Prof. Kitila Mkumbo: Vijana watengenezewe mazingira rafiki ya Biashara

Prof. Kitila Mkumbo: Vijana watengenezewe mazingira rafiki ya Biashara

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610


Profesa Kitila Mkumbo akizungumza na Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri nchini kuhusu Dira ya Taifa ya Maendeleo na nafasi yao katika kuwezesha biashara nchini. Alisisitiza umuhimu wa Viongozi wa serikali kuweka mazingira wezeshi kwa vijana kufanya biashara. Katika kuzungumzia jambo hili Mkumbo alisema:

Hakuna nchi yoyote iliyoendelea bila kufungua mazingira rafiki ya biashara. Tukiendelea kuwa na mazingira magumu ya biashara katika nchi yetu tusahau kuondokana na umaskini, kwa sababu hatuwezi kuwawezesha wananchi kutengeneza kipato.
Hivi saivi tunazungumzia asilimia 76 ya Watanzania wapo chini ya miaka 35, hii nchi ni nchi ya watoto na vijana wadogo. Sasa young people hawa tutawaajiri wapi?
Njia pekee ya kuwakomboa ni lazima tuweke mazingira mazuri ya Biashara na Uwekezaji ili wachakarike. Sasa hii tabia yetu wanaanza tu kabiashara umeshamminya hasogei kila mtu amemsogelea pale.
PIA SOMA
- Prof. Kitila Mkumbo: Pato la kila Mtanzania ni milioni 2.8
 
Ametengenezewa na dirisha dogo ikulu na kupewa sikio la karibu na Mh Raisi kwenye masuala ya "Uwekezaji"

"Uwekezaji" (Investments opportunities) huu unaowezeshwa kwa mgongo wa Vijana hao kwa kutwishwa madeni ya mbeleni huko(madeni ya mikopo)na madeni ya Taifa, hawapewi kipaumbele katika Uwekezaji kwenye nchi yao wenyewe mfano Public Private Partnership

Yaani ukiskia neno Mwekezaji ujue huyo ni mgeni!

Ukiskia Public ujue ndio huyu Kijana.

Ukisikia Private ujue ni Mzungu, Mhindi, Mwarabu na wageni wengine.
... na Ukisikia Partnership ni kwa wale wanaopendelewa kwasababu wapo tayari kutoa 10% Partner! Nasisitiza.

Sawa lakini
 
Watengenezewe na nani? Anayesababisha hayo mazingira magumu ni nani? Nchi imejaa utitiri wa kodi, tozo, vibali na upuuzi mwingine alafu waziri anaongea siasa tu. Pumbavu kabisa.
 
Watengenezewe na nani? Anayesababisha hayo mazingira magumu ni nani? Nchi imejaa utitiri wa kodi, tozo, vibali na upuuzi mwingine alafu waziri anaongea siasa tu. Pumbavu kabisa.
Na wanapokuja sehemu ya biashara ukaanza kuwapa uhalisia ni wabishi utadhani huwa mnakaa pamoja hapo ofisini, wabishi kama mashipa.
 
Back
Top Bottom