Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Profesa Kitila Mkumbo akizungumza na Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri nchini kuhusu Dira ya Taifa ya Maendeleo na nafasi yao katika kuwezesha biashara nchini. Alisisitiza umuhimu wa Viongozi wa serikali kuweka mazingira wezeshi kwa vijana kufanya biashara. Katika kuzungumzia jambo hili Mkumbo alisema:
Hakuna nchi yoyote iliyoendelea bila kufungua mazingira rafiki ya biashara. Tukiendelea kuwa na mazingira magumu ya biashara katika nchi yetu tusahau kuondokana na umaskini, kwa sababu hatuwezi kuwawezesha wananchi kutengeneza kipato.
Hivi saivi tunazungumzia asilimia 76 ya Watanzania wapo chini ya miaka 35, hii nchi ni nchi ya watoto na vijana wadogo. Sasa young people hawa tutawaajiri wapi?
Njia pekee ya kuwakomboa ni lazima tuweke mazingira mazuri ya Biashara na Uwekezaji ili wachakarike. Sasa hii tabia yetu wanaanza tu kabiashara umeshamminya hasogei kila mtu amemsogelea pale.
PIA SOMA- Prof. Kitila Mkumbo: Pato la kila Mtanzania ni milioni 2.8