uwezo mkubwa wa masuala ya katiba, anaifahamu vyema historia ya ukombozi wa nchi kabla na baada ya Uhuru, ni mzalendo wa kweli mwenye kuipenda Tanzania kwa dhati.
Ameshiriki kwa kiwango kikubwa kuandaa Rasimu ya Katiba ya Mzee Warioba hivyo kama mchakato wa katiba mpya utaendelezwa pale kwenye Rasmi ya Mzee Warioba basi Prof.Kabudi ndiye mtu sahihi wa kuendeleza mchakato huo na hata kama mchakato utaanza upya kabisa Prof.Kabudi ni mtu sahihi kwa uwezo na ujuzi wake katika masuala ya sheria na Katiba kutupatia katiba iliyo bora.
Ninaamini Prof. Kabudi ni mtu sahihi kabisa wa kutupatia katiba bora.