Prof Kitila: Bajeti ya 2025|26 miradi mikubwa itatekelezwa kwa PPP

John Paul The Second

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2024
Posts
298
Reaction score
343

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema Bajeti ya mwaka 2025/2026 kipaumbele kikubwa kitakuwa ni utekelezaji wa miradi mikubwa kwa ushirikiano na Sekta Binafsi na Umma (PPP), ili kukuza uchumi kwa kasi.

Prof. Kitila Mkumbo, amesema hayo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bajeti ya Bunge ambapo amenukuu kanuni ya 113(1) na (2) ya kanuni za kudumu za Bunge iliyochapishwa Februari 2023, ambapo mapendekezo hayo yanawasilishwa kwa kamati ili kukusanya maoni kutoka kwa wabunge wakati wa maandalizi.

Amesema Serikali imejipanga kutumia mfumo wa PPP katika utekelezaji wa miradi mikubwa, hivyo katika bajeti ijayo wataweka nguvu huko kibajeti.

"Katika mwaka wa fedha 2025/26 kipaumbele cha bajeti kitaelekezwa kwenye PPP kwani ndio njia inayoweza kutekeleza miradi mikubwa inayochochea ukuaji wa uchumi na maendeleo," amesema.

Amesema mapendekezo hayo yameweka mazingira ya mpango wa maendeleo wa taifa, unaozingatia kuimarisha uwekezaji katika sekta mbalimbali, kujenga uchumi imara, kuongeza uzalishaji wa viwanda na kuboresha huduma za umma.

“Mapendekezo ya mpango wa maendeleo wa taifa wa 2025/26 yanaongozwa na dira ya maendeleo ya taifa 2025, ambayo inalenga kuiweka Tanzania kati ya nchi za kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 na kufikia viwango vya juu vya maendeleo ya binadamu,” amesema.

Soma Pia: Miradi ya PPP iliyopo katika tovuti ambayo yahitaji wawekezaji wa nje, kwanini wawekezaji wakimbilia Tanesco pekee ambayo haimo hata kwenye orodha?

Waziri Kitila amesema mapendekezo hayo yanajikita katika kuendeleza na kutekeleza mipango ambayo inatoa matokeo katika maeneo matano ya kipaumbele yaliyoainishwa katika mpango wa tatu wa miaka mitano.

Pia ametaja maeneo muhimu ambayo yatatekelezwa kwa mfumo wa PPP ni miundombinu ya usafiri na uzalishaji wa viwanda.

Amongeza kuwa jumla ya miradi 17 bora imepangwa kutekelezwa katika mwaka ujao wa fedha, huku akibainisha mafanikio kutoka kwa mpango wa sasa wa maendeleo wa 2023/24.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Oran Njeza ameipongeza serikali kwa kuja na mpango huo na kwamba matarajio yao ni kuona miradi inatekelezwa kwa ufanisi.

PPP iliyochini ya kituo cha Ubia nchi PPP-CETRE chini ya Mkurugenzi wake Bw David Kafulila na katika Serikali ya Sita ya Rais Samia Suluhu Hassan wameonesha wazi nchi inaweza kutekeleza miradi mingi na mikubwa bila kutumia Kodi Wala Mikopo toka katika taasisi na mashirika tofauti tofauti ya ndani na nje ya nchi kwenye miradi hasa yenye sura ya kibiashara na hivyo kuopa nafuu nchi kutekeleza miradi mingine isiyo na sura hiyo ya kibiashara.

======================

Minister: PPP projects crucial in next Budget​

Prof. Kitila Mkumbo, the Planning and Investment state minister in the President’s Office

THE government will prioritise the implementation of flagship projects in collaboration with the private sector to significantly boost the economy during fiscal 2025/26.

Prof. Kitila Mkumbo, the Planning and Investment state minister in the President’s Office, stated this position at a presentation to the Budget committee of the National Assembly here on Thursday, citing rule 113(1) and (2) of parliamentary standing orders published in February 2023, where the proposals are being submitted to the committee to gather feedback from MPs during the preparation process.

He said that the government’s focus on flagship projects reflects a commitment to leveraging public-private partnerships for sustainable economic growth and development prospects.
The proposals set the stage for the national development plan, focusing on enhancing investments across various sectors, creating a resilient economy, increasing industrial production and improving public services.

“The proposals for the national development plan for 2025/26 are guided by the national development vision 2025, which aims to position Tanzania among middle-income countries by 2025 and achieve high human development standards,” he stated.
These proposals concentrate on developing and implementing initiatives that yield results in five priority areas outlined in the third five-year plan, he said, citing key areas as enhancement of the transport infrastructure and industrial production.
A total of 17 flagship projects are planned for execution in the upcoming financial year, he said, highlighting achievements from the current development plan for 2023/24.

Positive trends in the global scenario and national economy include a decrease in inflation, with effective implementation of projects depending on robust collaboration with the private sector to ensure that projects produce substantial outcomes, he emphasised.

The minister was accompanied by the permanent secretary, Dr Tausi Kida and key officials of the Planning Commission, while Oran Njeza (Mbeya Rural), the committee chairman, hailed the proposals.

They included supplementary information on progress made in development projects undertaken in partnership with the private sector, he said.
In a related development, members of the Administration, Constitution and Law standing committee chaired by Florent Kyombo(Nkenge) discussed a report on the Planning Commission and ministerial performance along with drafting the Development Vision 2050, following an update on progress made.
 
