Tetesi: Prof. Kitila Mkumbo kuchuana vikali na Nyalandu jimboni

Tetesi: Prof. Kitila Mkumbo kuchuana vikali na Nyalandu jimboni

Utafiti wake sijauona mimi, au anafanyia kwenye karatasi?
Tafuta Mkuu au unadhani Mbowe atakuletea tafiti alizofanya Prof Mkumbo wakati alimbatiza jina la Msaliti ili alinde maslahi binafsi ya Chagademus & Pliers?
 
Kitila Mkumbo Pr, akichukua fomu ya kugombea singida kaskazin , nitakuja kukupigia kampen na ninaamini ndiye mtatuzi wa matatizo hapo.

Pr ,Kitila ni mtu ambaye yupo smart na anafanya research na kutambua chanzo cha matatizo katika utendaji kwa mana
Alipokuwa cdm, cdm ilikuwa moto kwanini jibu ni dogo sana ,huyu mh alikuwa haonekani lakin kazi yake ilikuwa kubwa sana kufanya tafiti na kuwaletea viongozi wa juu wa cdm ,kama Zitto, Mbowe na Slaa.

Pr, Kitila ndiye aliyekuwa anafundisha vijana kujenga hoja pale cdm , na ikafikia mahali hata serikali awamu ya nne kuwaagopa wadogo kama ,Zitto, Mnyika na Mdee. Lkn leo baada ya baba kuondoka angalia uwezo wao ulivyopomoko

Angalia pia Udsm alivyofanya kazi iliyotukuka.


Singida Kaskazin inamhitaji zaid Mkumbo kuliko yeye anavyohitaji
tatizo mnasahau kuwa kitila katokea act wazalendo kwenda ccm. kama alikuwa smart tueleze ni vipi kaisaidia act wazalendo
 
umpigie kampeni ya nini??? Kwani ninyi huwa mnategemea kura kuchukua madaraka???!
 
1. Mkumbo Kitila HAJAWAHI kuwa na "chembechembe" za UPINZANI. Ni ccm DAMU tangu zamani.
2. Mkumbo Kitila anatoka NDAGO (Singida Kusini), kugombea Singida Kaskazini ni kujitangaza KUSHINDWA kabla ya ushindani kuanza.
3. Itakuwa ni ushindani wa Kitila "aliyeTOKA" upinzani kwenda CCM na Nyalandu aliyetoka CCM kwenda upinzani. Watakuwa wanajibu swali la Paskali wa JF: "Yupi mzuri, shetani aliyebadilika kuwa Malaika, au Malaika aliyebadilika kuwa shetani?"
4. Inawezekana pia wana Singida wakapiga kura "KUMPA ZAWADI TLS" .....
Kitila hatoki Ndago. Ila anatokea Mtowa karibu na Shelui
 
Weka ufisadi wake tuuone. Acha kuchekea uvunguni huku unatoa udenda.
Siweki ufisadi wake sasahivi lakini bwana yule anatumiwa na Shirika flani ya kijasusi kwa iyo apo ni wasiwasi wa uzalendo tu. Uzi upo humu JF tena kitambo wakati anavaa kijani
 
Siweki ufisadi wake lakini bwana yule anatumiwa na Shirika flani ya kijasusi kwa iyo apo ni wasiwasi wa uzalendo tu. Uzi upo humu JF tena kitambo wakati anavaa kijani
Hahahahaaa! Ndiyo ninyi mkimuona mwehu anaongea kiingereza mnasema ni shushushu!
 
Back
Top Bottom