Tetesi: Prof. Kitila Mkumbo kuchuana vikali na Nyalandu jimboni

Tetesi: Prof. Kitila Mkumbo kuchuana vikali na Nyalandu jimboni

kawaida ni CCM kwa CCM hivyo hakuna cha kupoteza hapo...
 
Kakonko kwa CDM ana andaliwa Prof wa elimu akalikomboe jimbo....
Mbeya mjini ana andaliwa Dr. naibu spika akalikomboe...
na majimbo mengine kama ya DSM wana fanya maendeleo ya hali na mali ili baadae wawe na hoja nzito zidi ya upinzani na kurudisha jiji kwa watawala... Chuga napo hali ni ile ile kama DSM... moshi wamemtumia mpinzani akasawazishe mambo... 2020 kura nyingi za urais zitaongezeka kwa watawala na kupungua kwa wapinzani kwa mikakati waliyo nayo na CDM wana jifanya kama vipofu... waamke
 
Hizo ni zama za kaleeeeeeee

Ni nondo zitawamaliza huko..
Na sio hongo... mnalo bora msiweke mgombea Kitila akigombea eeeeeeh
Zama za sasa ni
[emoji379][emoji379][emoji379]Pyu.. pyu.. pyu.. pyu..
 
Hayawi hayawi, sasa yamekuwa. Kile kitendawili kigumu kilichokuwa kimekosa majibu sasa majawabu yake yako bayana! Kuna kila aina ya dalili CCM wanamuandaa Prof Kitila Mkumbo kuchauana vikali na Dr Lazaro Nyalandu katika uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika kumchagua mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini baada ya Dr Nyalandu kujiondoa CCM na kujiunga CHADEMA hivi karibuni.

Wataalamu wa masuala ya siasa wanabainisha kuwa CCM wamejithathmini na kuona wamteue Prof Kitila kuwa mgombea wao ili achuane na mgombea wa upinzani, Dr Nyalandu. Sababu zinazopelekea CCM walenge kumteua Prof Kitila ni kutokana na hali ya siasa za Kanda ya Kati ambazo hazitabiriki hata kidogo. Inadhaniwa Prof Kitila ana uwezekano wa kumuangusha Dr Nyalandu katika uchaguzi huo kwa kuwa bado ana chembechembe za upinzani, hivyo kuweza kujizolea mashabiki kutoka upande wa upinzani pamwe na upande wa CCM.

Aidha,upande wa CHADEMA nao wanatamba kuibuka washindi katika jimbo hilo kutokana na kuwa na hazina nzuri ya wafuasi, huku wakitarajia kupata "kura za chuki" za kutosha kutoka kwa wanaCCM, hasa wale wanaokerwa jinsi nchi inavyotawaliwa kwa sasa.

MAONI YANGU
Mimi kete yangu naitupia kwa Dr Nyalandu kuibuka na ushindi katika uchaguzi huo mdogo kwa kuwa bado ana wafuasi wa kutosha kutoka upande wa CCM, hasa wale wasioridhishwa jinsi CCM inavyomwandama Dr Nyalandu na kashfa za kutunga huku wakijua fika utumishi wa Dr Nyalandu haujawahi kuwa na doa lolote.

Je, wewe dau lako unalitupia kwa nani na kwa sababu gani? Toa maoni yako sasa!
Nyamaza kimya kama huijui Singida hilo haliwezi tokea na kama wanataka kuliweka jimbo rehani wampeleke Kitila. Kumbuka jimbo la nyalandu liko Singida vijijini ambapo kwa asili ni Wanyaturu, Kumbuka prof Kitila ni mnyiramba anaetoka wilaya ya iramba. Sasa umeambiwa hakuna wanyaturu kutoka jimbo hilo wenye uwezo hadi waazime MTU kutoka jimbo lingine? Hapana haitotokea kwani hata Elibariki Kingu alishinda ubunge wangu unyaturuni sababu alizaliwa huko alisomea huko na anamakazi huko.
 
Mkuu sihitaji nguvu kubwaaaa kukuaminisha ufisadi wa Nyarandu? Tuache siasa za ushabiki kama Premier League au Yanga na Simba.

Vitu viko wazi kama vazi la ma.la.ya
Dr Nyalandu aliwahi kushtakiwa mahakama ipi kwa UFISADI?
 
Kitila Mkumbo Pr, akichukua fomu ya kugombea singida kaskazin , nitakuja kukupigia kampen na ninaamini ndiye mtatuzi wa matatizo hapo.

Pr ,Kitila ni mtu ambaye yupo smart na anafanya research na kutambua chanzo cha matatizo katika utendaji kwa mana
Alipokuwa cdm, cdm ilikuwa moto kwanini jibu ni dogo sana ,huyu mh alikuwa haonekani lakin kazi yake ilikuwa kubwa sana kufanya tafiti na kuwaletea viongozi wa juu wa cdm ,kama Zitto, Mbowe na Slaa.

Pr, Kitila ndiye aliyekuwa anafundisha vijana kujenga hoja pale cdm , na ikafikia mahali hata serikali awamu ya nne kuwaagopa wadogo kama ,Zitto, Mnyika na Mdee. Lkn leo baada ya baba kuondoka angalia uwezo wao ulivyopomoko

Angalia pia Udsm alivyofanya kazi iliyotukuka.


Singida Kaskazin inamhitaji zaid Mkumbo kuliko yeye anavyohitaji
Mkuu mbona unaandika kama vile unaghani mashairi? Kulikoni?
 
Atashinda nyalandu, atatangazwa mkumbo
Kwa nini!
Hujaona ya tumbili
Umafia tu
 
Back
Top Bottom