Prof Kitila: Bajeti ya 2025|26 miradi mikubwa itatekelezwa kwa PPP

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema Bajeti ya mwaka 2025/2026 kipaumbele kikubwa kitakuwa ni utekelezaji wa miradi mikubwa kwa ushirikiano na Sekta Binafsi na Umma (PPP), ili kukuza uchumi kwa kasi.

Prof. Kitila Mkumbo, amesema hayo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bajeti ya Bunge ambapo amenukuu kanuni ya 113(1) na (2) ya kanuni za kudumu za Bunge iliyochapishwa Februari 2023, ambapo mapendekezo hayo yanawasilishwa kwa kamati ili kukusanya maoni kutoka kwa wabunge wakati wa maandalizi.

Amesema Serikali imejipanga kutumia mfumo wa PPP katika utekelezaji wa miradi mikubwa, hivyo katika bajeti ijayo wataweka nguvu huko kibajeti.

"Katika mwaka wa fedha 2025/26 kipaumbele cha bajeti kitaelekezwa kwenye PPP kwani ndio njia inayoweza kutekeleza miradi mikubwa inayochochea ukuaji wa uchumi na maendeleo," amesema.

Amesema mapendekezo hayo yameweka mazingira ya mpango wa maendeleo wa taifa, unaozingatia kuimarisha uwekezaji katika sekta mbalimbali, kujenga uchumi imara, kuongeza uzalishaji wa viwanda na kuboresha huduma za umma.

“Mapendekezo ya mpango wa maendeleo wa taifa wa 2025/26 yanaongozwa na dira ya maendeleo ya taifa 2025, ambayo inalenga kuiweka Tanzania kati ya nchi za kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 na kufikia viwango vya juu vya maendeleo ya binadamu,” amesema.

Soma Pia: Miradi ya PPP iliyopo katika tovuti ambayo yahitaji wawekezaji wa nje, kwanini wawekezaji wakimbilia Tanesco pekee ambayo haimo hata kwenye orodha?

Waziri Kitila amesema mapendekezo hayo yanajikita katika kuendeleza na kutekeleza mipango ambayo inatoa matokeo katika maeneo matano ya kipaumbele yaliyoainishwa katika mpango wa tatu wa miaka mitano.

Pia ametaja maeneo muhimu ambayo yatatekelezwa kwa mfumo wa PPP ni miundombinu ya usafiri na uzalishaji wa viwanda.

Amongeza kuwa jumla ya miradi 17 bora imepangwa kutekelezwa katika mwaka ujao wa fedha, huku akibainisha mafanikio kutoka kwa mpango wa sasa wa maendeleo wa 2023/24.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Oran Njeza ameipongeza serikali kwa kuja na mpango huo na kwamba matarajio yao ni kuona miradi inatekelezwa kwa ufanisi.

PPP iliyochini ya kituo cha Ubia nchi PPP-CETRE chini ya Mkurugenzi wake Bw David Kafulila na katika Serikali ya Sita ya Rais Samia Suluhu Hassan wameonesha wazi nchi inaweza kutekeleza miradi mingi na mikubwa bila kutumia Kodi Wala Mikopo toka katika taasisi na mashirika tofauti tofauti ya ndani na nje ya nchi kwenye miradi hasa yenye sura ya kibiashara na hivyo kuopa nafuu nchi kutekeleza miradi mingine isiyo na sura hiyo ya kibiashara.

Ndio mikakati ya kubinafsi nchi , na njia za kufua nguo chafu ili ziwe safi
 
Naiona Tanzania ya baraka sana hapo baadae
 
PPP inaweza kuifanya Tanzania kama US kwa mwaka mmoja tu lakini lazima nchi iwe na utulivu wa kisiasa
Hao watu wa kuifanya iwe kama US ni hawa tulionao madarakani? Wanyiramba? Mkoa wao umewashinda wamekimbilia vyeo kucha kupiga domo tuu.
 
Ukolini mambo leo huathiri maendeleo ya watu wake endepo viongozi wa kitaifa watakutana na viongozi wa nchi zingine kuhusu uweekezaji kwa kwa masilahi binafsi na kidogo sana kuhusu maendeleo ya jamii.

Swali fikirishi hiyo miradi ya ppp wahusika ni wazawa ama ni kutoka mataifa ya nje, kama ni wazawa naipa serikali kongole lakini kama ni raia wa kigeni nitawazomea.

Kama hawata weka uwiano ya miradi ya ppp, kwa kwa wazawa na wageni wanao dhani watawezesha kuendeleza hiyo miradi kumbe watakuwa wanaua uchumi wa Tanzania kwa upumbavu wao
 
Ukolini maendeleo huathiri maendeleo ya watu wake endepo viongozi wa kitaifa watakutana na viongozi wa nchi zingine kuhusu uweekezaji kwa kwa masilahi binafsi na kidogo sana kuhusu maendeleo ya jamii.

Swali fikirishi hiyo miradi ya ppp wahusika ni wazawa ama ni kutoka mataifa ya nje, kama ni wazawa naipa serikali kongole lakini kama ni raia wa kigeni nitawazomea kama hawata weka uwiano ya miradi ya ppp na hao wageni wanao dhani watawezesha kuendeleza hiyo miradi kumbe watakuwa wanaua uchumi wa Tanzania kwa upumbavu wao
Kwenye PPP kila mmoja anaruhusiwa awe wa ndani au nje
 
Nalifahamu hilo, je unafahamu kwamba vitu vingi tunavyo tumia kwa sasa na huduma hatuzalishi wenyewe, (we consume what we do not produce)

Watu tunao wapa dhamana wengi wanaahirisha kufikiri kizalendo, a.k. kujizima data

Why do we fail to manage our own affairs, and our own businesses

Je ppp unadhani ndiyo suluhisho kwa hapa Tanzania mimi nasema hapana hiyo miradi itaendelea kufa tu

Tuna mazingira mabovu ya biashara and unworking government machineries, ndiyo maana narudia kwakusema ppp kwa Tanzania haiwezi kufanikiwa

Na nafahamu kwamba asilimia 80 ya mafanikio kwenye biashara inamtegemea mjasiriamali na aslimia 20 ni mjasiriamali na yanayomzungu na hayo yanayo mzunguka kwa hapa Tanzania yana nguvu hata kuua biashara

I have the unlocking codes for the 20%
 
Mimi nadhani tusijigeuze shehe Yahya Wacha tuone mpaka mwisho wake
 
Back
Top Bottom