May 24, 2020
Dar es Salaam, Tanzania
Prof. Palamagamba Kabudi amesema ametumwa na Mh. Rais John Magufuli kuwashukuru waTanzania wote kwa maombi yao kipindi hiki cha janga la corona.
Prof. Palamagamba Kabudi akisoma ujumbe wa Rais unaosema alipoamua kutofunga nyumba za ibada wala kuifunga nchi kwa lockdown ni kuwa hakuyasema yeye kama binadamu (Mh.Rais) aliyeumbwa kwa nyama na damu bali alipata ujasiri na imani hiyo toka kwa Mungu. Kwani Mungu alimleta afanye kazi hiyo kama Musa alivyofanya kazi ya kuwavusha wana wa Israeli wavuke salama bahari ya Shamu kuwaepuka askari wa Farao.
Haikuwa uamuzi mdogo kwani kwa mujibu wa wataalamu idadi ya waTanzania zaidi ya 100,000 walitabiriwa lazima wafe kwa gonjwa la corona. Hivyo kutofunga Dar es Salaam wala Makanisa, Misikiti, Mahekalu na Masinagogi uamuzi huo ulikuwa mzito lakini Mungu ashukuriwe idadi ya vifo kutokana na corona ipo ndogo kabisa na vile ilivyotabiriwa kwa kweli ipo mbali sana na 100,000.
Mh. Rais anawaomba na kuwashukuru wa Tanzania walioomba Ijumaa, Jumamosi na Jumapili na waendelee kufanya hivyo kwa Mungu na kuliombea Taifa , anahitimisha Prof. Kabudi akiwakilisha Salaam za Mh. Rais kwa waTanzania.