Prof. Kitila Mkumbo: Pato la kila Mtanzania ni milioni 2.8

Prof. Kitila Mkumbo: Pato la kila Mtanzania ni milioni 2.8

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo amesema Ripoti ya Hali ya Uchumi Nchini imeonesha Pato la Mtanzania mmojammoja (GDP Per Capital Income) limeongezeka kutoka USD 399.5 (Tsh. 322,397) kwa thamani ya dola mwaka 2000 hadi kufikia USD 1,200 (Tsh. 2,880,000) Mwaka 2022.

Akiongea leo Jijini Dar es salaam Mkumbo amesema “Tuelewane hapa tukisema hivi Watu wanasema mbona hiyo hela sina mfukoni, hesabu zake unazipata kwa kukusanya mapato ya Nchi nzima Watu wote milioni 61.7 mapato yao yote ambayo yanakaribia kufikia Tsh. Trilioni 141 unagawanya kwa idadi ya Watu ndio unapata pato la kila Mtanzania mmojammoja”
Kitila fanya mpango za kwangu nizipate kabla ya krisimass nitakushukuru Sana.
 
Pato la Mo-Dewji, Bakhresa na mimi unajumlisha halafu unagawa na watanzania , huku Mo peke yake unakuta ni pato la watanzania malofa 10m.

Tuache porojo na akili za kufikiria uchaguzi, tufanye hesabu sahihi ya idadi ya masikini, kipato chao na nini kufanyike ili kuwatoa kwenye umasikini.
Jamani iko hivi:
Tuchukulie kweli Mko watatu tu-Wewe Bakhresa na Mo.

Maana yake ninini?

Ni kwamba Ukigawa Jumla ya Mapato yenu-Wewe utakuwa na Value ya Takribani 300B.

Lakini kimsingi utakuwa huna hata Kumi Mfukoni!

ISIPOKUWA:
-Huduma za Hospital utakuwa unatibiwa St Thomas.

-Barabara ya kwenda nyumbani kwako ni Lami.

-Ulinzi ni Warda Gusrd.

Na vitu kama hivo.

Matajiri wazawa wakiongezeka wanasaidia Huduma za kijamii kuwa Bora sana licha ya kwamba maisha ya mtu mmoja mmoja yanaweza yasiwe na Cash huko Bank.

Chukua mfano wa Nchi kama Libya kipindi cha Ghaddafi.

Au Sweden na Nyinginezo.

Mfano Mwingine ni kwamba Iwapo Bandari itatuwezesha kupata Mapato ya 2T kwa Mwezi pekee basi ni Rahisi Serikali kuacha watu wa Mitaji Midogo wasilipe kodi ili wakue.

Prof kitila Mkumbo yuko sahihi lakini kwa vile watu hawana Pesa mfukoni basi wanahasira!!
 
Back
Top Bottom