Prof Kabudi ni mtu ambaye ukimwambia aelezee ubora au faida za Nzi ni nyingi kuliko Nyuki anaweza shawishi watu wengi

Sodoku

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2016
Posts
1,271
Reaction score
2,903
Ni moja katika ya ma profesa wachache wenye kujua kuzungumza na kujua kuchezea lugha ya Kiswahili. Huwa namsifu.

Ni profesa ambaye unaweza ukampa kazi awaelezee watu faida za kufuga Nzi ni nyingi kuliko kufuga Nyuki. Na akaelezea kwa mbwembwe sana na wengi wakafurahia sana na kuanza kuangalia namna ya kufuga Nzi.

Ndivyo alivyo. Ila kwa yeye kama yeye sidhani kama ana kitu anasimamia. Sidhani. Umri umeenda anaangalia kwa haraka haraka tu ataishije na kustaafu.
 

Huyu ndie alitoa macho na kueleza dawa ya Madagascar itakavyo kuwa suluhisho la Uviko duniani... akapewa na ndege kwenda kuleta ili watanzania masikini wanywe wapone...
Alisema yeye alitolewa na Mwendazake majalalani
Ni yeye alikuwa akisimama anaelezea jinsi alivyo makini kupambana kunegotiate na mabeberu katika mikataba ya makinikia.

Yuko sirias na kwa kutoa macho sana ukimtazama anavyoongea.. unaweza kumuamini kama na wewe hauko makini.
 
Maana yake anakwenda na upepo hata alipokuwa anapitia kitabu cha Sokoine ,maeneo yanayo mkwaza bosi wake wa sasa alikuwa anayaruka kukwepa lawama.


TOKA MAKTABA :

 
Katika sifa zote ambazo anazo,ziwe nzuri au mbaya,kutoka kwake ambacho ninamkubali ni kiingereza chake.

Huyu jamaa kwenye yai Hana mpinzani bwana. Kabudi anatema yai kama Benjamin mkapa enzi zake. Sisi wengine tukiongea kiingereza tunakitafsiri kwanza kichwani kabla ya kukitoa mdomon na Kuna muda tunachapia(mfano mama wa kugalagala waziri wa afya dada Jeni) ila kabood anaongea kingereza kama kiswahili au kimakonde asee!!

Kwenye lugha ya kiingereza nampa 100/100.
 
Kwani we unafikiri nzi angetulia na kusoma asingekuwa na uwezo mkubwa wa kuzalisha asali kuliko nyuki!?
 
Nimekumbuka kwenye viunga vile pale Mlimani. Enzi za Kunji, Odwang Odwaa. Gone are the days.

Kuhusu mada: Proffesa amebarikiwa kipaji cha kueleza, kushawishi n kufundisha. Sema toka aje kwenye siasa binafsi simwelewagi. 😁
 
Iliwaponya wengi wakiwemo Mwenyekiti wa Chadema na mwanawe πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Acha kutudanganya wewe!

Hii dawa tuliambiwa inapelekwa NIMR hadi leo hakuna findings zozote za kusupport ilikuwa na matokeo dhidi ya kirusi kile.

Aliishia kunywa Kabudi na kina Jiwe kwa siri.
 

Sidhani kama anamfikia marehemu Augustine Mahiga...
 
Prof. Kabudi hana molali tena, maana alidhalilishwa sana na Samia wakati ule anatumbuliwa.
 
Ni profesa ambaye unaweza ukampa kazi awaelezee watu faida za kufuga Nzi ni nyingi kuliko kufuga Nyuki. Na akaelezea kwa mbwembwe sana na wengi wakafurahia sana na kuanza kuangalia namna ya kufuga Nzi.
Basi pia anaweza kuwa tapeli..maana matapeli wanaweza kukuaminisha kitu ambacho sicho.
 
Hili zee linaaa sana

Wakati linafundisha chuo
Tofauti na sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…