Lakini Kwa nchi kama zetu hizi za 10% PPP haiwezi kukubalika na wenye mamlaka, Watu walizoea kutumia pesa ya Serikali kujenga miradi na kuzigeuza kuwa zao na hata wakikupa kazi lazima uwaache na chochote,PPP mpaka ipenye sio rahisi
Kila kitu kinawezekana kabisa kama tutaamua kama Taifa,
DP WORLD wametusaidia sana pale bandarini Kuna watu walikuwa wanapiga hadi 100mil kwa siku
 
KAFULILA naona anapata nguvu kila kukicha aangaliwe sana
 
PPP inaweza kuifanya Tanzania kama US kwa mwaka mmoja tu lakini lazima nchi iwe na utulivu wa kisiasa
Nchi yetu ni tulivu na ina utulivu mkubwa wa kisiasa.nina imani kubwa sana na PPP hasa kutokana na uwepo wa Mzalendo wa kweli, mchapakazi na kijana mwenye maono ,uadilifu na weledi Mheshimiwa David Kafulila.
 
Lakini Kwa nchi kama zetu hizi za 10% PPP haiwezi kukubalika na wenye mamlaka, Watu walizoea kutumia pesa ya Serikali kujenga miradi na kuzigeuza kuwa zao na hata wakikupa kazi lazima uwaache na chochote,PPP mpaka ipenye sio rahisi
Mbona tayari kuna miradi imeshasainiwa? Mingine zamanai sana kabla ya Kitila?

Unajuwa daraja la Kigamboni lilianza kujengwa enzi ya Kikwete kwa aina hiyo hiyo.
 
PPP sioni ikipata mwitikio mzuri hasa ukizingatia anaweza kuja kiongozi anayejifanya mzalendo akaishia kuharibu makubaliano.
Mimi naona PPP inaweza ikapunguza sana Upigaji wa pesa za Umma kama itapewa nguvu inayostahili
 
Mbona tayari kuna miradi imeshasainiwa? M9ingine zamanai sana kabla ya Kitila?

Unajuwa daraja la Kigamboni lilianza kujengwa enzi ya Kikwete kwa aina hiyo hiyo.
Kigamboni haikuwa 100% PPP hili nafahamu vizuri
 
Lakini Kwa nchi kama zetu hizi za 10% PPP haiwezi kukubalika na wenye mamlaka, Watu walizoea kutumia pesa ya Serikali kujenga miradi na kuzigeuza kuwa zao na hata wakikupa kazi lazima uwaache na chochote,PPP mpaka ipenye sio rahisi
Umeongea vice versa
 
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema Bajeti ya mwaka 2025/2026 kipaumbele kikubwa kitakuwa ni utekelezaji wa miradi mikubwa kwa ushirikiano na Sekta Binafsi na Umma (PPP), ili kukuza uchumi kwa kasi.

Prof. Kitila Mkumbo, amesema hayo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bajeti ya Bunge ambapo amenukuu kanuni ya 113(1) na (2) ya kanuni za kudumu za Bunge iliyochapishwa Februari 2023, ambapo mapendekezo hayo yanawasilishwa kwa kamati ili kukusanya maoni kutoka kwa wabunge wakati wa maandalizi.

Amesema Serikali imejipanga kutumia mfumo wa PPP katika utekelezaji wa miradi mikubwa, hivyo katika bajeti ijayo wataweka nguvu huko kibajeti.

"Katika mwaka wa fedha 2025/26 kipaumbele cha bajeti kitaelekezwa kwenye PPP kwani ndio njia inayoweza kutekeleza miradi mikubwa inayochochea ukuaji wa uchumi na maendeleo," amesema.

Amesema mapendekezo hayo yameweka mazingira ya mpango wa maendeleo wa taifa, unaozingatia kuimarisha uwekezaji katika sekta mbalimbali, kujenga uchumi imara, kuongeza uzalishaji wa viwanda na kuboresha huduma za umma.

“Mapendekezo ya mpango wa maendeleo wa taifa wa 2025/26 yanaongozwa na dira ya maendeleo ya taifa 2025, ambayo inalenga kuiweka Tanzania kati ya nchi za kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 na kufikia viwango vya juu vya maendeleo ya binadamu,” amesema.

Waziri Kitila amesema mapendekezo hayo yanajikita katika kuendeleza na kutekeleza mipango ambayo inatoa matokeo katika maeneo matano ya kipaumbele yaliyoainishwa katika mpango wa tatu wa miaka mitano.

Pia ametaja maeneo muhimu ambayo yatatekelezwa kwa mfumo wa PPP ni miundombinu ya usafiri na uzalishaji wa viwanda.

Amongeza kuwa jumla ya miradi 17 bora imepangwa kutekelezwa katika mwaka ujao wa fedha, huku akibainisha mafanikio kutoka kwa mpango wa sasa wa maendeleo wa 2023/24.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Oran Njeza ameipongeza serikali kwa kuja na mpango huo na kwamba matarajio yao ni kuona miradi inatekelezwa kwa ufanisi.

PPP iliyochini ya kituo cha Ubia nchi PPP-CETRE chini ya Mkurugenzi wake Bw David Kafulila na katika Serikali ya Sita ya Rais Samia Suluhu Hassan wameonesha wazi nchi inaweza kutekeleza miradi mingi na mikubwa bila kutumia Kodi Wala Mikopo toka katika taasisi na mashirika tofauti tofauti ya ndani na nje ya nchi kwenye miradi hasa yenye sura ya kibiashara na hivyo kuopa nafuu nchi kutekeleza miradi mingine isiyo na sura hiyo ya kibiashara.

Master Kitila mkumbo
 
Back
Top Bottom